Naomba mnisaidie | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba mnisaidie

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Lady, Jan 20, 2011.

 1. L

  Lady JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kisiju ipo wapi?
  Kutoka Dar mpaka kufika hapo kuna usafiri gani na gharama zikoje?
  Nilipata taarifa kuwa kuna kuku wa kienyeji, katika mchakato wa kutaka kupunguza makali ya maisha nataka kuanza biashara ya kuku wa kienyeji. Nimeambiwa huko kuna kuku, naomba anayejua pia kuku wa kienyeji wanaweza kupatikana kwa bei ya jumla shilingi ngapi?
   
 2. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nakushauri, kabla hujaingia kwenye biashara usio ielewa kwanza endelea kufanya utafiti wa hiyo biashara. mfano; mayai ya kienyeji trey bei yake ni pesa ngapi? na wewe unataka kuuza nyama ya kuku za kienyeji au focus yako ni mayai wa kienyeji? Na je umejiandaa vipi kukabiliana na magonjwa ya kuku? Get to know mtaalam wa mifugo. Usikurupuke chunga sana you may cry with one eye!!
   
 3. N

  Neytemu Member

  #3
  Jan 20, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Natafuta sana pia wapi karibu na Dar nawezapata kuku wa kienyeji wakufuga.nilikua nao wachache toka Singida nikaamua kuwaongeza kwa kununua wa kutoka sokoni Buguruni haikuchukua muda wakafa wote.

  Ni biashara nzuri ila inahitaji uangalifu.
   
 4. M

  Malila JF-Expert Member

  #4
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ngoja nikujibu swali lako,

  Kisiju iko wilaya ya Mkuranga,kuna bandari hapo ya kwenda Mafya, na kuna bandari mpya inaitwa Nyamisati. Kimsingi Kisiju hakuna kuku wa kienyeji,isipokuwa kuku aina ya kuchi kutoka kisiwa cha Juani huko Mafya hufikia pale Kisiju bandarini na wajanja huwachukulia pale. Ukifika Mkuranga wilayani pale,ingia mkono wa kushoto,yaani unaiacha barabara ya Mtwara wewe unaingia kushoto. Na kama unaweza kujitoa mhanga, nenda Mbagala,pale kuna daladala za kisiju kwenda na kurudi kila siku.

  Usiku mwema.
   
 5. M

  Malila JF-Expert Member

  #5
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kama unataka kuwa mfugaji mzuri,mbegu bora ni muhimu,huwezi kupata mbegu bora sokoni kwa sababu wakulima hupenda kuuza kuku wasio na sifa(wasiotunza vifaranga,au wasiotaga mayai mengi,au wanaosusa kuatamia nk), kuku wa Singida dili zuri,lakini unatakiwa kuwa makini sana wakati unawasafirisha toka Singida kuja huku.

  Wape tiba huko huko Singida kabla hawajaanza safari, naamini ukiwaona watalaamu wa kuku watakupa utalaam zaidi ili ukipata kuku wageni siku nyingine usiwachanganye na wenyeji mapema.

  Vipi wale bata mzinga bado unao? Bado niko nje ya Dar, nikirudi nitakutafuta ili tumalize biashara kabisa,kwa sababu nawataka ili nifuge, sasa usiniuzie bata kimeo!!!!!!!
   
 6. L

  Lady JF-Expert Member

  #6
  Jan 21, 2011
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nashukuru kaka.
   
 7. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #7
  Jan 21, 2011
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,807
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Asante sana Malila kwa ushauri wa nguvu mwenyewe nilwahi kutoa kuku toka Arusha kwaajili ya kuwafuga lakini walipofika hapa Dsm wakakaa mwezi tu wakaanza kufa kwa haraka sana
   
 8. N

  Neytemu Member

  #8
  Jan 21, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks Malila.
  kuku wa Singida wazuri mno!ningefurahi kuunganishwa na mtu/watu wanaowasafirisha kuja Dar nione kama naweza kuagiza.

  Kuhusu Bata Mzinga watakuwepo hapa Dar nafikiri baada ya wiki mbili zijazo na utajichagulia mwenyewe,ukiweza kuja na mtaalamu akusaidie kuchagua mazao bora ruksa
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Jan 21, 2011
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Nina kijana wangu kwao Singida,nataka akanichukulie kuku wa majaribio ili nichanganye na kuchi toka Mafya nipate breed mpya. Naamini nikija dar mwezi ujao itabidi tutafutane ili tusaidiane kwa hii mipango. Bata nitakuja niwachague bila taabu.
   
 10. N

  Neytemu Member

  #10
  Jan 22, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks Malila ukifika tutafutane soon.nataka sana kuku bora wa kienyeji kwa ajili ya mayai.
   
Loading...