airwing
JF-Expert Member
- Dec 8, 2017
- 306
- 398
Habari?
Kuna changamoto niliipata na kampuni moja ya ukopeshaji mtandaoni.. Nilikopa kwao pesa 21/01- Na makubariano yalikuwa niwalipe siku ya tarehe 27. Ilikuwa siku ya tarehe 27 nikapokea simu kutoka kwao wakinikumbusha kulipa deni lao niliwajibu nipo njiani naendesha gari ila sikuhiyo hiyo ningekamilisha malipo.
Mchana wakanipigia tena, Nikawaambia nitalipa kabla ya tarehe 27 kugeuka, nimepata hitilafu ya tairi ninairekebisha ila nikifanikiwa kutoka hapo nitatafuta mpesa iliyokaribu nitafanya malipo.
Dakika chache baadae nikaanza kupokea simu kutoka kwa watu wangu wa karibu wakidai wanapokea message kutoka kwenye kampuni hiyo ikinituhumu mimi kuwa ni tapeli "mjanja mjanja" nisiyetaka kuwalipa pesa zao. Waliwashirikisha deni langu na taarifa zangu binafsi.
Nilijaribu kuwatafuta watoa huduma wao ambao niliwasiliana nao awali, inakuwaje?
Wakadai wakati najisajili huwa wanaingilia mifumo ya namba za simu za mteja, nikauliza pia mbona sijakataa kuwalipa deni lao! Wakanijibu shit.
Je kwa upande wa sheria ninaweza kuishtaki hii kampuni?
Kwa kunidharirisha kuniita tapeli
Kwa kuingilia mifumo yangu ya simu pasipo ridhaa yangu,
Kwa kunichafua kwa watu wangu wa karibu kwa kuniita mimi ni kitu ambacho sicho.
Ushahidi wa vyote ninao.
NB: Deni lao nililipa siku usiku kama ilivyo makubaliano