V V T-I ni Variable Valve Timming,kwa engine ya cylinder 6 ina valve 24 yaani inlet 12 na exhaust valves 12.Katika inlet manifold kuna censor ambayo ni controlled na throtle au engine depression na wamelink na engine controlls.Iwapo gari inatembea katika speed chini ya 60kmh to 80kmh valve 12 yaani 6 za inlet na 6 za exhaust hujifunga na kubaki valve 12 tu zinafanya kazi yaani 6 inlet na 6 exhaust.Speed ya gari ikizidi 60 au 80kmh(inategemea setting) valve zingine 12 zinafungua na kufanya valve 24 zote zifanye kazi hivo engine perfomance inaongezeka na fuel consuption inapungua.Ndiyo maana kwa gari kama GX-100 kutembelea hapa mjini ktk foleni na speed ndogo utalalamika inakula mafuta sana tofauti ukiingia safari ndefu ndiyo utaona raha yake zile down za chalinze mpaka segera unapanda na 120kmh bila gari kupungua nguvu.Kifupi hizi ni gari za masafa siyo za kutanulia mjini.Kuhusu technologia wapo vijana wanatengeneza sana,hapa Dar nenda Mivinjeni Garage ya Mabenzi kwa kijazi vijana wapo.Kama kuna ishu complicated wanaingia ktk computer.Siku hizi manual zipo ndani ya mtandao ukilog-in aina sahihi ya engine na taarifa sahihi unapata kila kitu hata majibu ya trouble shooting.