Waungwana nahitaji kuwa programmer si kwa minajili ya kuajiliwa hapana kwan mm ni mwajiliwa pale MMP ila napenda tu huo ujuz.
Nawezaje kuwa hvyo pasipo kupitia chuo? Kama kuna mtu anaweza kunipa elimu hiyo tuwasiliane tafadhali.
Maswali aliyouliza 'Aqua' ni muhimu sana.
Ni kweli ku-code kunahitaji uwezo mkubwa wa kufikiri ila siyo lazima uanze na kutengeneza complex software. Unaweza ukaanza kidogo kidogo kwa kutengeneza vi-code rahisi kama kuprint maneno haya kwenye screen 'hii ni code yangu ya kwanza' halafu ukaendelea kucode alarm clock ambayo itacheza wimbo wako unaoupenda ili ikuamshe kila asubuhi. Chamuhimu hapa ni utundu na kujaribu kutatua matatizo madogo madogo unayokumbana nayo kila siku kwa kutumia computer.
Ok.Kuna swali moja hujalijibu,mara ya mwisho ulipokuwa shule ulisomea mambo gani?
Swali la 'Aqua' kuhusu mara ya mwisho ulisomea nini, maana yake ni kutaka kujua machakato wako wa kimawazo. Hii ni muhimu kwasababu katika programming unatumia sana hatua (steps) mbali mbali ili kufikia lengo fulani tofauti na comon sense tunayotumia wanadamu. Kwa mfano kama kuna giza chumbani kwako common sense itakuambia washa taa, lakini computer haiwezi kujua bila ya kuwa programmed kutambua kuwa kama kuna giza basi labda taa inabidi iwashwe.
Tatizo kubwa lililopo wakati unajifunza ku programa ni kuwa sisi wanadamu tuna-superior brain ambayo mara nyingi tuna 'take things for granted' (yaani ubongo unatufanyia mambo bila sisi kujua), hiki ni kitu unachotakiwa kuwa macho. Mfano mzuri ni pale unavyonyanyua glasi ya maji na kunywa, hapa kuna hatua nyingi sana ambazo ubongo wako unazifanya bila ya wewe kufikiria/kujua. Kuna jinsi ambanyo inabidi ubongo wako ufikirie "angle" gani itumike ili unyanyue mkono wako kuifikia glasi, halafu utumie nguvu kiasi gani kuinyanyua na misuli ipi itumike na kwa muda gani ili iifikie mdomo.Vipimo hivi vikikosewa utaweza kujiumiza au kujimwagia maji, kama utatumia nguvu kubwa kunyanyua glasi.
Sasa unapo-program lazima ufikirie kama computer (siyo kama wewe), kama alivyosema 'Aqua' (thinking out side the box), kwasababu computer haiwezi kukufanyia/kukufikiria kama vile ulivyozoea ubongo wako kukufanyia. Ndiyo maana kwenye masomo ya sayansi au hisabati tunafundishwa kufanya vitu kwa hatua. Utakuta hata 'A-levels' programming inafundishwa kwenye Advanced math, japokuwa vijana wengi huwa hawajui kuwa wanajifuna programming, kwa mfano nakumbuma wakati nipo 'A' level tulijifunza iterative methods, kama Newton Raphson, ambapo tulijifunza kukadiria roots.
Sijui unapendela nini lakini programming ina flavors nyingi (language) kutokana na unachotaka ku-program. Unaweza ku program kitu chochote kwa language yoyote ile lakini kuna languages ambazo ni nzuri (effective) kwa mambo fulani. Kwamfano PHP ni nzuri kwa mambo ya web development lakini kama unataka kutengeneza heavy duty website kama facebook inabidi baadhi ya mambo utumie language nyingine kama C++.
kwahiyo ndugu yangu fikiria unataka kufanya nini ili utuambie tukuelekeze njia nzuri ya kufuata. Ni havo tuu.