naomba msaada wa hatua za kisheria .kuhusu ukumbi wa muziki kutupigia kelele jirani na makazi yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

naomba msaada wa hatua za kisheria .kuhusu ukumbi wa muziki kutupigia kelele jirani na makazi yetu

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by morenja, Feb 18, 2012.

 1. morenja

  morenja JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 3,523
  Likes Received: 1,051
  Trophy Points: 280
  naomba ushauri nifanyaje mimi na jirani zangu ,kuna ukumbi wa muziki anaitwa ACTIVE CLUB hupo mbauda. kata ya sombetini Arusha mjini ,wana piga muziki kelele zinatoka nje ya ukumbi jirani atulali vema ,tumelalamika kwa katibu kata ,diwani ccm ,mkurugenzi wa jiji ,kamanda wa polisi ,tume ya sheria na haki za binadamu ,na kumalizia na kwa mbunge Arusha mjini Chadema ,lakini wapi wanapunguza kelele siku 2 mara kelele zinarudia kama kawaida ,mwaka wa 6 sasa ,ni kama mwenye ukumbi ana wapatia rushwa au sijui ni vipi ? Tunaadhirika sana naomba msaada wana jf
   
 2. Bwa'Nchuchu

  Bwa'Nchuchu JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,178
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Hilo ni janga la kitaifa!

  Mabaa na madanguro bubu yamo katikati ya makazi ya watu na watu wengi wanaona hiyo ni kawaida tu.

  Sitaki kukukatisha tamaa lakini.....hmmmm
   
 3. Amavubi

  Amavubi JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Dec 9, 2010
  Messages: 29,452
  Likes Received: 4,736
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni Public Nuisanse (kero) kwa hiyo kama mnaweza kujenga hoja za kisheria vizuri (msije kuwa ninyi ndio tresspassers) au ramani ya mipango miji inasemaje) mnaweza ku-win..............kama mnaona mmeshalalamika kwa wanasiasa vya kutosha nendeni kwenye vyombo vya sheria........hapa Magomeni tulishaletewa shauri kama hilo na Baa hiyo kwa sasa imefungwa...........its a win loose though wanywaji itabidi wasafiri kamwendo.....angalia pia jinsi Waholanzi walivyoandamana na sasa uwanja wao wa ndege unafungwa saa 5 kamili usiku
   
 4. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  mimi nipo karibu na kanisa kila siku ilikua kelele,sio jumapili wala jumatatu.dawa yao ilikuwa moja tu nilikodisha mziki nikaweka show ya hakunaga wakati ibada inaendelea......mchungaji akaja tukayaongea.
   
 5. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kama mmeshaenda kote huko kwa muda wa miaka 6 bila mafanikio kilichobaki ni nguvu ya umma. nyie mjikusanye mshinikize huo ukumbi ufungwe
   
 6. B

  Bandio Senior Member

  #6
  Feb 21, 2012
  Joined: Feb 19, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zingatia ushauri wa Amavubi. Hivi watu wa mipango miji wapo kweli au wako likizo za kudumu? Tatizo la mipango mibovu ya miji ni la kitaifa, wananchi wanajenga sehemu yeyote bila kujali mipango na hawa watu wanaojiita maafisa mipango miji wanatoa vibali vya ujenzi bila kuzingatia mipango, maeneo ya makazi ya watu wanachanganya viwanda, karakana, vituo vya mafuta, n.k. Nafikiri rushwa imeota mizizi kwenye hii idara, na Arusha tatizo ni kubwa.
   
 7. Bondpost

  Bondpost JF-Expert Member

  #7
  Feb 22, 2012
  Joined: Oct 16, 2011
  Messages: 1,979
  Likes Received: 501
  Trophy Points: 280
  Ishu ya public nuisance aisee ipelekeni mahakamani, nanyi itabidi mlete ushahidi kuathirika kwenu kama mnataka kuwadai fidia ila hapo panakuwaga ni ishu maana kuna mambo hadi ya kidaktari hapo.

  Ila nadhani mnaweza kuomba injunction kuzuia wasiendelee na makelele yao. Angalieni ramani ya city plan then ndio muende kuomba temporary injunction mpaka wautengeneze ukumbi wao usitoe kelele au permanent injunction ili kuwazuia kupiga huo muziki.
   
 8. N

  Ngereja JF-Expert Member

  #8
  Feb 22, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 796
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Kwanza nikupe ushauri ufuatao:

  Unatakiwa upeleke malalamiko kwa kiongozi anayehusika katika eneo lako kwa maandishi siyo kwa mdomo. Kiongozi anayehusika akishapoke malalamiko anatakaiwa achukue hatua mara moja kwa mujibu wa sheria. Lakini, pia kuwakomesha hao unaweza kutafuta wakili akawapa kusudio la kushitakiwa iwapo hawataacha.

  Tumia sheria ya "THE LOCAL GOVERNMENT (URBAN AUTHORITIES) ACT, 1982 (CAP. 288)" na Regulations zake yaani "THE LOCAL GOVERNMENT (URBAN AUTHORITIES) (DEVELOPMENTCONTROL) REGULATIONS, 2008"

  Kwenye regulations inasema:

  PART III: SANITARY

  (b) Nuissance

  8.-{ 1) No owner or occupier of a premises, building or land or any
  other person shall in any manner make a nuisance or cause a nuisance to
  be made to a person or public.
  (2) For the purposes of this Part, "nuisance" includes the following:-

  (a)....
  (b)...
  ......
  (w) any noise likely to be dangerous, hazardous or injurious to health or offensive and which is made by a person or group of persons, whether originating from a dancing hall, club, bar,restaurant, hotel, social hall, theatre, plaY!,'Tound, dwelling house,premises or not, made irrespective of musical instrument or
  any other source.
  (3) Any person affected by nuisance shall complain in writing to an
  inspector responsible in the respective area.
  ......

  Kuna mambo mengi na utaratibu na hatua za kuchukua, kwa hiyo itafute uisome yote.
   
Loading...