eskobas2016
Member
- Jul 14, 2016
- 71
- 31
Habari wana Jamii Forums
Ninaomba msaada wa kisheria kuhusiana na mambo ya Bank kama mteja sikutendewa HAKI.
Tatizo lenyewe limetokea hivi.
Ilikuwa ni siku ya tarehe 4th / 08/ 2016 muda wa saa saba mchana, nilikwenda bank iitwayo Advance kuweka Float kwenye account yangu ya M-Pesa (wakala). Kwa kawaida ukifika kwa Teller huwa anakupa karatasi unaandika namba yako ya simu au code unazotumia plus jina lako na kiasi, nami nilifanya kama taratibu zilivyo na kumpatia dada muhusika ili aniwekee pesa zangu kwenye account yangu kiasi cha shilling Laki tatu. Alipomaliza kuweka akaniambia ‘Jina lako............’ Nikamwambia ‘’Hapana angalia kwenye hiyo karatasi nimeandika kila kitu iweje uniambie jina tofauti’’ naye akadai nimeandika kama ulivyoniandikia kwenye karatasi lakini imetokea jina tofauti. Nilimkatalia na kumwambia kuwa amekosea, ukweli dada alibisha na tumeshindana hivyo akijifanya hajakosea kwa takribani dakika Tano, sikutaka kubishana nae zaidi bali nilikwenda moja kwa moja kwa manager wa tawi nakueleza kisa kizima, yule dada akaitwa but still alikuwa anagoma ila manager alinambia kuwa kweli dada amekosea ila nenda na uje kesho tujue inakuwaje, nilikataa na kudai niludishiwe pesa yangu, ila manager wa bank alikataa na kudai hadi waludishiwe na Vodacom ndipo waniludishie, niligoma kutoka bank hadi wanipe pesa yangu ama float, sikutaka kuanzisha ugomvi kwani bank si mahala pa ugomvi, Ilibidi niwaambie wanipe barua ya uthibitisho kuwa kweli wamekosea na wana pesa zangu. Wakanipatia. Leo 5th nimeludi bank wakadai hawana la kufanya hadi vodacom wawaludishie ndipo wanipatie ila hawajui ni lini but within 7days. Ukweli niliingiwa hasira kwani makosa wamefanya wao, pesa hawataki niludishia float hawataki kunipa, pesa yangu ya mzunguko wa biashara yangu wameipunguza, muda wangu wamenipotezea. Naomba wanaojua sheria wanisaidie hapa TAFADHALI.
1. Nifanyeje ili waniludishie pesa yangu as soon as possible (kisheria )
2. Wanilipe
a. Usumbufu walionisababishia
b. Muda wangu walionipotezea
c. Gharama za kwenda na kuludi bank kudai pesa yangu kwa siku tatu
3. Kashfa na manyanyaso waliyonionyesha.
4. Kuyumbisha biashara yangu na kunisababishia hasara kwa siku kadhaa
Thank you so much.