Naomba msaada wa kisheria kwa wizi wa fedha za wanafunzi-udom | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada wa kisheria kwa wizi wa fedha za wanafunzi-udom

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by WATSON, Jan 31, 2011.

 1. W

  WATSON New Member

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TAARIFA YA WIKILEAKS-UDOM
  HATIMA YA UDOSO-FEDERAION
  UTANGULIZI:
  Kwanza kabisa tunapenda kutoa pongezi kwa makamanda wote wapigania haki za msingi kwa wanafunzi wenzetu, tutakuwa wachoyo wa fadhira kama hatuto mpongeza mh. Leornad singo na waziri wake mkuu na baraza lake la mawaziri na serekali yake kwa ujumla wao.
  Kwa masikitiko makubwa duniani mpaka mbinguni kwa usaliti uliyo fanywa na unaoendelea kufanya na UDOSO-FEDERATION inayo ongozwa na mh. BAISI(RAIS) akisaidiwa na kibaraka wake wa karibu anayejiita GENERAL SECRETARY(GS) au WAZIRI MKUU wa udoso-federation mh. JOSEPH MARWA(B.COM HRM 3rd year) hawa wote hawajui majukumu yao kama viongozi wa kubwa katika serekali ya UDOM.
  Kabla hatujaenda kokote tujue UDOSO-FEDERATION ni serikali ya namna gani; hii ni serikali ya shirikisho inayo unganisha collage zote hapa UDOM. Lakini cha kushangaza UDOSO-FEDERATION ni serikali iliyo kufa kimahamuzi mpaka kiutendaji ndio maana inafikia hatua inashindwa kutoa mahamuzi yenye tija kwa maendeleo ya chuo chetu kwa taarifa hii na chelae kusema safari yao ya kwenda IKULU kuonana na MH. RAISI(JAKAYA KIKWETE) ilikuwa na agenda za siri juu ya mstakabali wa maisha yetu hapa chuoni na tabu zinazo tukabili sababu hawajaweza kutoa taarifa kwa UMMA wa wanaUDOM safari yao IKULU ilikuwana mantiki gani na kama ilikuwa na sababu za kiuwazi kwanini hawaja tupa taarifa hadi sasa(IKULU wameenda miezi miwili iliyopita)
  UDOSO-FEDERATION imekuwa ni serikali inayo dandia hoja kwa mbele na sio kuanzisha za kwao wenyewe kama serekali yenye nguvu kimaamuzi. MFANO; mgomo wa education & social science and humanities. UDOSO-FEDERATION haija husika hata chembe katika mafanikio ya madai yetu ambayo wao UDOSO-FEDERATION wa nasema hayana msingi hata tija,lakini yenyewe imekuwa ni serekali ya kutafuna FEDHA za wanafunzi kwa kufanya SAFARI NJE YA NCHI na kujilipa POSHO NYINGI.
  MADHUMUNI YA TAARIFA:
  Madhumuni ya taarifa hii ni kufanya ushawishi kwa wanafunzi wote wa UDOM kushinikiza UDOSO-FEDERATION kujiuzuru wenyewe bila ya nguvu ya UMA wa UDOM kutumia nguvu ya kuwaondoa kwa maandamano sababu niya tunayo na sababu tunayo na uwezo tunao na nguvu tunayo.sababu za kujiuzuru kwa UDOSO-FEDERATION ni kama zifuatovyo;
  · Ushiriki wa UDOSO-FEDERATION katika mgomo wa EDUCATION
  Ndugu wana UDOM nasikitika tena sana kuona UDOSO-FEDERATION walivyo wanafiki katika kuwapigania wafunzi wenzao. Ndio maana chuo chetu kina kithiri migomo kila kukicha sababu uongozi wa shirikisho hautatui matatizo ya wanafunzi. Ndio maana RAISI BAISI hawataki kumuona EDUCATION na hawatambui serekali yake na vibaraka wenzake akiwemo GS(JOSEPH MARWA) ndio maana tunaomba mstep down kwa hiari yenu wenyewe.

  · Ushiriki wa UDOSO-FEDERATION katika mgomo wa SOCIAL SCIENCE
  Hapa cha kushanga siku ya Tarehe 20/12/2010, siku ya mgomo wa wanaume wa social science RAISI (BAISI) na kibaraka wake WAZIRI MKUU wake (JOSEPH MARWA) walikuwa CLUB 84 wakati wanafunzi wenzao wakiwa katika harakati za kudai FIELD. Hawa jamaa ni vibaraka wa serikali ndio maana wameenda kuonana na RAISI bila taarifa tena kuna tetesi zinasema wamekwenda IKULU kwa kutumia FEDHA za UDOSO kufanya safari za KICHAMA.

  · MSTAKABALI WA UFISADI KATIKA UDOSO-FEDERATION
  Hapa napenda tuwekane sawa kuna mambo takribani 15 yanayo husiana na UFISADI katika UDOSO-FEDERATION ya Bwana Baisi(RAISI) na katibu wake mkuu(JOSEPH MARWA), ndio maana WIKILEAKS-UDOM imeyabaini na kujilidhisha,tena yapo mambo mengi sana wanayo fanya hawa jamaa wa UDOSO-FEDERATION tutayachambua moja moja mpaka wajiuzuru hawa vibaraka wa UTAWALA.
  (1)Safari ya NAIROBI(KENYA) ya kimichezo
  Nashindwa kuchelea kusema katibu mkuu(JOSEPH MARWA,B.COM HRM 3rd year) kujiuzuru kwa sababu amekwenda Nairobi kwenye safari ya kimichezo kimya kimya bila taarifa za kiofisi ndio maana safari yake inakadiriwa kugharimu kiasi cha million 8 za kitanzania.
  (2)kujilipa posho kwasiku 20000/= kama fedha ya mawasiliano kwa siku
  Nikiwa kama mwanaudom watu hawa kweli ni mafisadi kama kwa siku wanajilipa 20000,kwa mwezi ni laki sita pata mchanganua wa siku kwa semester mbili( siku 252 kwa mwaka) watu hawa mpaka uongozi wao unafika kikomo wanapata fedha kwa ajili ya mawasiliano ni milioni tano na arobaino elfu(5,040,000/= tu),sijui haya mawasiliano wana fanya na nani na kwamanufaa gani kama hawajui hakizao za kimsingi. Naomba wajiudhuru wenyewe bila nguvu ya uma kuchukua mkondo wake katika maamuzi.
  (3)kuandaa matamasha ya kifisadi ya kimichezo kwa siri kubwa kwa makusudi ya kifisadi;
  mfano: tamasha lililo fanyika KILIMANI linakadiliwa kutumia kiasi cha milioni 11 za wanafunzi tena watoto wa mkulima wakati kunawanafunzi takribani 192 hawajapata mikopo yao kama hii fedha wange kopeshwa hawa wanafunzi si ingekuwa bora zaidi kuliko hasara walioipata.
  (4)kupika safari na vikao visivyo kuwa na tija ili kujipatia posho.
  Mfano:
  · Safari ndani ya Dodoma perday ni 20000/=
  · Safari nje ya Dodoma perday ni 40000/=
  · Posho ya kikao kimoja perday ni 30000/


  (5)kupanda gharama za bidhaa madukani na vyakula cafeteria inasadikika kuwa UDOSO-FEDERATION wana pata 10% ya mapato.
  (6) inasadikika wamechoma ofisi ya UDOSO chimwaga kwaajili ya kupoteza ushaidi wa nyaraka zao za kifisadi hasa mapato na matumizi.
  (7) inasadikika MH. BAISI(RAISI) amenunua gari aina ya COSTA inayofanya safari DODOMA-MOROGORO yenye namba T 123BACU,kwa kutumia fedha za wanafunzi kujinufaisha wenyewe.
  (8)wanafanya mkakati wa kuandaa serikali ya UDOSO-FEDERATION na serikali ya social science ilikupunguza makali ya collage ya social science katika kudai haki zao vile vile kuficha WIZI wanaoufanya ofisini.mkakati huo unafanywa na katibu mkuu(JOSEPH MARWA,B.COM HRM)
  (9)Katibu mkuu na Raisi UDOSO-FEDERATION kung'ang'ania fedha za takribani milioni 18 za collage ya social science kutofanya mambo yake yanayo husu utendaji mfano: kununua vifaa vya kimichezo. Kama vile kulipia BILL YA DSTV.nk

  (10) kutumia fedha za wanafunzi kwenza Dar-es-salaam kwenye shughuli za chama IKULU,kuonana na RAISI bila kutupa ripoti nini walicho kwenda kuzungumza na RAISI KIKWETE IKULU. Huku mtendaji mkuu wa safari hivyo mpaka kufanikiwa alikuwa ndugu terry ambaye ni kada maarufu sana wa CCM.
  WALIOKWENDA HIYO SAFARI NI:
  BAISI(RAISI FEDARATION).
  JOSEPH MARWA(KATIBU MKUU FEDERATION)
  SUMERA FYEKA(MJUMBE WA CCM)
  NA WENGINE(WAJUMBE WA CCM)

  MAADHIMIO
  · Kufanya mapinduzi ya UDOSO-federation ndani ya masaa 48 kuanzia sasa.sababu hatuoni kazi yao bali ni kula fedha za wana UDOM tu.
  · Watoe tamko kwanini walikwenda IKULU kwa shughuli za kichama na kwa nini walikuwa hawataki college ya social science waende FIELD.
  · Tunawapa masaa 48 ya kujiuzuru.
  ANGALIZO
  Serikali zote za college ziunge mkono kupinduliwa kwa UDOSO-federation sababu wao ndio vikwazo na chanzo cha matatizo yote yanayotokea hapa UDOM.

  NAKALA.
  Mbao zote za matangazo
  · College of informatics.
  · College of social science and humanities
  · College of education
  · College of natural science
  · College of health
  · Chimwaga Hall.
   
 2. n

  nyabhera JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 426
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 60
  laana inawafata wote wote
   
Loading...