Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,103
- 8,037
Siku ambayo Judge atatoa hukumu imekaribia. Kuna watu wamejiandaa kushangilia, lakini wengine mioyo yao inadunda kwa hofu, kwakuwa wanajua ni wakosaji. Je, Judge huyu atatoa hukumu ya haki? Je, anaweza kuhongwa ili abadilishe hukumu? Wakati tunaisubiri siku ya hukumu, hebu tutafakari "CV" ya Judge huyu:
• Jina: Yesu Kristo
• Cheo: Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana (Ufu. 19:16)
• Asili: Alpha na Omega - wa kwanza na wa mwisho. (Ufunuo 1:17-18)
• Tabia: Mtakatifu, mwenye haki, kweli, asiye na dhambi (Ebr. 4:15)
• Uzoefu: Alikufa kwa ajili ya wenye dhambi, akafufuka, na yuko hai milele (1 Kor. 15:3-4; Ufu. 1:18)
• Uwezo: Anajua yote yaliyo moyoni mwa mwanadamu (Yoh. 2:24-25)
• Mamlaka: Amepewa mamlaka ya kuuhukumu ulimwengu kwa haki (Matendo 17:31)
Siku ya hukumu haiko mbali. Na Yesu ndiye atakayetoa hukumu. Wanaokataa kuacha dhambi na kumwamini, hukumu yao ni kutupwa katika ziwa liwakalo moto. Lakini watakatifu wataambiwa: "...Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu. Kwa maana nalikuwa na njaa, mkanipa chakula; nalikuwa na kiu, mkanipa maji; nalikuwa mgeni, mkanikaribisha." (Mathayo 25:34-35)