Naomba msaada wa Dawa ya kuua (bedbugs) kunguni

Jodoki Kalimilo

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Messages
10,073
Points
2,000
Jodoki Kalimilo

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2012
10,073 2,000
Mkuu mi sijawah kuwa hata na nzi wala mbu geto kwangu wala mende, na nilikua bishoo ila najua kuna mpuuzi mmoja tu alikuja nao tuu maana siwez kujua ntawazalishaje mwenyewe na niliishi home fresh tuu tangu nazaliwa ndo nije kuwa nao ukubwani, theory ya uchafu ni uongo, maana nakumbuka utotoni sikuwa msafi, na boarding nimesoma sijawaona, na chuo hosteli sijawaona ndo nimekuja kuwaona baada ya kupanga uswazi na kukaribisha washkaji tu wanachill wanacheki muvi nini wanaenjoy mara haaaooo,

Sent from my TECNO W1 using JamiiForums mobile app
Soma vizuri mkuu nilichoandika, unaweza ukawa msafi ila kuna wachafu wengine wametumika kuzalisha kunguni na ndio maana wakawa transfered kutoka kwa washikaji wako kuja kwako maana kama wangekuwa wanajielewa wewe usingewapata...ni sawa na tunapoambiwa ukiugua kipindupindu ni kwamba umekula mavi na sio wote wanaougua kipindupindu wamekula mavi directly bali alisalimiana na mgonjwa ama katika kumhudumia mgonjwa akajikuta ameukwaa ugonjwa kwa bahati mbaya. Ndivyo na kunguni hivyo hivyo kuna watu wamejenga mazingira ya kunguni kuwa sehemu ya maisha yao na mwisho wa siku wanafanya kuwahamisha...kunguni akiwepo ndani kwanza shuka tu zinachoka na kama mtu amekaa nao mpaka anakuletea wewe unadhani hilo gheto lake likoje mkuu kama sio chafu (uchafu sio lazima kuoga kila siku hata kurundika nguo, kuweka viatu ovyo nakadhalika
 
Ndadyeletse

Ndadyeletse

Member
Joined
Nov 26, 2015
Messages
86
Points
95
Ndadyeletse

Ndadyeletse

Member
Joined Nov 26, 2015
86 95
Naombeni mnisaidie dawa itakayo maliza kunguni maana wamevamia chumba changu
na pia nimeckia ile dawa ya RUNGU spray yaweza ua kunguni je hii ni kweli?

Msaada please namna ya kuwatoa hawa wadudu!
View attachment 801832


Baadi ya michango ya wadau;


KUFIKIA katikati ya karne ya 20, ilionekana kwamba wanadamu wamefaulu kuwadhibiti kunguni. Watu fulani walifahamu kunguni kupitia tu wimbo wa zamani wa Kiingereza ulioimbwa na watoto wa shule za nasari (au chekechea) uliosema: “Usiwaache kunguni wakuume.” Hata hivyo, katika miaka ya 1970, nchi nyingi ziliamua kupiga marufuku matumizi ya dawa ya DDT—iliyokuwa dawa kuu ya kuua kunguni—kwa kuwa ilikuwa yenye sumu na iliharibu mazingira.

Hata hivyo, kemikali nyingine zilipotumiwa ilionekana kwamba kunguni walikuwa sugu na hazikuwaua. Pia watu walianza kusafiri mara nyingi zaidi na bila kujua walihama pamoja nao. Matokeo yakawaje? Ripoti moja ya mwaka wa 2012 kuhusu kuwadhibiti wadudu hao inasema: “Katika miaka 12 ambayo imepita kunguni wameanza kuonekana tena nchini Marekani, Kanada, Mashariki ya Kati, nchi kadhaa za Ulaya, Australia, na katika sehemu fulani za Afrika.”

Huko Moscow, Urusi, katika mwaka mmoja hivi karibuni, ripoti za kutokea kwa kunguni ziliongezeka mara kumi kuliko ilivyokuwa hapo awali. Wakati huohuo, upande ule mwingine wa ulimwengu, huko Australia, kumekuwa na ongezeko la asilimia 5,000 la kunguni tangu mwaka wa 1999!

Watu fulani hubeba kunguni bila kujua wanapoenda dukani, kwenye kumbi za sinema, au hotelini. “Upende usipende utabeba kunguni,” anasema meneja fulani wa hoteli nchini Marekani. “Maadamu hoteli inapata wateja lazima kunguni wataendelea kuwapo.” Kwa nini ni vigumu kiasi hicho kuwamaliza kunguni? Unaweza kujilindaje? Kunguni wanapovamia nyumba yako, unaweza kuchukua hatua gani zinazofaa ili kuwaondoa na kuwazuia wasirudi tena?

Wadudu Wasiokufa kwa Urahisi

Kwa kuwa wadudu hao ni wadogo kama mbegu ya tofaa na wana mwili bapa, kunguni wanaweza kujificha mahali popote pale. Wanaweza kujificha katika godoro lako, fanicha zako, sehemu ya ukutani ya kuunganishia vitu vya umeme, au hata kwenye simu yako. Kwa kawaida kunguni hupenda kujificha mita tatu hadi sita kutoka kwenye vitanda na maeneo ya kuketi. Kwa nini? Ili wawe karibu na chakula chao, yaani, wewe!*

Mara nyingi, kunguni huwauma watu wanapolala. Hata hivyo, watu wengi hawahisi wanapoumwa kwa sababu mdudu huyo humdunga mtu kitu kinachogandisha kinachomwezesha kuendelea kula kwa dakika kumi hivi bila kukatizwa. Na ingawa kunguni wanaweza kula kila juma, imesemekana kwamba wanaweza kuendelea kuishi bila kula kwa miezi mingi.

Tofauti na mbu na wadudu wengine, inaonekana kwamba kunguni hawaenezi magonjwa ya kuambukiza. Hata hivyo, wanapomuuma mtu wanatokeza mwasho na baadaye sehemu hiyo inavimba, na watu wengi huathiriwa kihisia. Watu walioumwa na kunguni wanaweza kupoteza usingizi, kuaibika, na hata kufikiri kwamba kunguni amewauma muda mrefu baada ya wadudu hao kutoweka. Jarida moja nchini Sierra Leone linasema kuwa kunguni “ni wasumbufu sana na wanawakosesha watu usingizi” na linaonya kuhusu “aibu inayohusianishwa na kunguni.”

Kuwadhibiti Kunguni

Kunguni wanaweza kumsumbua mtu yeyote. Ni rahisi kuwadhibiti ukitambua mapema kwamba wapo. Kwa hiyo, jifunze kutambua ishara za kwamba wapo nyumbani na unaposafiri. Chunguza fanicha zako na vitu vingine vya mbao pamoja na mizigo, uone ikiwa kuna mayai madogo yanayofanana na mbegu ndogo nyeusi au alama za damu. Tumia tochi unapowatafuta kunguni ili uweze kuwaona.

Usiruhusu kunguni wawe na sehemu nyingi za kujificha. Ziba nyufa zote ukutani na kwenye viunzi vya milango. Ingawa kunguni hawaletwi na uchafu, itakuwa rahisi zaidi kuwatambua na kuwadhibiti ikiwa unasafisha nyumba kwa ukawaida na kupunguza vitu vilivyorundamana. Ukiwa hotelini, unaweza kupunguza uwezekano wa kubeba kunguni kwa kuepuka kuweka masanduku yako sakafuni na kitandani.

Kunguni Wanapovamia Nyumba Yako

Ukipata kunguni nyumbani au hotelini, huenda ukawa na wasiwasi au hata ukaaibika. Dave na mke wake waliumwa na kunguni walipokuwa likizoni. Dave anasema: “Tuliaibika sana. Tulijiuliza tutawaambia nini watu wa familia na marafiki tutakapofika nyumbani? Je, wakati wowote wanapojikuna au kupatwa na mwasho wa ngozi wangejiambia ni kwa sababu walitutembelea?” Hata ingawa ni kawaida kuwa na maoni kama hayo, usiache aibu ikuzuie kutafuta msaada. Wizara ya Afya ya Mwili na Akili ya New York City inatoa uhakikisho huu: “Ni vigumu, lakini inawezekana kuwaangamiza kunguni.”

Chunguza uone kama kuna kunguni kisha uchukue hatua za kuwazuia wasijifiche nyumbani kwako
Hata hivyo, usifikiri kwamba ni rahisi kuwamaliza kunguni. Kunguni wakivamia nyumba yako, unaweza kupata msaada kutoka kwa mtaalamu wa kuwadhibiti wadudu wasumbufu. Ingawa kemikali zilizotajwa awali hazitumiwi tena, wataalamu hao hutumia mbinu kadhaa zinazofaa ili kuwaangamiza kunguni. Dini M. Miller, mtaalamu wa wadudu anasema hivi pia: “Kuwadhibiti kunguni kunahitaji ushirikiano mkubwa sana kati ya wakaaji wa nyumba, wamiliki wa nyumba yenyewe, na kampuni ya kuwadhibiti wadudu wasumbufu.” Kwa kufuata mwelekezo wa mtaalamu na kuchukua tahadhari zinazohitajika, unaweza kutimiza sehemu yako na ‘kutowaacha kunguni wakuume’!
Jumla DAWA ya LARVA
 
nosspass

nosspass

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2013
Messages
4,240
Points
2,000
nosspass

nosspass

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2013
4,240 2,000
hao jamaa kunguni - land rover 109, wako fasta ajabu.....yaani utoe kila kitu nje ndio upulize dawa....wanaenea kwa kasi ya ajabu..
 
Kibajajitz

Kibajajitz

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Messages
4,068
Points
2,000
Kibajajitz

Kibajajitz

JF-Expert Member
Joined Apr 20, 2013
4,068 2,000
Hahaha
Sasa wewe uliyekutana nao gesti ilibidi ukirudi nyumbani kwako uache nguo zako barazani zichomwe, uingie mlango wa mbele uchi wa mnyama. Assuming ulikuwa hufanyi dhambi huko gesti maana wanaweza kuwa walipata upenyo wamejificha kunakofichwa madawa.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
H

hakisoni

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
477
Points
225
H

hakisoni

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
477 225
jamani kunguni wamekuwa tishio nyumbani kwa miaka 10 sasa, nimetumia dawa nyingi za poda (sevin dudu dust, aerial powder), diazoni, ngao, kuchemsha maji, povu la sabuni, rungu spray na chaki ya kuchora lakini wapi! Ivyo wanajamvi kwa yeyote anayeweza kunishauri (dawa) nini cha kufanya naomba sana msaada wenu binadamu wenzangu. Asanteni!
Mkuu kanunue ddt ndio kiboko yao hutakaa uwaone tena maishani mwako. Cha kufanya ni hiyo dawa na vipimo vyake unaua hadi mayai kwishney hutawasikia tena hapo unapokaa. Kama wamezidi sana hiyo dawa paka kwenye hizo conner za vitanda na kabati kavu usidilute na maji paka hivyo hivyo habari yao utaimaliza.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Messages
18,939
Points
2,000
imhotep

imhotep

JF-Expert Member
Joined Oct 13, 2012
18,939 2,000
Mimi iko siku nilitoa kitanda nikakipulizia dawa nikasafisha chumba pamoja na cha watoto wangu kazi hiyo ilichukua weekend yangu nzima

Vitanda nikahamishia Stoo godoro nikaliweka chini huku nikijisemea moyoni kwangu kuwa kiama chao kimewafikia

Nikalala kwenye godoro kama wiki hivi kabla ya usiku mmoja wa Mvua Tandu akaniingilia kwenye shuka na kuning'ata sintosahau maumivu yale
 
Esker

Esker

Member
Joined
Aug 13, 2019
Messages
26
Points
45
Esker

Esker

Member
Joined Aug 13, 2019
26 45
Mimi iko siku nilitoa kitanda nikakipulizia dawa nikasafisha chumba pamoja na cha watoto wangu kazi hiyo ilichukua weekend yangu nzima

Vitanda nikahamishia Stoo godoro nikaliweka chini huku nikijisemea moyoni kwangu kuwa kiama chao kimewafikia

Nikalala kwenye godoro kama wiki hivi kabla ya usiku mmoja wa Mvua Tandu akainiigilia kwenye shuka na kuning'ata sintosahau maumivu yale
Pole mkuuu hao viumbe ni hatari
 
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Messages
37,608
Points
2,000
Sky Eclat

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2012
37,608 2,000
Mimi iko siku nilitoa kitanda nikakipulizia dawa nikasafisha chumba pamoja na cha watoto wangu kazi hiyo ilichukua weekend yangu nzima

Vitanda nikahamishia Stoo godoro nikaliweka chini huku nikijisemea moyoni kwangu kuwa kiama chao kimewafikia

Nikalala kwenye godoro kama wiki hivi kabla ya usiku mmoja wa Mvua Tandu akainiigilia kwenye shuka na kuning'ata sintosahau maumivu yale
Tandu aling’ata sehemu gani?
 
nkumbison

nkumbison

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2013
Messages
1,065
Points
2,000
nkumbison

nkumbison

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2013
1,065 2,000
Hao nilipambana nao sana Studio! Mpaka leo nimetoa masofa na proof ni mwendo wa mabenchi na wateja wakitoka nayatoa kwanza hadi nifanye upembuzi yakinifu maan hawa wadudu pumbav sana hawategemeani kuzaliana akishiba damu tuu anataga.

Dawa isiyo rasmi ila inawapunguza sana kama sikuwamaliza.
Chukua mafuta ya taa kama ni nusu lita ongeza na maji kidogo tuu hata kikombe cha chai kidogo mix na sabuni ya unga ya kiasi haitazidi wala kupungua then paka kwenye fenicha kona zote kipindi hiko ndani umetoa nguo zote na kuzifua upya huku ukiziacha kwa kamba hata siku mbili tatu.
 
kadagala1

kadagala1

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2016
Messages
5,901
Points
2,000
kadagala1

kadagala1

JF-Expert Member
Joined Nov 23, 2016
5,901 2,000
Mimi iko siku nilitoa kitanda nikakipulizia dawa nikasafisha chumba pamoja na cha watoto wangu kazi hiyo ilichukua weekend yangu nzima

Vitanda nikahamishia Stoo godoro nikaliweka chini huku nikijisemea moyoni kwangu kuwa kiama chao kimewafikia

Nikalala kwenye godoro kama wiki hivi kabla ya usiku mmoja wa Mvua Tandu akainiigilia kwenye shuka na kuning'ata sintosahau maumivu yale
Nasikia tandu wanafata mende chumbani
 

Forum statistics

Threads 1,334,284
Members 511,934
Posts 32,471,852
Top