Naomba mawazo yako! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naomba mawazo yako!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Oman - Muscat., Jan 13, 2012.

  1. Oman - Muscat.

    Oman - Muscat. Member

    #1
    Jan 13, 2012
    Joined: Jan 1, 2012
    Messages: 38
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Za asubuhi ndugu zangu!
    Naombeni mnishauri nini cha kufanya kupunguza maumivu ya kuachana na mpenzi wako wa muda mrefu.
    Nimeachana na shemeji yenu jana na hali yangu ki roho si nzuri kabisa hata moyo wangu umekua unauma sana kiasi nahisi nakosa nguvu.
    Thanks in advence.
     
  2. T

    Tall JF-Expert Member

    #2
    Jan 13, 2012
    Joined: Feb 27, 2010
    Messages: 1,433
    Likes Received: 5
    Trophy Points: 0
    1.Umemuacha ambae bado unampenda.POLE SANA.......huenda yeye ndie kakuacha au umemwacha kwa hasira.
    2. Kama unaweza kusamehe na mkarekebisha...rudiana nae ili upate kile ROHO INAPENDA..KAMA HAIWEZEKANI.

    TAFUTA MBADALA HARAKA SANA.
    1.Tafuta mtu ambae atakuwa na sifa zaidi ya zile alizokuwa nazo.
    2. Futa kumbukumbu zake zote kwako eg. namba za simu, e mail, picha zake weka mbali na wala usiwasiliane na wale wote waliokuwa connected nae.
    3. Ule wakati ambao huwa mnakuwa wote fanya kitu mbadala eg kusoma vitabu,michezo,kunywa au kwenda club or any social activity.
     
  3. fazaa

    fazaa JF-Expert Member

    #3
    Jan 13, 2012
    Joined: May 20, 2009
    Messages: 2,986
    Likes Received: 8
    Trophy Points: 0
    Kwanza wewe ni mwanamke au mwanaume?

    Pili tatizo ni aje mana mpenzi wako wa mda mrefu vipi muachane? c ndo hapo nashangaaaaaaa!!

    Kama ni mwanaume wanawake wameisha kuwa wengi asikubabaishe utapata tu wengine.

    Kama ni mwanamke hapo kazi usikimbilie kupenda mwingine mara moja unaweza kutangaziwa kama malaya.


    Kama ni mwanamke cool down kwa mda afu nenda kwa step usije kukutana na dume lingine huni ukawachwa tena.
     
  4. Judgement

    Judgement JF-Expert Member

    #4
    Jan 13, 2012
    Joined: Nov 13, 2011
    Messages: 10,361
    Likes Received: 61
    Trophy Points: 145
    OMAN sometimes sisi wachangiaji Thread inatuwia vigumu namna ya kupanga maneno ikiwa hatuelewi tunaemwambia ni mtu wa Jinsia gani ! Ofcoz mimi sioni mantik ya ku'hide gendar sanasana kwangu mie naona kama ni uhuni flani hivi.
     
  5. c

    cheks lady Member

    #5
    Jan 13, 2012
    Joined: Dec 11, 2011
    Messages: 6
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    ingawaje hujaonesha deteils vizuri....., itategemea kama uliyemuacha unampenda ama laa! au umeachwa?,, je tatizo ni kubwa?,,, na je linasovika!
     
  6. Annael

    Annael JF-Expert Member

    #6
    Jan 13, 2012
    Joined: Sep 26, 2011
    Messages: 9,101
    Likes Received: 5,214
    Trophy Points: 280
    Nenda kamshitaki kwa mwenyekiti wa mtaa
     
  7. Smile

    Smile JF-Expert Member

    #7
    Jan 13, 2012
    Joined: Jul 18, 2011
    Messages: 15,407
    Likes Received: 125
    Trophy Points: 160
    nichukue mimi
     
  8. Cantalisia

    Cantalisia JF-Expert Member

    #8
    Jan 13, 2012
    Joined: Sep 26, 2011
    Messages: 5,227
    Likes Received: 9
    Trophy Points: 135
    Pole sana mshukuru mungu kwa hilo,
    Jaribu kuji kip bize na ishu nyingine,
    Mwombe mungu atakupatia aliyeko wako,
    Huyo hakua wako ndio maana meachana ili anayestahili apate nafasi kwako.
     
  9. Sniper

    Sniper JF-Expert Member

    #9
    Jan 13, 2012
    Joined: Mar 8, 2008
    Messages: 1,940
    Likes Received: 10
    Trophy Points: 135
    Tafuta chombo kipya kikali zaidi yake, wanawake wapo kama milioni mia mbili hivi, ya nn kuumiza kichwa, upate presha, BP na sheli?
     
  10. Oman - Muscat.

    Oman - Muscat. Member

    #10
    Jan 13, 2012
    Joined: Jan 1, 2012
    Messages: 38
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Samahani kwa sikutambua gender yangu haiko, mimi ni mwanamke wa miaka 25 nimegombana nae akapata hasira kutaka tuachane, nimemuomba tumalize ugomvi kwa njia nyingine alikataa. Mimi ndio mkosaji kwakua nilingangania tuonane ile siku
     
  11. Oman - Muscat.

    Oman - Muscat. Member

    #11
    Jan 13, 2012
    Joined: Jan 1, 2012
    Messages: 38
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Thanks a lot, nitalifanyia kazi nimeona hata mimi napata tabu kuona Emails zake pictures , pia kwenye BB.
     
  12. mikatabafeki

    mikatabafeki JF-Expert Member

    #12
    Jan 13, 2012
    Joined: Dec 29, 2010
    Messages: 12,837
    Likes Received: 2,070
    Trophy Points: 280
    ulitaka muonane na akaktaa,akatoa sababu gani???/

    kwani kuna limit ya kuonana na mpenzi wako????

    alikua anatafuta chanzo cha kuachana tuhuyo,mulika mwizi.


     
  13. Perry

    Perry JF-Expert Member

    #13
    Jan 13, 2012
    Joined: Feb 24, 2011
    Messages: 9,918
    Likes Received: 613
    Trophy Points: 280
    afu mie utanitosa au?
     
  14. FaizaFoxy

    FaizaFoxy JF-Expert Member

    #14
    Jan 13, 2012
    Joined: Apr 13, 2011
    Messages: 55,534
    Likes Received: 17,026
    Trophy Points: 280
    Huyo mpenzi wako ni mkeo? mumeo?

    Kama si mkeo wala mumeo, ushukuru mungu kwa kukutoa katika dhambi za zinaa.
     
  15. Maundumula

    Maundumula JF-Expert Member

    #15
    Jan 13, 2012
    Joined: Nov 4, 2010
    Messages: 7,045
    Likes Received: 40
    Trophy Points: 145
    Rudiana nae kama huwezi kuishi bila yeye
     
  16. aikaruwa1983

    aikaruwa1983 JF-Expert Member

    #16
    Jan 13, 2012
    Joined: May 6, 2011
    Messages: 1,273
    Likes Received: 1,026
    Trophy Points: 280
    jamani dia mambo yetu umeyaweka hadharani huku!!!! basi nimekusamehe hata mm roho inaniuma ntapata nani wa kunipa mbadala wa kitumbua zaidi yako.........dia njoooo. mis yu so machi
     
  17. Tulizo

    Tulizo JF-Expert Member

    #17
    Jan 13, 2012
    Joined: Jun 13, 2011
    Messages: 842
    Likes Received: 19
    Trophy Points: 35
    Mara nyingi sababu za kuachana ndiyo faraja. Ila kama umeachwa au kupigwa chini kwa lugha nyingine basi faraja yako ni Imani yako kwa Mola ukiamini Mungu anakuepusha na mengi.
     
  18. Oman - Muscat.

    Oman - Muscat. Member

    #18
    Jan 13, 2012
    Joined: Jan 1, 2012
    Messages: 38
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Kwanza hapakua na limit za kuonana ila baadae tukaamua tuonane Mara 1 kwa wiki mana tunaishi umbali wa kilometres 80. Nina wiki 2 sijamuona, nikapata matatizo ya kifamilia nilimuhitaji sana ndio sabab nilingangania kua nae.
     
  19. Oman - Muscat.

    Oman - Muscat. Member

    #19
    Jan 13, 2012
    Joined: Jan 1, 2012
    Messages: 38
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
     
  20. Oman - Muscat.

    Oman - Muscat. Member

    #20
    Jan 13, 2012
    Joined: Jan 1, 2012
    Messages: 38
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Hahahaha! Thanks a lot, you made me smile.
     
Loading...