Naomba leo niseme japo kwa uchache

Waugwadu

JF-Expert Member
May 28, 2019
350
589
Unajua kisayansi kuna kitu kinaitwa atom najua unajua, mfano kuna Oxygen atom, hydrogen atom na zingine zote.

Zina sifa na tabia tofauti tofauti, hizi atom kwa upekee na sifa zake tofauti zinaweza kuungana miongoni mwao na kutoungana miongoni mwao pia.

Zikiungana tunapata kitu kinaitwa molecule, ambapo hizi molecule pia huja na tabia tofauti na zile tabia za kila atom zilizotumika kuungana. Sasa unajua oxygen atom akiungana na hydrogen atom tunapata maji, moja ya muungano mzuri zaidi, au sodium atom akiungana na chlorine atom tunapata hii chumvi ya mezani, pia oxygen atom mbili tunapata hewa hii ya oksijeni tunayovuta.

Lakini chlorine zikiungana tunapata hewa ambayo ni inapalia na hata inaweza kuua.

Kadhalika carbon na oxygen tunaweza pata hewa ya carbon monoxide inayoweza kuua pia.

Nataka kusema nini?

Unajua kwenye haya maisha watu ni kama atom, tuna sifa na tabia tofauti miongoni mwetu. Tukiungana miongoni mwetu tunatengeneza molecule tofauti tofauti.

Kuna baadhi ya ndoa ni kama maji, kila mtu uitumia ndoa hiyo kama kielelezo cha upendo, zingine kama chumvi yaani ukisikia au itajapwo ladha ya mapenzi na utamu wake watu hupata picha ya ndoa hiyo.

Kuna baadhi ya urafiki ni kama oxygen yaani watu wakizungumzia umuhimu wa kuwa na rafiki, hutumia marafiki hao kama kielelezo cha upendo na mshikamano.

Vivyo hivyo kuna baadhi ya ujamaa ni kama chlorine au carbon monoxide kila mtu hukataa mazoea na watu huku akitolea mfano huo ujamaa uliokuwa wa kinafiki.

Matatizo mengi kwenye jamii yangeweza tatulika kama tungezingatia miunganiko yetu, kuna ndoa wanandoa wanaona kabisa sisi tukiishi pamoja ni hewa sumu lakini bado wanafunika kombe.

Kuna washikaji unaona kabisa hawa sio ni sumu, wanatembea na wake za watu, bado unaishi nao mara paah wanamtaka mkeo.

# Jifunze kuwa mdadisi.
 
Halafu kuna muunganiko wa maji na mafuta🤣🤣

Mpaka yesu anarudi .....atavikuta vilevile ndio baadhi ya uchumba wa sasa


Ila unapoint usikilizwe

Wewe unaandika habari za mixtures, mwenzako kaandika habari za chemical reactions....
 
Wewe unaandika habari za mixtures, mwenzako kaandika habari za chemical reactions....
Sema kasema vizuri sana, unajua uzuri wa mixture kila kilicho ungana kinabaki na tabia zake za awali, sasa kwenye huu uchumba wa karne hii pia unakuta nyingi mixture.

Mfano mwanamke mlevi, anapenda matumizi makubwa na mwanaume muumini na anapenda maisha rahisi au hana maisha makubwa na kinyume chake, hawa watu pia ni changamoto na sio afya kuwa na hii mixture kwenye jamii kama hawataamua ku-compromise baadhi ya mambo.
 
hii ya kitoto ndio advance physics
utakuwa wa hkl, haya jipange kichama uchukue udiwani
Nkmesema amenikumbusha physics wakati nasoma advance, nimesoma PCB advance. Sasa aliyesema hii advanced physics nani?

Kuna watu wanapenda living za kijinga. We did study this in form five, advance.
 
Back
Top Bottom