Naomba mchango wa harusi

Naomba mchango wa harusi

Zeni2017

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
1,247
Reaction score
534
Mtu hujikuna anapopafikia!

Tajiri hakusanyi michango ya harusi. Huwezi kusikia Jay Z anaomba mchango wa harusi.

Kijijini mzee mwenye uwezo wake akifanya shughuli ya mwanawe kijiji kizima kitatingishika lakini haombi mchango wa harusi.

Ngoma iko kwa makabwela wa mjini. Holi la harusi milioni kumi. Bwana harusi elfu kumi benki hana.

Hapo ni mwendo wa michango. Yaani michango kiasi utamkuta mtu anakuhesabia michango ya harusi ni sehemu ya matumizi yake ya mshahara.

Ujinga tuache. Una milioni 30 yako unataka kuitumbua siku moja kwenye harusi. Fanya harusi alika watu waje na zawadi tu.

Ingekuwa la maana mtu akikwama ada ya shule mwaka wa mwisho achapishe kadi kwa ndugu na jamaa wamsaidie. Na anaweza kupanga siku watu wakaja na michango yao kukawa na tafrija ndogo na vinywaji watu wakafurahi.

Si tunaiga wazungu? Wenzetu wana rent party. Mtu akikosa kodi akiwa karibu kufukuzwa kwenye nyumba wanafanya pati michango inakusanywa mwenye shida anasaidiwa.

Utafikiri wabongo sio wabunifu. Ni wabunifu mno ila kwenye vitu vya hovyo hovyo. Utakuta bwana harusi kavalishwa gagulo la mtemi Mirambo, kilemba cha Tippu Tip bado gobore tu afanane na muuza watumwa. Wengine wanavaa makoti ya kuendeshea meli yaani tafarani mtindo mmoja. Kesho asubuhi bwana na bibi harusi wana madeni na kodi ya nyumba hawana.

Ushauri wa bure tufanyeni harusi ndogo halafu tuwe na utaratibu wa kuwakabidhi maharusi zile pesa za michango ili ziwasaidie kuanza maisha.
 
Ukisema uwape michango waanzie maisha kuna watu watakuwa wanaoa na kuacha kila mwaka. Suala la harusi ni suala zito sana na kwa sasa makabwela hata ingekuwa harusi yenye gharama ya Tsh milioni 5 bado tungeomba michango tu.

Cha msingi nadhani tusiwekeane viwango tu, kama nina elfu 10 chukua hiyo hiyo.
 
Mnapowekwa kwenye kamati mnachekelea lakini mnalalamika!
 
Duuh mke wakwako mtonyo wakwetu kweli bongo bahati mbaya
 
Ukisema uwape michango waanzie maisha kuna watu watakuwa wanaoa na kuacha kila mwaka. Suala la harusi ni suala zito sana na kwa sasa makabwela hata ingekuwa harusi yenye gharama ya Tsh milioni 5 bado tungeomba michango tu.

Cha msingi nadhani tusiwekeane viwango tu, kama nina elfu 10 chukua hiyo hiyo.
PRODA LTD
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hivi bado mnachangianaga michango ya harusi? nilishaacha siku nyingi na siku ya kuolewa kwangu nitamwambia huyo mwanamume kwetu hatunaga michango, kuna mahari na kwenda kanisani full stop. akiamua kuchangishana kwao ni juu yake na tukishaoana hakuna kumchangia mtu.

Nshachoka mie
 
Haya mambo ya kijinga we acha tu. Juzi juzi mmoja kidogo anirudishe wodini kwa kupandwa na nyongo. Alinitumia ujumbe huu:

Habari mpendwa, nakukumbusha mchango wa harusi ya (Jina lake)
itakayofanyika tarehe (siku iliyolaaniwa).
Wewe ni mtu wa muhimu sana kwangu, nakutegemea.
Muda uliobaki ni mchache sana kufanya maandalizi.
Mchango wako ufikishe kwenye namba 07XX656X67,
07X576X789 (Jina Lake).
Asante na Mungu akubariki!
​

Wakati ananitumia ujumbe wake huu mimi ndio kwanza niko wodini nauguza donda la operesheni. Nikamjibu kwa kumueleza hali yangu, naye akahitimisha kwa neno POLE SANA. Babake zake, mpk wa leo ni mwezi sasa sijasikia lolote toke kwake. Ndio najiuliza, MTU MUHIMU KWAKE ameshasahaulika?
 
ahhaaaaa eti siku iliyolaaniwa ahahaaa jamani
 
Moja ya biashara ambayo imenishinda ni hii, sipendi na siiwezi kabisa.
 
Yani mimi Mpaka Nikasema nipo nje ya mji
Bora aisee ulivyowadanganya mana hadi unakosa amani kwa sababu kila simu ikiita unawaza uongo wa kuwaambia.

Ila saa nyingine wanazidi pale wanapofanya ni jambo la lazima wakati ni hiari.
 
Hii habari inakera kwakweli yaan mtu akikupa kadi ya mchango wa harusi inakuwa kama deni,watu wajipange kwanini wasifanye sherehe kulingana na uwezo wao?
 
Bora aisee ulivyowadanganya mana hadi unakosa amani kwa sababu kila simu ikiita unawaza uongo wa kuwaambia.

Ila saa nyingine wanazidi pale wanapofanya ni jambo la lazima wakati ni hiari.
Yani kila siku message mwisho wakutuma mchango mchango. Atanipa mkewe na mimi nimfaidi au
 
Yaani hela nitoe mm halafu raha ya kukojozana mpate nyie.
 
Back
Top Bottom