Msaada wa jinsi ya kusamehe na kuachilia

Mnabuduhe

JF-Expert Member
May 8, 2015
348
1,000
Habari wana JF!

Mimi ni Muhanga wa hali hii nimevumilia sana lakini nimeshindwa. Juzi kuna jamaa yangu amekuja hapa kunihadithia kisa kilichomkuta maishani mwake ameshindwa kabisa kusamehe na kuachilia inagawaje anadai hana shida na watu waliomuumiza na kumpiga majungu.

Baada ya kunieleza kisa chenyewe akawa kama amenitonesha kidonda. Nakumbuka ilikuwa 2017 kazini (Naomba nisitaje kazi ninayofanya,ukiconnect dots naomba utulie tu). Ndipo nilipoona hamna maana ya kuwa na marafiki na kuwathamini sana na ndio kilichonifanya kutambua kuwa bado nina maumivu moyoni kama ya jamaa yangu huyu aliyenielezea kisa chake ambacho kwa leo nakiweka kipolo nieleze kisa changu kwanza.

Ilianza hivi,nilimpokea jamaa kazini akawa rafiki yangu wa karibu,alisema alishawahi kuwa mtumishi wa kada yetu huko sekta binafsi lakini akawa hakuna anachojua,nikawa msaada mkubwa kwake na tukaendelea na maisha vizuri tu,tukaendelea kupokea watumishi wengine tukawa tunaongezeka pale kazini pakachangamka sana.

Bahati mbaya Boss wetu akapata matatizo akawa kashushwa cheo,Jamaa yangu akapata kile cheo,alipopewa barua breki ya kwanza akaja kwangu akanionesha barua akaniomba nimsaidie niwe msaidizi wake namba mbili huku akirejea jinsi ambavyo tuliishi vema na msaada niliompa wakati wote. Nikakubali nikamwambia tupige kazi.

Akaja jamaa mwingine mtu mzima kama yeye! akaripoti pale kazini,kwa jinsi alivyoonekana alionekana ni Mtaratibu na mshika dini sana,basi jamaa akamchagua kuwa msaidizi chini yangu,hivyo tukawa watu watatu ndio tuna sauti pale kazini.

Sasa watumishi wenzetu wakawa wanamsema sana Boss! kuwa hajali watu anajiamuria mambo bila kushirikisha wengine,na wakati wanamsema hivyo wanasubiri mimi nikiwa nao ndio wanayasema hayo,na wengine wana sisitiza we si ndio msaidizi wake mwambie jamaa yako mambo huwa hayaendi ivo.

Basi nikajiridhisha kuwa kuna hoja ni za msingi na hoja zingine ni majungu tu! Nikamfuata ofisini nikamwambia tuongee kidogo,nikampasha nini kinaendelea pale kazini na nikamshauri kuwa mengine ni majungu lakini mengine ajaribu kuyatolea ufafanuzi wa kina kwa watumishi wenzetu ili kuondoa tashwishi na ili mambo yaendelee vizuri.

Basi jamaa akawa kama amenielewa akaniagiza niandike memo ya kuwataarifu kuwa siku flani kutakuwa na kikao,nikafanya hivyo kama alivyoagiza.

Hali ikanibadilika ghafla jamaa akaanza kunipiga vijembe, mara watumishi wengine wanalalamika kuwa ananipendelea sana mimi, mala mimi ni mzembe, mambo yakawa mengi sana.

Sikujua nifanye nini? Baada ya muda watumishi wengine wakaanza kunipa ubuyu,(Wanawake Mbarikiwe sana) Huyu Mdada tunafanya nae kazi akanieleza siku ambazo haujaja kazini jamaa yako anakusema vibaya sana,anadai humsaidii mara umebadirika sana hukuwa hivyo mwanzo,hasa baada ya kufunga ndoa umekuwa wa tofauti sana,Labda Ndoa inakusumbua?

Sikujali nikapuuza! Sasa pale ofisini jamaa sio mtaalam sana wa mambo ya mifumo ya Serikali, mimi ndie nilikuwa kilaka pale,akawa ananiagiza kufanya mambo bila malipo,nikaendelea kufanya bila shida.

Nikaja kupata taarifa kuwa yule jamaa aliyeteuliwa kuwa msaidizi wako na Boss ndie anayekufitini sana! Nikajiuliza sana,inamaana Boss hanifahamu kabisa mpaka anaamini kila anachoambiwa na Jamaa naomba hapa nimpe jina la Shemasi huyu Mfitini wangu.

Basi Shemasi akawa ndie mwandani wa Boss, sikujali sana, sasa wakaanza kuwa wana ni SIDELINE,yaani Kama wananiepuka vile,Ikawa Boss akiondoka kikazi ananiachia majukumu lakini kumbe shemasi kaagizwa anifautilie kwa ukaribu.

Hilo sikulipenda ila nikajikaza,lakini pia nikashidwa,ikabidi nimshirikishe Mke wangu!Mke wangu akaniambia fitina ni kawaida komaa nao! Usiache hiyo nafasi endelea kumsaidia jamaa ako.

Mimi Ni Mkristo nikaanza kusali na kuomba maarifa nifanyeje sasa! Ikafika kipindi hasira ikapanda sana nikasema sasa! Ngoja nikamripue huyu asinifanye mimi zuzu kwa kuwa najua anachonifanyia ila nimeamua kunyamaza tu! Nilipanga nikaseme ukweli wote na yanayoendelea kuwa najua asinifanye mie Mjinga,lakini Kabla sijafanya hiyvo nikaingia kwenye Maombi - Baada ya Kuomba nikasikia msukumo wa ajabu - Kuwa Nisiseme chochote nitulie tu! Basi nikaisikiliza ule msukumo nikatulia.

Mambo yakaendelea vile vile hakuna mabadiliko! Jamaa chuki ikazidi sana juu yangu,nikasikia anadai kuna mtumishi mwenzetu huko Chuo Kikuu akija tu! basi atanitoa na atampatia huyo Jamaa Nafasi yangu.

Kwa kweli nilipigwa majungu sana ambayo mengine siwezi eleza hapa ili kuendelea kuficha jina na Taasisi ninayofanyia Kazi.

Nikaona isiwe tabu sana! Nikamfuata Ofisini kwake kwa Upole sana! Nikamwambia Boss mi naomba nimpumzike sasa! Kama ni uzoefu wapo wengi wanaoweza kukusaidia! Mimi naomba nipumzike kwa Sababu kuna Mambo ambayo nataka kufanya yanaweza kuathiri utendaji wangu.

Hakuafiki! akaniambia unaweza kuendelea tu kunisaidia na ukaendelea na mambo yako pia! Nikakataa nikamwambia hapana kabisa.

Basi baada ya Muda Shemasi akapandishwa cheo akahama pale,na muda huo huo yule jamaa akarudi toka masomoni,Akamshawishi jamaa kuwa msaidizi wake, jamaa nae akakataa kabisa akidai wapo wakongwe na watu wenye Uzoefu mzuri kuliko yeye! inakuwaje ametoka masomoni tu afikie kushika nafasi.

Basi akaniiita akanieleza kuwa jamaa amekataa akawa amenishilikisha kuwa kati ya Hawa (Akawataja Majina) na nani anafaa? sikuweka neno la ziada zaidi ya kusema wote wanafaa,basi akachagua mmoja wa wale alionitajia majina nikamuunga mkono kuwa huyo aliyechangua ni mtendaji mzuri anafaa.

Muda si Mrefu Nikawa nimepata Nafasi ya kusimamia zoezi flani hivi lina pesa kiasi! Nikawa Boss kwa muda sikuwa na roho ya Kinyongo - Ingawaje nilipomshirikisha Wife alinishauri nisimchague kwenye hilo zoezi kabisa,lakini sikufanya hivyo nikamteua na kuteua na watu wake wa Karibu bila Kinyongo tukamaliza ile kazi,kila mtu akapata cha kwake,ingawaje yeye aliacha kabisa kunipa deal za pesa,akawa anawapa wale wanaomfurahisha tu.

Sasa Jamaa baada ya Kuja kunisimulia jinsi alivyo nyanyaswa na Mkubwa wake kazini, nimegundua kwamba nilishamsamehe jamaa lakini bado nina maumivu na mbaya zaidi nimegundulika kuwa na Matatizo ya kiafya ambayo sikuwahi kuwa nayo huko nyuma na ni imani yangu ya kuwa kwa namna moja ama nyingine huyu jamaa alivyonitendea ndio chanzo cha hypertension yangu.

Naomba msaada ndugu zangu! Sihitaji kulipa kisasi,nahitaji maisha yangu yaendelee! nawezaje kuachilia nahisi kama bado ipo hali ya kuumia kila wakati ninapokumbuka yaliyonisibu.

Asanteni.
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
28,214
2,000
Mind your own business.

Concentrate sana kwenye present thing.

Mtu anaye concetrate kwenye past huwa anaishia kupata depression na stroke.njia ya kufuta past ni ku concentrate sana kwenye present.

Mleta mada present is more important than past .Mimi mtu akinikosea simuwazi wala nini naendelea na mambo yangu atajjiua huko mwenyewe.Siwezi acha kufanya mambo yangu kisa nimelibeba kichwani naliwazia jitu lililonikosea.
 

Jesusfreak08

JF-Expert Member
Jul 20, 2019
718
1,000
Unaweza ukasema umemsamehe mtu kumbe wapi hata uja msamehe lakini jambo zuri ambalo linaweza kukusaidia

1. Jiambie mwenyewe kuwa Huyu mtu nimemsamehe jiambie zaidi ya mara moja
2. Shukuru kwa kila jambo zuri ulilonalo na linalo tokea kwenye maisha yako
3. Mpe hongera huyo mtu kwa yale mazuri aliyoyafanya
4. Kwa kuwa wewe ni mkristo soma maandiko ukiyatafakari yatachukua nafasi ya yale maumivu na kuleta furaha
 

Ngosha Mashine

JF-Expert Member
Sep 21, 2017
400
1,000
Hakuna kitu kibaya kama kuhifadhi chuki inauma sana na mbaya zaidi unaumia sana wewe kuliko aliekukosea

Mimi kuna namna mbili tu nazitumia kuzitoa chuki

1:- KUSAMEHE
Hapa ili nisamehe ni mpaka huyo alienikosea aje akili mbele yangu kuwa kakosea na aniombe msamaha ndipo nitasamehe, asipo omba msahaha siwezi kusamehe maana huenda hajui kama kanikosea. Sasa nitamsamehe vipi mtu ambaye yeye anadhani hajanikosea, na asipofanya kuomba msamaha itaniongezea chuki zaidi itanifanya niamni kuwa jamaa ana kiburi na hapo ndipo nitaitumia njia ya pili ambayo ni.

2:-KULIPIZA KISASI
Ili niyatoe maumivu itabidi nilipize kisasi, hapa nitahisi kutulia maana maumivu yatakuwa yamehama kutoka kwangu na kuhamia kwa huyo alienikosea.

Kusema nijifanye nimesamehe bila kuombwa nisamehe nikujindanganya bure na siwezi, mbaya zaidi huyo alienikosea aendelee kuniudhi siwezi aiseeeeeeee
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
5,666
2,000
Kuna mbwa mmoja anaitwa Godfrey. Mbwa huyu nilimtoa jalalani na kanipigia MAGOTI mpaka nikaona ngoja nimsaidie. Alivyokuja Mara ya kwanza mabosi walimkataa lkn nilimpigia debe mpaka akaajiriwa. Lunch nikawa nampeleka za nguvu huyu mbwa kwa hela zangu. Bar na hotel asizojua tulienda nae ili apate uzoefu wa kuwa wa mujini. Eeeh bwanaeh.

Alipojua udhaifu wa big boss, alijipenyeza na majungu ya Khali ya juu mpaka kwa hiari yangu nikaacha kazi.

NEVER WAKE A SLEEPING DOG. IT WILL WAKE UP AND BITE YOU.

Na Ninyi wanawake msipende sana ku wa introduce marafiki zenu wa kike kwa boyfriend zenu au Waume zenu.
Wengi wamelia.
 

mulwanaka

JF-Expert Member
Feb 19, 2017
4,283
2,000
Mkuu hayo yote ta kawaida sana fitna majungu kama hayo nimepata mengi sanaa, mengine na ya sahau mengine hatasitaki kuyataja kwasababu naona haniongezee kitu.

'keep on focused on your goals' the only friend to trust is your self and probably your biological children. Wengine fyekelea mbali.
 

Miguel Alvarez

JF-Expert Member
May 28, 2019
379
500
Iko hivi kabla ya yote anza kufanya Toba ndani yako kwa kuwa ulkuwa na kinyongo nae na pia kuna muda ulimchukia hata kujaribu kulipa kisasi ndio maana ndani yako bado.kuna kitu kinachokufanya ukumbuke yale waliyokutenda kwa hali kama hiyo ni ngumu kusamehe, kwa. Kitu chochote kibaya ulichofanyiwa na mtu ukikumbuka ni ishara moja wapo yakujua kuwa hujasamehe,nakushauri hivi anza kwañza kumuomba Mungu akusamehe kwanza wewe ndio itakuwa wepesi kwako kusamehe wengine
 

iam Lucha

JF-Expert Member
Aug 24, 2018
1,926
2,000
inaonekana wewe ndo una wivu maana kwenye maelezo yote mm sijaona ubaya alio kufanyia huyo boss wako mpya, Sasa unaomba ushauri unataka ujue njia ya kumsamehe mtu ambae hajakukosea chochote?
 

Mnabuduhe

JF-Expert Member
May 8, 2015
348
1,000
inaonekana wewe ndo una wivu maana kwenye maelezo yote mm sijaona ubaya alio kufanyia huyo boss wako mpya, Sasa unaomba ushauri unataka ujue njia ya kumsamehe mtu ambae hajakukosea chochote?
Wivu wangu uko wapi hapo? Nisaidie!
Jamaa anawatangazia watumishi wenzagu kuwa sitakuja kukaa nikapata fursa - zinazopitia mkononi mwake! Ungelikuwa wewe ungefanyaje Kiongozi?
 

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
17,184
2,000
Mimi roho ya kusamehe niliiacha mwaka 2012 ( nilikua sijawah huru kiuchumi. Ivo ikawa inanilazimu kua Mpole )

Siku hizi roho yangu ni ya visasi tu .. Ukinifanyia ufedhuli, kama unahitaj nikulipue hapo hapo ,nakulipua, kama unahitaj twende kichwa kichwa tunaenda


Kikubwa Nilichofanya, Ni kutokuchukulia kwa uzito , Yaan Unanifanyia ubaya. Nachukulia poa, lkn ukae ukitambua dawa yako ipo jikoni inakwiva na utainywa tu.


Haya maisha yamenipa Amani sana !!


Kwa jambo kama lako, kwa sheria yangu, mimi sio mtu sahihi wa kukushauri hapa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom