Naomba msaada kwa wanaojua SHERIA ZA BANK (nimeonewa)

eskobas2016

Member
Jul 14, 2016
71
31
Habari wana Jamii Forums
Ninaomba msaada wa kisheria kuhusiana na mambo ya Bank kama mteja sikutendewa HAKI.

Tatizo lenyewe limetokea hivi.
Ilikuwa ni siku ya tarehe 4th / 08/ 2016 muda wa saa saba mchana, nilikwenda bank iitwayo Advance kuweka Float kwenye account yangu ya M-Pesa (wakala). Kwa kawaida ukifika kwa Teller huwa anakupa karatasi unaandika namba yako ya simu au code unazotumia plus jina lako na kiasi, nami nilifanya kama taratibu zilivyo na kumpatia dada muhusika ili aniwekee pesa zangu kwenye account yangu kiasi cha shilling Laki tatu. Alipomaliza kuweka akaniambia ‘Jina lako............’ Nikamwambia ‘’Hapana angalia kwenye hiyo karatasi nimeandika kila kitu iweje uniambie jina tofauti’’ naye akadai nimeandika kama ulivyoniandikia kwenye karatasi lakini imetokea jina tofauti. Nilimkatalia na kumwambia kuwa amekosea, ukweli dada alibisha na tumeshindana hivyo akijifanya hajakosea kwa takribani dakika Tano, sikutaka kubishana nae zaidi bali nilikwenda moja kwa moja kwa manager wa tawi nakueleza kisa kizima, yule dada akaitwa but still alikuwa anagoma ila manager alinambia kuwa kweli dada amekosea ila nenda na uje kesho tujue inakuwaje, nilikataa na kudai niludishiwe pesa yangu, ila manager wa bank alikataa na kudai hadi waludishiwe na Vodacom ndipo waniludishie, niligoma kutoka bank hadi wanipe pesa yangu ama float, sikutaka kuanzisha ugomvi kwani bank si mahala pa ugomvi, Ilibidi niwaambie wanipe barua ya uthibitisho kuwa kweli wamekosea na wana pesa zangu. Wakanipatia. Leo 5th nimeludi bank wakadai hawana la kufanya hadi vodacom wawaludishie ndipo wanipatie ila hawajui ni lini but within 7days. Ukweli niliingiwa hasira kwani makosa wamefanya wao, pesa hawataki niludishia float hawataki kunipa, pesa yangu ya mzunguko wa biashara yangu wameipunguza, muda wangu wamenipotezea. Naomba wanaojua sheria wanisaidie hapa TAFADHALI.

1. Nifanyeje ili waniludishie pesa yangu as soon as possible (kisheria )

2. Wanilipe

a. Usumbufu walionisababishia

b. Muda wangu walionipotezea

c. Gharama za kwenda na kuludi bank kudai pesa yangu kwa siku tatu

3. Kashfa na manyanyaso waliyonionyesha.

4. Kuyumbisha biashara yangu na kunisababishia hasara kwa siku kadhaa

Thank you so much.
 
Ndio bank zatu. Nenda kwa mwana sheria au nenda kwa coo wa bank maana hii imekaa vibaya
 
Hakikisha tu ile karatasi uliyomundikia unayo...ingewezekana kama ile cku.ya kwanza wao wangeigonga stamp na kuiambatanisha na iyo barua.
 
Hii ni personal promblem na sio kosa la bank umempa mtu akuwekee pesa yako akaacha kufanya kama vile taratibu za kibank zinavyoelekeza yeye akafanya anavyojua yy mwenyewe iweje sasa uanze kuidai bank?? Huyu dada uliempa pesa zako na yy akafanya kinyume na taratibu za kibank ndoa wa kushitaki kama angekuwa ametuma kwa jina lile lile na pesa haikufika kwako hapo ndo ungeshitaki bank husika ila kwa kuwa kakosea yy mwenyewe nenda polis fungua case dhidi ya huyu dada maana ndo anajua ni nani alimtumia pesa maana alifanya kinyume na utaratibu wa kaz yake akaamua kutuma pesa kwa mtu.mwingine ama kwa bahat mbaya au makusudi.....
 
Sio personal problem aisee!! Unafikiri kila kosa linalofanywa na kampuni halifanywi na watu? Ngoja tusubiri wanasheria, ila kwa ufahamu wangu wa kiasi juu ya sheria, hapo benki inawajibika. Baada ya kuwajibika ndio watadili wenyewe na huyo mhudumu wao
 
Kuwa mvumilivu subiri huo muda walio sema! iKISHINDIKANA peleka malalamiko yakpo BOT(Benk kuu) Ndio wasimamizi na wafuatiliaji wa mienendo ya mabenki yote.
 
Hii ni personal promblem na sio kosa la bank umempa mtu akuwekee pesa yako akaacha kufanya kama vile taratibu za kibank zinavyoelekeza yeye akafanya anavyojua yy mwenyewe iweje sasa uanze kuidai bank?? Huyu dada uliempa pesa zako na yy akafanya kinyume na taratibu za kibank ndoa wa kushitaki kama angekuwa ametuma kwa jina lile lile na pesa haikufika kwako hapo ndo ungeshitaki bank husika ila kwa kuwa kakosea yy mwenyewe nenda polis fungua case dhidi ya huyu dada maana ndo anajua ni nani alimtumia pesa maana alifanya kinyume na utaratibu wa kaz yake akaamua kutuma pesa kwa mtu.mwingine ama kwa bahat mbaya au makusudi.....
Dada kaajiliwa na bank,so bank ndo inawajibika then wao kwa wao ndo watadili na huyo dada kama staff wao
 
Hii ni personal promblem na sio kosa la bank umempa mtu akuwekee pesa yako akaacha kufanya kama vile taratibu za kibank zinavyoelekeza yeye akafanya anavyojua yy mwenyewe iweje sasa uanze kuidai bank?? Huyu dada uliempa pesa zako na yy akafanya kinyume na taratibu za kibank ndoa wa kushitaki kama angekuwa ametuma kwa jina lile lile na pesa haikufika kwako hapo ndo ungeshitaki bank husika ila kwa kuwa kakosea yy mwenyewe nenda polis fungua case dhidi ya huyu dada maana ndo anajua ni nani alimtumia pesa maana alifanya kinyume na utaratibu wa kaz yake akaamua kutuma pesa kwa mtu.mwingine ama kwa bahat mbaya au makusudi.....
Sio personal problem hio mkuu...
 
Pesa huchukua zaidi ya siku Tatu kurudi.. Kuwa mvumilivu. Kesi unaiweza gharama yake?
 
Hii ni personal promblem na sio kosa la bank umempa mtu akuwekee pesa yako akaacha kufanya kama vile taratibu za kibank zinavyoelekeza yeye akafanya anavyojua yy mwenyewe iweje sasa uanze kuidai bank?? Huyu dada uliempa pesa zako na yy akafanya kinyume na taratibu za kibank ndoa wa kushitaki kama angekuwa ametuma kwa jina lile lile na pesa haikufika kwako hapo ndo ungeshitaki bank husika ila kwa kuwa kakosea yy mwenyewe nenda polis fungua case dhidi ya huyu dada maana ndo anajua ni nani alimtumia pesa maana alifanya kinyume na utaratibu wa kaz yake akaamua kutuma pesa kwa mtu.mwingine ama kwa bahat mbaya au makusudi.....
Kama hujui kitu bora utulie kimya...kwani bank ni majengo na jina au ni watu?
Unaposema teller akifanya kosa nia personal una maana gani?
 
Hii ni personal promblem na sio kosa la bank umempa mtu akuwekee pesa yako akaacha kufanya kama vile taratibu za kibank zinavyoelekeza yeye akafanya anavyojua yy mwenyewe iweje sasa uanze kuidai bank?? Huyu dada uliempa pesa zako na yy akafanya kinyume na taratibu za kibank ndoa wa kushitaki kama angekuwa ametuma kwa jina lile lile na pesa haikufika kwako hapo ndo ungeshitaki bank husika ila kwa kuwa kakosea yy mwenyewe nenda polis fungua case dhidi ya huyu dada maana ndo anajua ni nani alimtumia pesa maana alifanya kinyume na utaratibu wa kaz yake akaamua kutuma pesa kwa mtu.mwingine ama kwa bahat mbaya au makusudi.....
Hiyo sio personal issue, huyo dada ni muajiriwa wa bank na yupo hapo kwa niaba ya bank hivyo bank wana kila sababu ya kuwajibika. Refer: Kesi ya Dk.Magu na ile meli ,serikali ilibidi ilipe kwa sababu Magu alifanya kwa niaba ya serikali.
 
Hii ni personal promblem na sio kosa la bank umempa mtu akuwekee pesa yako akaacha kufanya kama vile taratibu za kibank zinavyoelekeza yeye akafanya anavyojua yy mwenyewe iweje sasa uanze kuidai bank?? Huyu dada uliempa pesa zako na yy akafanya kinyume na taratibu za kibank ndoa wa kushitaki kama angekuwa ametuma kwa jina lile lile na pesa haikufika kwako hapo ndo ungeshitaki bank husika ila kwa kuwa kakosea yy mwenyewe nenda polis fungua case dhidi ya huyu dada maana ndo anajua ni nani alimtumia pesa maana alifanya kinyume na utaratibu wa kaz yake akaamua kutuma pesa kwa mtu.mwingine ama kwa bahat mbaya au makusudi.....
Acha kukurupuka kama hujui
 
Kisheria taasisi inawajibika kwa kosa lililiofanywa na mfanyakazi wake akiwa katika utekelezaji wake wa majukumu ya kiofisi.Teller ni mtumishi wa benk.Teller alipokosea namba za mteja kuweka pesa alikuwa akifanya hivo kaika utekelezaji wa majukumu yake kama mtumishi wa benki.Kwa maana hiyo benki inawajibika moja kwa moja kwa kosa lililotendwa na mfanyakazi wake akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kikazi.Ushauri wangu:Kuwa na subira kaka usijeukaharibu na ukajitia gharama zisizoza msingi.Ikishindikana tupeana taarifa zaid
 
CHA MSINGI NI VYEMA UKIPATWA NA CHANGAMOTO KAMA HIZI KWA YEYOTE ULE, UWE UNATUNZA NYARAKA MBALIMBALI UNAZOTOA AU KUPOKEA KWENYE MAMBO MUHIMU KAMA HAYA, NA NI VIZURI KUWA UNATOA COPY YA NYARAKA YOYOTE UNAYOWASILISHA POPOTE PALE AU UKISHAPOKEA KOKOTE KULE. HIVYO MWISHO WA SIKU HUWA EVIDENCE KAMILI YA MLOLONGO MZIMA NA KUSAIDIA KAZI YA KOSA KUWA RAHISI, POLISI HADI MAHAKAMANI.
 
nenda makao makuu strait kwa chief operating oficer peleka madai yako moja kwa moja branch manager hawez saidia maana anajilinda yeye na mtu wake,hili si kosa la mteja hata kidogo wala hatakiwi kuwa sehemu ya kusubiria hiyo kampuni ya simu irudishe bali alipaswa awekewe float upla hiyo hasara waibook
 
Kesi ya 2016 aende kwa Branch Manager mwaka 2019?!

Bila shaka muhusika alirudishiwa pesa zake ndani ya siku saba
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom