Kuna mtu hapo juu ka comment kuwa ukiona hupigiwi baada ya kuchukua namba basi elewa huna thamani/matumizi kwao.
Binadamu tumeumbwa na ubinafsi wa kupenda kupata manufaa katika kila jambo.
Mlipokuwa shule mlikuwa marafiki sababu mlikuwa eneo moja na mishe zenu ni moja (kusoma).
Kitendo cha kupotezana kila mtu anapata watu wengine wanaendana kimishe na kimaisha.
Kosa kubwa ambalo binadamu tunalo ni kupenda kutathmini kwa muonekano.
Ikitokea umekutana na mtu uliepotazana kwa muda jambo la kwanza bila hata kudhamiria ni ku assess maisha yake kupitia muonekano.
Ukiona mtu anaonekana ana hali duni automatically unajijengea hali ya kuwa atakuwa mzigo kwako kupitia vizinga. Akionekana mambo safi basi unajipa faraja kuwa atakupa michongo. Hivyo kutaka kuendeleza mawasiliano. Ila kumbuka huko kuhukumu kimuonekano hata huyo mwenzio keshaufanya hivyo kutokana na hali yako ndipo kutaamua jinsi gani na yeye atarudisha mawasiliano kwako.
Ukiona umeliwa bati au unajibiwa kwa nyodo elewa ushaonekana miyeyushe.
Chukulia ukienda sehemu kutafuta kazi ukakutana na rafiki yako wa zamani mliosoma wote. Hali utakayokutana nayo kwake hapo kazini itaamua kwa kiasi kikubwa jinsi gani mawasiliano yenu yatakavyokuwa.
Ikiwa umemkuta kama Boss hapo kazini basi lazima wewe ndie utakaekuwa wakumtafuta na kukumbushia uswahiba wenu hii yote kwa matumaini kuwa atakuwa msaada kwako kupata kazi.
Na uwezekano wa yeye kukujibu kwa mapozi ni mkubwa.
Jifunze kujithamini mwenyewe katika maisha. Usiruhusu hali ya mwingine iamue jinsi gani utam treat huyo mtu.
Ukituma msg mbili bila majibu yenye bashasha basi elewa kuwa ushafanyiwa assessment kuwa huna manufaa. Futa namba endelea kuishi maisha yako.