Naomba msaada kuhusu huyu mpenzi

Naomba msaada kuhusu huyu mpenzi

Sirm

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2013
Posts
561
Reaction score
370
Nilipewa namba ya msichana na rafiki yangu mmoja, nilichat nae kwa muda mrefu hadi tukawa wapenzi.

Kipindi cha karibuni nilimuuliza kiutani kama aliwahi kua na Boyfriend akawa hataki kunijibu, lakini niliamua kumsisitizia swali hilo hadi akaamua kuniambia kua ni kweli anae na akaniambia "NAOMBA TUACHANE".

Nilipomuuliza kwanini akanambia kwasababu kuna mtu ANAMPENDA kama vile mimi ninavyompenda yeye.

Nilichoamua kumuomba ni mimi kuonana na yeye ukichukulia ni kama mwezi mmoja tangu tufahamiane.

Kakubali tuonane kesho lakini nimebaki na mawazo ni vitu gani hasa natakiwa nivifanye;-

1)Kwasababu hatujawahi kuonana nianze kumtongoza upya?
2)Nianze kwa kumbembeleza asiniache?
3)Hakuna jipya litakalotokea bora nisiende nitazidi kuumia moyo tu!

Naombeni mnipe ushauri jamani nimechanganyikiwa!
 
umechanganya jukwaa mkuu hii habari peleka mmu watakupa ushauri utakaokusaidia!
 
kwa haraka haraka unaonekana kua mtu wa wasiwasi wasiwasi!nenda ulikoelekezwa"
 
Hahaha utapewa Hata namba za majini uyatongoze alafu cku ya appointment yakunyonye damu. Ndg zako wanataarifa maana unaweza ukawa kama ndege ya Malaysia
 
Mdanganye ubonyeze 0713 ukifanikiwa hatokusumbua tena wala kukuambia ujinga kama huo tena
 
Kashakwambia ana mtu wake ya nn kung'ang'ania?
Unataka kuharibu mapenzi ya watu ww
 
Unapoomba kuna majibu mawili kukubaliwa au kukataliwa,
Huenda katika nawasiliano yenu kaona huna vigezo anavyotafuta hivyo kaamua kuuvunja uhusiano.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom