Naomba msaada wa haraka wana jf | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba msaada wa haraka wana jf

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by ikizu, Dec 5, 2011.

 1. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [h=1]Naomba Kufafanuliwa Ufunuo 13:1-18 na 17:1-18[/h]15 Jun [​IMG]Bwana Yesu asifiwe wapendwa!Mimi ni mfuasi wa Yesu ambaye nimeokoka na niliamua kuachana na mambo yote ya kidunia na kumfuata Yesu. Nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa Bibilia kwa kipindi hiki hasa nikiwa kazini lakini kuna sehemu huwa inanichanganya sana hasa katika kile kitabu cha Ufunuo wa Yohana 13:1-18 na ile sura ya 17:1-18. Naomba mnisaidie kuufahamu ufunuo huu ili niweze kuelewa vizuri na mimi juu ya huyo mnyama, kanisa na wafalme walio hai na waliopita.Nawashukuru sana katika Bwana wetu Yesu kristo
   
 2. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii ndo inamaanisha ndo mwisho wa Dunia?
   
 3. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  hii kitu ni jukwaa la kina gavana na maxshimba..:shock:
   
 4. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #4
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kuna baadhi ya makanisa huwa hayataki kusoma maeneo haya hata kwa bakora wanasema wanazalilishwa.
  naomba kuwasilisha
   
 5. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  John Rwezaura
  Tuesday, June 21, 2011 at 6:58 pm # Kitabu cha ufunuo ni kitabu kinachozungumza habari za mwisho na hasa katika kipindi cha DHIKI KUU cha miaka saba ambayo itakuwa chini ya utawala wa Mpinga Kristo akisaidiana na nabii wa uongo.
  Mnyama ni MpingaKristo ambaye atakuwa anatawala kwa nguvu za Shetani mwenyewe na atakuwa kinyume kabisa na wote wanaomwabudu Mungu aliye hai yaani Mungu wa Israel.
  Vichwa viwili ni pande mbili za dunia yaani Magharibi (nchi za Asia ambapo inasemekan zitaongozwa na mataifa makubwa ya magharibi kwa upande mmoja, na nchi za magharibi zikiongozwa na mataifa makubwa ya ulaya na magharibi. na Pembe kumi ni mataifa makubwa yatakayomuunga mkono kiuchumi, kisiasa na kidini.
  Sehemu kubwa ya kitabu cha ufunuo imezungumzia zaidi juu ya taifa la Israel na mabaki ambao wataokolewa katika kuja kwa Kristo mara ya Pili katika utukufu wake. Mwanamke anayetajwa aliyejifungua mtoto ni taifa la Israel, ambapo mtoto ni wale mabaki watakaokolewa katika dhiki kuu, japokuwa wengi wanasema ni Yesu Kristo. Ukienda katika ukweli halisi, mawazo kuwa mtoto aliyezaliwa na kunyakuliwa mbinguni ni Yesu, hayana ushahidi kabisa; sana sana watu wanaishia katika kuchanganyikiwa tu.
  Wengine wameenda mbali kusema mwanamke ni Mariam aliyemzaa Yesu na kutafsiri jangwa alikopelekwa kuwa ni pale alipoenda Misiri. Hii nayo haina ukweli wowote.
  Jambo la kuelewa ni kwamba mpingakristo hajaanza kazi rasmi, na dhiki kuu haijaanza bado. Inaaminika na wasomi wengi kuwa dhiki kuu haitaruhusiwa kuanza wakati kanisa (waliookoka) likiwa hapa duniani. Wakinyakuliwa, ndipo mpingakristo atakuwa huru kuwatawala na kulazimisha watu wote wamtii ambapo wote watakaokataa watateswa sana na kuuawa kwa kifo cha mateso ya polepole na makali sana yasiyoweza kuvumilika kabisa.

  HERI NA MTAKATIFU NI YEYE ALIYE NA SEHEMU KATIKA UFUFUO WA KWANZA (Atakayenyakuliwa wakati wa ufufuo wa kwanza utakaowahusu watakatifu waliolala katika Kristo.) 1Thesalonike 3:13-18.
  Haggai Kinyau
  Wednesday, June 22, 2011 at 10:12 am # Ndugu John Rwezaura,

  Mungu akubariki sana kwa ufafanuzi wako juu ya hayo yaliyoulizwa. Kwa ujumla kitabu cha Ufunuo kinashindikana kueleweka kwa wakristo wengi kwa sababu ni kitabu kinachoeleza mafunuo ya mwisho wa ulimwengu huu. Inahitajika sana uongozi wa Roho Mtakatifu wakati unasoma Kitabu hiki cha Ufunuo wa Yohana, sina maana kwamba sehemu zingine za biblia utazielewa bila uongozi wa Roho Mtakatifu.

  Pamoja na yale yote aliyoyaeleza ndugu Rwezaura, mimi naomba niongeze kitu kidogo tu, hasa kutoka Ufunuo sura ya 17 kuhusu vichwa saba na pembe kumi za mnyama huyu, na kisha yale mavazi ya zambarau na nyekundu aliyovaa yule mama wa makahaba na machukizo ya dunia. Kwa kifupi pembe ni mamlaka na vichwa saba vya huyu mnyama ni nyenzo mbalimbali au njia mbalimbali ambazo zinamwezesha huyu mnyama kuwaangusha yamkini hata wateule au wale waliookoka. Njia hizi saba ni DINI, SIASA, MAJESHI,TEKNOLOJIA, ELIMU AU UJUZI NA MAARIFA, UCHUMI na MEDIA(magazeti, vipeperushi, radio, television n.k). Kwa sasa sitaweza kufafanua kimoja kimoja lakini unaweza kuona wazi jinsi dini sasa inavyotumika au ilivyotumika hata enzi za Yesu, kuwafungia watu kumjua Mungu wa kweli na hatimaye kuokoka.

  Ufunuo 17 mstari wa nne unazungumzia mavazi aliyovaa huyu mwanamke ambayo ni mavazi ya Zambarau na nyekunde. Mavazi ya zambarau na nyekundu ni mavazi ya kikuhani(kitakatifu). Ukitaka kujua mavazi haya vizuri hebu soma KUTOKA sura ya 28 yote, mavazi haya matakatifu yanampa mtu ukuu na heshima(Kutoka 28:2), ndio sababu huyu kahaba amehakikisha au amefanikiwa kuwanyang’anya watakatifu mavazi yao na kijivika yeye ili apate ukuu na heshima katika dunia hii. Ufunuo 17:5 unatupa jina la mwanamke huyu kuwa ni “BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA MACHUKIZO YA DUNIA”. Sasa swali la kujiuliza na kulitafakari sana ni hili; kama huyu ndiye mama wa makahaba na machukizo yote ya dunia, iweje sasa amevaa mavazi ya kitakatifu? Ameyapataje mavazi haya?

  Mavazi kwa tafsiri nyingine ya kibiblia ni maneno na matendo tunayosema/nena na kutenda juu yetu au juu ya watu wengine. Kwa hiyo pale watu wa Mungu kama makuhani(waliookoka) na makuhani wanaofanya kazi makanisani(wachungaji, maaskofu,n.k) wanaponeneana au kunenewa maneno mabaya ndipo mavazi mema huondoka kwa hao wateule na anavikwa huyu mama wa makahaba na machukizo. Wakati mwingine tunafanya uzinzi na mambo mengine ya machukizo, hayo ni mavazi, tunajivika mavazi mabaya na yale mazuri anajivika huyu kahaba. Kanisa la Tanzania na dunia nzima limeshikwa sana kwa sasa na roho ya uzinzi na ukahaba NA uchawi na uganga(sio utabibu). Kwa maana hiyo sisi ndio tumempa nafasi huyu kahaba ibilisi kutunyanganya mavazi yetu ya utakatifu, na ndio sababu sasa ameshika mkononi mwake kikombe kilichojaa MAMBO YA MACHUKIZO NA UCHAFU WA UZINZI WAKE, amezini na nani? Amezini na watu wa Mungu hasa makuhani(kumbuka uzinzi kibiblia ina maana pana sana, wala sio hii tu tuliyoizoea ya tendo la ndoa nje ya ndoa).

  Ni hayo tu kwa leo kama kuna wengine wanaoweza kutufafanulia zaidi itapendeza kwa utukufu wa Mungu wetu.

  Mbarikiwe na Bwana Yesu.
  samwel
  Wednesday, June 22, 2011 at 11:36 am # Nashukuli sana bwna Johh nimefurahi kwa maelezo yako lakini nimekuwa nikifuatilia reference mabalimbali kuhusiana na hii na pia nimejaribu kufungu a blog mbali mbali . Mfano katika kitabu cha Wken G white amejaribu kufafanua huyu myama kuwa ni kani sa kubwa ambapo pembe hiizo pia ni wafalme lakini kutokana na hizo point zote zikaja kuoana na kanisa kubwa kabsa duniani ambalo kwa kiasi kikubwa ndolinatawala dunia hvyonlitaka kupata ushaidi kwa watu waliookoka nione kuwa hizi reference zinafanana kiasi gani , kiukweli ninahtaji maoni mengi sana kuhusiana na hii mada ili nilewe za idi

  Asante sana na Mungu awabariki wote katika jina La bwana wetu Yesu kristo
  samwel
  Wednesday, June 22, 2011 at 3:04 pm # nashukuru pia bwana Kinyau kwa mafafanuzi yako kiukweli kitabu cha ufunuo ni kinahitaji Roho Mtakatifu ili tuweze kuyaelewa maandiko haya yana maanisha nini lakini kama kuna watu ambao tayari Roho Mtakatifu amewajalia wanaweza kutuelewesha

  Jina la Bwana Wetu Yesu lihimidiwe.
  John Rwezaura
  Friday, June 24, 2011 at 7:40 am # Bwana Samwel nashukuru kwa kunishukuru.
  Nimeyaona maelezo yako na ya Kinyau. Mimi ni mtafiti katika maandiko na tumekutana na theory zote ulizozipata na bahati mbaya unaelekea kuziamini kwamba kwa kuwa waadishi wake wamenukuu vifungu vya Biblia!
  Moja kati ya mambo ya msingi unaposoma andiko lolote katika Biblia, usilitafsiri kwa kuangalia waandishi mbalimbali ya waandishi tu ili kupata ukweli. Katika ulimwengu wa wasomi wa theologia kuna msemo muhimu unaosema “The Bible interprets itself” yaani uhitaji kitabu kingine chochote kuitafsiri Biblia, bali inajitoshereza.
  Wengi wameanzisha dini za kutisha na imani potofu kwa kushindwa kuitumia Biblia kujitafsiri yenyewe.
  Sasa basi, kitabu cha ufunuo si kigumu kama wengi wanvyosema. Mnyama si kanisa kubwa linalotawala dunia. Hiyo ni tafsiri inayotokana na mafundisho ya Hellen G. White muasisi wa dhehebu la wasabato duniani. Tendo la kuliweka kanisa (katoliki) katika nafasi hiyo ni kupoteza maana na asili halisi (context)ya maadiko, na kwa kufanya hivyo, siku zote kitabu cha Ufunuo kitakuwa kigumu tu.
  Hoja ya msingi ni kwamba watakaotumika kumuunga mkono Mnyama (Mpinga Kristo) ni wengi zikiwemo dini kubwa duniani, wanasiasa, na wachumi wa dunia. Lakini, Mnyama atakuwa ni binadamu wa kawaida na atakuwa ni rais wa dunia, vichwa ni mamlaka kuu za ulimwengu, na pembe ni mataifa makubwa na yenye nguvu za kisiasa na kiuchumi. Wote hao wakisaidiana na technology vitamwezesha mpingakristo kuutawala ulimwengu kirahisi. Ndiyo maana wakati Yesu anarudi mara ya pili, atawakamata Mpingakristo na nabii wa uongo na kuwatupa katika ziwa la moto.

  ONYO: Kitabu cha ufunuo hakitafsiriwi kwa mtu kupata mafunuo binafsi, bali tafsiri yake inapatikana katika Biblia kutoka katika kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo. Maisha ya mkristo wa sasa na mambo yote anayofanya, hayana uhusiano kabisa na Mnyama na ukahaba unaozungumzwa katika Ufunuo. Isipokuwa yeye anayeshindwa kuishi kama Yesu anavyotaka ajiandae kukutana na hukumu kama atakufa kabla mpingakristo hajaanza kazi, au akutane na kibano cha mpingakristo wakati wa dhiki kuu.
  Hivyo, nimeandika hayo kwa kuwa nimekuwa na shaka na tafsiri yako na ya Ndugu Kinyau kwa kuwa zote hazina msingi wa maandiko, bali watu wanalazimisha maandiko kuhalalisha mawazo yao na ndoto zao, jambo ambalo ni la hatari kwa mkristo yeyote.

  Asante Samwel kwa hoja hii.
  John
  Paul Holella
  Friday, June 24, 2011 at 2:30 pm # Shalom,
  kitabu cha ufunuo ni kitabu ambacho kimezaa mijadala mingi sana miongoni wa wanafunzi wa biblia…. na sababu si watu wengi wana utaratibu wa kuomba Mungu atie nuru fahamu zao ili waelewe maandiko wamekuwa wakipata shida sana kuelewa haya maandiko…. Pia nisema mambo mengi yaliyonenwa katika kitabu cha ufunuo yapo pia ktk vitabu vingine vya biblia……
  Niende moja kwa moja kwenye swali Tafsiri ya mnyama ufunuo sura ya 13 na 17…… habari ya huyu mnyama inafanana na ufunuo 12:3

  ufunuo sura ya 17 kuanziia mstari ule wa 7-18 malaika anatoa tafsiri…. maana ya vile vichwa saba na zile pembe kumi…..
  pia hii habari inapatikana ktk kitabu cha daniel 2 kumbuka ile ndoto ya mfalme nebkadneza …….
  malaika anamwambia Yohana …..Na yule malaika akaniambia, Kwani kustaajabu? Nitakuambia siri ya mwanamke huyu, na ya mnyama huyu amchukuaye, mwenye vile vichwa saba na zile pembe kumi. ……. Malaika anatoa siri ya huyo mnyama na mwanamke aliye juu ya huyo mnyama….. mstari wa 9 Hapo ndipo penye akili zenye hekima. Vile vichwa saba ni milima saba anayokalia mwanamke huyo. 10.Navyo ni wafalme saba. Watano wamekwisha kuanguka, na mmoja yupo, na mwingine hajaja bado. Naye atakapokuja imempasa kukaa muda mchache. …ndugu samwel vile vichwa saba ni wafalme saba….. ni falme 7 ambazo ziliwahi kutawala dunia na zingine zilikuwa bado hazija tawala bado……. rudi kwenye ndoto ya nebkadneza ile ya sanamu….. kile kichwa (dhahabu) kilikuwa ni ufalme wa babel…. ikafuata kifua(fedha)..umedi na uajemi..ikafuata tumbo (shaba)…uyunani na miguu ya chuma (Rumi) na vidole kumi vya chuma na udongo ….. linganisha hivi vidole na zile pembe kumi…..

  Sasa huyu mnyama ni mfumo (ambao mpinga kristo yumo ndani yake)….. ambao Mpinga Kristo na shetani wamekuwa wakiutumia na watautumia kupitisha mambo yao duniani…….
  vichwa saba bi dola saba zilizotawala na zingine bado hazijatawala….. wakati daniel anatafsi ndoto ya Nebkadneza tayari kulikuwa na dola kubwa mbili zimeisha aanguka…. nazo ni Egypt na Assyria (Ashuru) kwa hiyo ya Babeli ilikuwa ya tatu……
  ngoja niziandike vizuri
  1.Misri
  2.Ashuru
  3.Babel
  4.wamedi na waajami
  5.Wayunani
  6. Warumi….hapa ndipo kichwa cha 6 na wakati Yohana anapata huu unabii…. huyu ndo mmoja aliyekuwepo
  7.alikuwa hajaja ila imempasa kukaa muda mchache… turudi kwa yule malaika kuangalia aliendeleaje…..
  mstari wa 11..Na yule mnyama aliyekuwako naye hayuko, yeye ndiye wa nane, naye ni mmoja wa wale saba, naye aenenda kwenye uharibifu. 12.Na zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi, ambao hawajapokea ufalme bado, lakini wapokea mamlaka kama wafalme muda wa saa moja pamoja na yule mnyama.
  Mfalme wa 7/ kichwa cha 7 ni hawa wafalme kumi ambao huu utakuwa ni muungano… ila unanguvu za chuma kumbuka Daniel alichosema na hawa ndo watampa mpinga kristo mfalme wa 8 mamlaka yao….. kama ufunuo sura ya 17 inavyomalizia …..
  nafikiri kwa leo niishie hapa…
  kama unamaswali zaidi uulize usiogope pitia maandiko mengine yenye habari kama mathayo 24, luka 21, Daniel…

  Sijatafsiri habari ya Mwanamke aliye juu ya mnyama…hii siku nyingine… Mungu akubariki kwa kutaka kujua.
  lwitiko
  Saturday, June 25, 2011 at 2:41 pm # Ukitaka kusoma vizuri kitabu cha ufunuo na kupata mwanga zaidi lazima usome na kitabu cha Daniel hasa, ni vitabu viwili ambavyo unapaswa kuvielewa vizuri, hasa Daniel, ni kitabu ambacho utasoma sura za mwanzo ila utakapoanza kufikia sura ya 8 kwende mbele unaweza usielewe lakini yupo Roho Mtakatifu anayetufunulia akili tupate kuyaelewa na maandiko.

  Lakini kwa msaada kidogo huyu mnyama wa kwenye ufunuo anawakilisha kufufuka kwa ufalme uliokuwepo harafu ukatokomea lakini huo ufalme upo tayari kurudi tena yaani ni revival of the Roman empire, which will be the Union of Nations where the beast will be governed. Na EU au umoja wa ulaya ni alama mojawapo ya kurudi kwa huyu mnyama, Anti christ anatokea ulaya na wala sio katika uislamu kama wengi wanavyofikiri, wengine wanasema ni marekani lakini sio marekani, Ukisoma ufunuo utaona mnyama anatokea baharini baharini ina maana yake, Baharini ni mkusanyiko wa maji mengi amabo unawakilisha ya kwamba huyo mnyama lazima atokea katika Muunganiko wa mataifa

  kuna mabadiliko makubwa sana yanakuja ndani ya umoja wa mataifa( UN) wengi wataona na kusikia habari ya mabadiliko ya mfumo wa Umoja wa mataifa au ndani ya UN lakini ni mabadiliko ambayo siyo mazuri kwasababu yanatengeneza njia ya moja kwa moja ya kuwa na one world Government, na EU au umoja wa ulaya unatuta kuwa na nafasi muhimu au kitio cha kudumu ndani ya UN, na vatican wako karibu sana kufanikisha hili jambo, kuna uwezakano wa kupata a powerful structure itayopelekea EU kuwa a diminutive super power orgainization ndani ya umoja wa mataifa ili kuondoa nguvu au kusapress nguvu ya marekani ndani ya umoja wa mataifa

  France, Germany, Italy, Spain, Portugal, Vatican, Greece, Luxembourg, Sweden, Switzerland ni baadhi ya mataifa ya kuyaangalia sana, huyu mnyama atakayekuja haya mataifa yatakuwa yanatengeneza mamlaka ya The Beast,
  vichwa saba ni wafalme saba, na kimoja kati ya vichwa saba kikaonekana kuwa na Jeraha la Mauti nalo lile jeraha likapata kupona, kile kichwa chenye jeraha la Mauti ndio mfalme yule ambaye Daniel amemzungumziua sana ile sura ya 11 mpaka kumi na mbile ndio mkuu au kiongozi wa hiyo Global empire or Roman empire au Anti Christ, kumbuka anti christ atakuwa ni mtu, He is a person ambaye atakuwa ana uweza wa ajabu na kipawa cha ajabu sana na cha hali ya juu sana atakuwa ni military dictactor mwenye nguvu kubwa sana za kijeshi, kiiuchumi na kidiplomasia , ulimwengu utamstaajabia lakini hautajua ya kwamba nyuma yake na ndani yake yupo shetani na ana operate katika nguvu na mamlaka ya Shetani pembeni yake kukiwa na yule nabii wa uongo afanaye Ishara kubwa sana ili watu wapate kumwabudu na kumsjudia yule mnyama na sura(image) yake. hata sanamu ya yule mnyama ipate kunena. Uenda itakuwa ni kwa teknologia au kwa njia nyingine ya kimaajabu image ya yule mnyama itaweza kuongea hata yeye mwenyewe asipokuwepo hapo sehemu yoyote ambayo image yake ipo itaweza kuongea, atafanya agano thabiti na watu wengi sana kwa muda wa miaka 7 hasa taifa la Israeli akijaribu kuleta amani kati ya Taifa la Isareli na nchi za kiarabu na hasa palestine lakini katikakati ya miaka saba au baada ya miaka31/2 ( miatatu na nusu) atarudi Israeli na kuangalia hilo agano tena lakini atakuta wameacha kulifuata na yeye atalivunja rasmi na ataisimamisha sadaka ya kuteketezwa ya daima ndani ya patakatifu pa hekalu na badala yake atasimamisha picha au taswira yake patakatifu akitaka yeye apate kuabudiwa na sadaka kutolewa kwake kama Mungu, hilo ndio chukizo la uharibifu,
  samwel
  Monday, June 27, 2011 at 2:18 pm # Asante bwana Lwitiko kwa mafafanuzi yako kiukweli katika makanisa yetu mengi ya kiroho somo hili huwa hatufundishwi sanasana ndo maana hata bwana Jonh kasema ni vilahisi sana kupelekwa kwenye msimamo wa watu wengi ambao wmeundda hoja zao binafsi, Pia kinasema katika ile mstari wa 9 kuwa huyo mwanamke yuko juu ya vlima saba na ukiangalia jiji la Rome liko juu ya vilima saba. hivyo basi kwa mimi naona kama hizi factor zinangukia kabisa na kanisa kuwabwa kama nlivyotangulia kusemma awali
  samwel golanga
  Wednesday, July 6, 2011 at 10:35 am # Bwana asifiwe wapendwa si vibaya tukiendelea kueleweshana kuhusu n=nad nilioianazia hapo juu juu ya kutabu hichi cha ufunuo . Tukiangalia ule mstari wa 18 tunaona kuwa zile namba ni tarakimu za kibina damu ambazo ni 666 na ambazo nikichunguza katika vyanzo vangu ni ile taito ya papa ambayo ni ”VIARIUS FILLII DEI” (latin)
  ambapo ukipata jumla yake kama ifuatavyo
  V….5 F…0 D…500
  I…1 I…1 E…0
  C…100 L…50 I….1
  A…0 I…1 _______
  R…0 I…1 =501
  I…1 ______
  U(v)…5 =53
  S…0
  ______ TOTAL 666
  =112

  Naomba pia kupata ufafanuzi huu kuhusu hii namba kwa sababu kwenye bibilia imeeandikwa kuwa ni namba ya kibinadamu , lakini pia kuna vitu vingi ambavyovina namba hiyo mfano atm card ber code nk.
  Mungu awabariki sana wapesandwa katika jina ka bwana wetu Yesu kristo
   
 6. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wana jf nimeamua kuwawekea hayo maelezo ya watutu wengine ili kama kuna anayejue zaidi ya hao atujuze maana mpaka sasa sijaelewa ndo maana nimeomba msaada
   
 7. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  poleni sana kama nimewaboa wana jf.
   
 8. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asanteni wana jf kwa michango yenu
   
 9. ikizu

  ikizu JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2011
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 431
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  jamani mpo mbona kimya?
   
Loading...