Naomba maelezo ya Kisimiri High School

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Mwanangu amechaguliwa kutoka Alliance Girls Mwanza kusoma HKL kidato cha tano shule ya Kisimiri high school iliyoko Meru mkoa wa Arusha.

Binafsi sikuwahi kujua kama kuna wilaya ya Meru ila najua kuna Arumeru. Tumejitahidi kugoogle kuiona haifunguki. Kwa anayeijua shule hii naomba maelezo yanayoihusu maana tumeambiwa ni maalum kwa watoto wa wafugaji wa kimaasai na iko kwenye manyata ya kimaasai. Sasa mkurya na mmaasai wapi na wapi.

Maramia
Mwanza.
 
Ni shule nzuri sana iliyoko chini ya mlima Meru.
Kama ni mara ya kwanza kwenda Arusha utafikia Arusha mjini then utafute magari yanayoenda Moshi au Kikatiti, utashukia njia ya kwenda Momela (Arusha National park) hapo utakuta magari ya kwenda Ngarinanyuki. Utawaambia unaenda Kisimiri bila shaka watakusaidia kufika uko. Mjitahidi kwenda na masweta mazito kwasababu kuna baridi kali sana.
Kwa upande wa ufaulu wako vizuri top 10 na 20 awabanduki ni mtoto wako tu kutia juhudi katika kusoma na comb yake ni rahisi sana atokosa div 1 .
 
Ngarenanyuki kuna wameru wengi zaidi ya wamasai na wanafanya shughuli zote za kilimo na ufugaji kwa pamoja.
 
Mwaka jana ilishika nafasi ya 8 kitaifa
290f209d00206e33572763b00c9efa6b.jpg
kiufupi nilatamani dogo wangu apangiwe hii shule lakini katupwa uko Mbeya vijijini.
 
Welcome

The History of Kisimiri Secondary School

Kisimiri Secondary school is the product of a collective initiative by the people of Kisimiri village. The local initiative later received a major impetus through a charitable donation from Prof. Emil Karafiat of Switzerland whose roots and earlier childhood life can be traced to this village located on the slopes of mount Meru in Ngarenanyuki ward, Meru district in Arusha Region-65 kilometres away from Arusha City.

Kisimiri Secondary School began on May 2002 with only forty students under Education coordinator Mr. A. Meena. At this humble beginning, the school teaching staff included the following Mr. Godlove Siara, Miss Eliakesia Mbise, Miss Neema and Nalaila Yona. Except for Mr. Godlove Siara, non had undergone a formal teaching training being only form six leavers.

It was only until 10th October 2002 that the government started allocating teachers to the school. Up to now the school has 32 government teachers.

Kisimiri secondary school is a fully registered government school and it is a Co-education school teaching science and arts subjects. It offers two combinations which are HKL (History, Kiswahili and English Language) and PCM (Physics, Chemistry and Advanced Mathematics) for form five and six. The school consists of both day and boarding scholars; all of them have one study cycle from morning up to afternoon. All A ‘level students are boarding Scholars.

The school has cherished under a good leadership of Mr. Emmanuel John Kisongo who is the third Headmaster of this school preceded by Mr. Martin Raphael Hari and Mr. Togolan Stanley Mbwambo.

You are all welcome to Kisimiri secondary school. The home of talents.
Website ya shule hii hapa Welcome

Website ya shule Kisimiri Secondary School | Education for Success
 
Nenda mpaka stand ya mabasi Arusha ukifika kuna bus za Urio au Neema za Mungu zinafika mpaka shule kabisa kama hawajabadili muda gari zinatoka mjini kuanzia sa 8 mchana hivyo muwahi siti na kwa Urio muulize maana nyingine hazipiti momela zinazungukia kikatiti kule...ni shule nzuri sana ipo mbali na mjini baridi la kutosha asisahau blanket
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ni special school kwa Advanced level though ina O-level pia...

ina combinations mbili tu yaan PCM na HKL.. ni co-Gender.. wanatusua sana tokea 2012,
 
Yaan Kisimiri nishule ya ukweli na ipo juu sana,ilisha kuwa ya 3 kitaifa nadhan kat ya mwaka juzi kama ckosei,ila ipo ndani kabisa au nje ya mji,mdg wangu ndo yupo 4 m4 mwaka huu na anafanya vzr sana darasan ucogope kabisa miundo mbinu ya shule imetuli.
 
Ni one of the best current government's school. Ni shule ya vipaji Maalum kwa Advance,japo haifanyi vema kwenye kidato cha NNE. Ina michepuo miwili pekee yaani PCM na HKL. Imekuwa ikiwa ya kwanza kitaifa kwa shule za serikali Mara kadhaa. Ipo pembeni kabisa Ya Mlima Meru karibu na Ngarenanguki. Ukienda Arusha tafuta Mabasi ya Urio na Neema za Mungu zitakufikisha mpaka shuleni.

Shule ni nzuri,sema kama mtoto ni wa bata Sana ambaye hajazoea kijijini,huko atapata tabu Sana. Vumbi limejaa,baridi ya kufa mtu kwa baadhi ya vipindi. Wazawa wa eneo hilo wengi ni Wameru na Wamasai. Kuna Prof mzungu anayefadhili Advance,jina lake Emil.
 
Hapana ashuki momela kuna Basi zinaitwa Urio bus service,atapandia hapo mjin znaondokaga saa nane zingine saa tisa.
 
Mwanangu amechaguliwa kutoka Alliance Girls Mwanza kusoma HKL kidato cha tano shule ya Kisimiri high school iliyoko Meru mkoa wa Arusha.

Binafsi sikuwahi kujua kama kuna wilaya ya Meru ila najua kuna Arumeru. Tumejitahidi kugoogle kuiona haifunguki. Kwa anayeijua shule hii naomba maelezo yanayoihusu maana tumeambiwa ni maalum kwa watoto wa wafugaji wa kimaasai na iko kwenye manyata ya kimaasai. Sasa mkurya na mmaasai wapi na wapi.

Maramia
Mwanza.
Upo sahihi,Hakuna Wilaya ya Meru. Meru ipo ndani ya wilaya ya Arumeru kulipo jimbo la Arumeru Mashariki kwa Mh. Nassari.

Sisi wote ni Watanzania,ukiona mwanao hafai kwenda shule hiyo kwa sababu yeye ni Mkurya na wenyeji wa eneo hilo ni Wamasai na Wameru basi sioni mantiki ya yeye kusoma Mwanza kwa Wasukuma. Angesoma huko Musoma kwa Wakurya wenzake.

In fact shule ni njema na itabutua hata zaidi ya hiyo Mwanza Alliance.
 
Wilaya ya Arumeru imebadilishwa na kuwa wilaya ya Meru.
4d54220d74d7d8027b22429c1f93ea3d.jpg
 
Inaonekana shule ni nzuri sana.

Kwa watu wa pwani hilo jina la shule lazima ulitamke herufi zote zisikike vizuri, vinginevyo inaweza kusikika ni "kashmir" au hata vinginevyo pia!!!
 
Ni shule nzuri sana iliyoko chini ya mlima Meru.
Kama ni mara ya kwanza kwenda Arusha utafikia Arusha mjini then utafute magari yanayoenda Moshi au Kikatiti, utashukia njia ya kwenda Momela (Arusha National park) hapo utakuta magari ya kwenda Ngarinanyuki. Utawaambia unaenda Kisimiri bila shaka watakusaidia kufika uko. Mjitahidi kwenda na masweta mazito kwasababu kuna baridi kali sana.
Kwa upande wa ufaulu wako vizuri top 10 na 20 awabanduki ni mtoto wako tu kutia juhudi katika kusoma na comb yake ni rahisi sana atokosa div 1 .
Asante sana kisu cha ngariba
 
Natumaini kwa haya machache yatakusaidia.
Lo! Maelezo yako yamenipa shibe ya ajabu. Hivi ninavyoandika namfanyia mhusika shopping ya vifaa vya shule.
Alikuwa tayari ameomba na amechaguliwa kusoma kozi ya banking certificate katika chuo cha Bank kuu ya Tanzania kilichopo Kapri-point Mwanza.
 
Back
Top Bottom