Naomba msaada kwa Mwanasheria mwenye namba ya DPP

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Kuna tukio lilitokea Mwanza mwaka jana,kwa ufupi mwanajeshi na mgambo waliwapiga watuhumiwa, ndani ya ofisi ya kata, mmoja alifariki. Polisi walidanganya marehemu aliuwawa na wananchi.

Baadae mke wa marehemu alimuona mkuu wa mkoa,na upelelezi ukafanyika na maelezo yakachukuliwa,na kesi ilikuwa imefunguliwa. Jalada lilienda kwa mwanasheria wa mkoa.

Lakini mpaka hivi sasa watuhumiwa hawajakamatwa. Mwanasheria wa mkoa anasema ameshafungua mashitaka anasubiri watuhumiwa wakamatwe,ila Rco anawakingia kifua. Naomba msaada mwenye namba ya Dpp ili aweze kusaidia.
 
Hili la kubambikiza kesi hata JPM analifahamu.

Chagu wa mawingu kafanya nini jiwe kuliondoa hilo tatizo la bambikizi?

Hujasikia wa kwa Heche wa kampeni? Wanashitakiwa kwa ujambazi wa kutumia silaha.

Wale wagombea wa njombe ticket ya cdm? Wanashitakiwa kwa kesi ya mauaji. Je nduguye kachero mbobezi? Kutakatisha pesa.

Subiria usikie body guard wa Esther Bulaya. Ukisikia alikuwa kuwadi wa mashoga usiseme miye nabii.

Tanzania ya jiwe haina haki wala uhuru.

Ndiyo maana Oct. 28 tuna jambo letu naye. Akitaka kutuchezea wallah patachimbika.

Hiiiii bagosha!
 
Kuna tukio lilitokea Mwanza mwaka jana,kwa ufupi mwanajeshi na mgambo waliwapiga watuhumiwa, ndani ya ofisi ya kata, mmoja alifariki. Polisi walidanganya marehemu aliuwawa na wananchi.

Baadae mke wa marehemu alimuona mkuu wa mkoa,na upelelezi ukafanyika na maelezo yakachukuliwa,na kesi ilikuwa imefunguliwa. Jalada lilienda kwa mwanasheria wa mkoa.

Lakini mpaka hivi sasa watuhumiwa hawajakamatwa. Mwanasheria wa mkoa anasema ameshafungua mashitaka anasubiri watuhumiwa wakamatwe,ila Rco anawakingia kifua. Naomba msaada mwenye namba ya Dpp ili aweze kusaidia.
Suala la haki halina ushabiki wa vyama wekeni kando Uchadema, hawa watumishi wa chini ndio wanamkwamisha JPM.
 
Unataka kutukumbuka kama kina Zuchu yanapowakuteni?

Kwani wewe unadhani yale mabomu ya Serengeti, ifakara, kahama etc; Ile engua engua za wagombea; Ile simamisha simamisha ya wagombea kukampeni nk; zinatofauti yoyote na hizi bambikizi ambazo mzizi wake ni kutokuwapo kwa haki unakokuongelea leo hapa mburula wewe? Tuseme wewe ndiyo kwanza umetoka sayari nyingine?

Yapo mengi mno bwana Mawingu. Kwamba tumechoka? Tumechoka kweli kweli!

La maana ambalo jiwe angefanya hapa tulipo, ilikuwa kukabidhi nchi kwa amani akaenda zake kuchunga ng'ombe na farasi wake Chatto.

Serikali mpya haitakuwa na visasi kama yake.
 
Tatizo lako wewe unabase kuangalia wanaCdm wanaopigwa mabomu au kuenguliwa bila kuangalia chanzo.

Mimi nataka haki sawa kwa kila mtanzania,ndio maana JPM huwa anawatumbua watumishi wanaokandamiza haki za wananchi.
 
Hukuwahi kusikia nyani huwa haoni kundule jombi?

Ungejiridhisha kuona kama unaona lako mjomba?
 
Chanzo cha watu au wanasiasa kunyimwa haki zao ndio suluhu hapa.

Sio wote wanaonewa pia. Kuona kundule nyani akitumia kioo analioana.
 
Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

Anwani/Mahali OFISI YA TAIFA YA MASHTAKA, Chuo cha Masomo ya Biashara na Sheria cha Chuo Kikuu cha Dodoma- UDOM, S.L.P 1733, Dodoma,Tanzania
Simupapo: +255 26 2963634
Nukushi: Nō: +255 26 2963635
Barua Pepe: dpp@nps.go.tz
Hii ni ya makarani wake tu, sisi tunataka kumtwangia ya mkononi, maana mwendesha mashitaka mkoa wa mwanza ananyima watu haki zao.
 
Chanzo cha watu au wanasiasa kunyimwa haki zao ndio suluhu hapa.

Sio wote wanaonewa pia. Kuona kundule nyani akitumia kioo analioana.
Basi tumia kioo jombi.

Kama si wote wanaoonewa, wengine wanaonewa. Ndiko kukokosekana haki huko. Ndiyo maana uko busy sasa kutafuta namba ya DPP.

Katafiti wanaoonewa ni wengi kama wote tu.
 
Kuna tukio lilitokea Mwanza mwaka jana,kwa ufupi mwanajeshi na mgambo waliwapiga watuhumiwa, ndani ya ofisi ya kata, mmoja alifariki. Polisi walidanganya marehemu aliuwawa na wananchi.

Baadae mke wa marehemu alimuona mkuu wa mkoa,na upelelezi ukafanyika na maelezo yakachukuliwa,na kesi ilikuwa imefunguliwa. Jalada lilienda kwa mwanasheria wa mkoa.

Lakini mpaka hivi sasa watuhumiwa hawajakamatwa. Mwanasheria wa mkoa anasema ameshafungua mashitaka anasubiri watuhumiwa wakamatwe,ila Rco anawakingia kifua. Naomba msaada mwenye namba ya Dpp ili aweze kusaidia.
Raisi wa wanyonge tayari ana taarifa zake. Wewe tulia hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom