Are You Great Thinkers?.
Busara ni pamoja na kukubali jambo usilolielewa na kuacha wanaolielewa kuchangia.Badala ya kumshambulia mtoa hoja katika namna ya majibu ya DHIHAKA ni bora usichangie lolote na utakuwa umeisaidia jamii forum kwa kutokuwa na midahalo mingi isiyo na msingi pamoja na kuishushia hadhi.
Kuanzia kwa Jambo Forums na baadaye Jamii Forums ya Mwanzoni na hadi kufikia Miaka ya Juzi 2015 kurudi nyuma ilikuwa ni Pahala pema pa miongoni mwetu kujifunza mengi katika namna ya Busara sana.Hakukuwa na Haya majibu ya Facebook wala Instagram.
Leo hii kila mtu anaanzisha mada yeyote na Kuchangia chochote kwa kisingizio cha Jina feki.Ikumbukwe kuwa "Japo tunatumia Usernames na Avatar tofauti,hilo halibadilishi uhalisia wa nafsi na Mioyo yetu".Tuwe wataarabu na tusiigize ustaarabu.
Binafsi Nachukizwa na Majibu ya Hovyo humu Jamii Forums.Kama huna la kuchangia Ni BORA UKAE KIMYA.
Back to the question.Mkuu
Felice1 ,Namna bora ya kuongeza Uwezo na stadi ya kuzungumza katika halaiki ya watu ni Kusoma vitabu,Articles mbalimbali kuhusu PUBLIC SPEAKING pamoja na Kuhudhuria semina mbali-mbali kuhusu hitaji yako.Kwa kuufuata huu ushauri utajikuta uki-master Kuzungumza mbele ya watu katika namna isiyoelezeka.
I stand to be corrected.