Naomba kuongea na wewe kwa maandishi (as a serrious issue)

Naomba kuongea na wewe kwa maandishi (as a serrious issue)

love more than100

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2014
Posts
2,061
Reaction score
715
JE, FEDHA ZAKO ZA BANK ZIPO SALAMA?! NAOMBA KUZUNGUMZA NAWE...

Jamani imenitokea mimi siku ya LEO na hivyo iwe fundisho, angalizo na umakini kwa wengine. Account zetu za Bank hazipo salama hata kidogo. majuzi nikiwa nimepozi na ndugu zangu huku tukiwa tunapata kinywaji, na Wenzetu maeneo mengine ya nchi wakisheherekea sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, niliamua kwenda Bank kuchukua vijisenti kidogo. Nikiwa ndani ya chumba cha ATM pale sheli Total Mlimani City nilichomeka kadi yangu na kutaka kutoa fedha kwenye account yangu ya NBC.

ATM machine iliashiria ya kwamba sikuwa na kiwango cha fedha cha kutosha kuweza kukamilisha muamala unaozidi 100,000/-. Nilipaswa kuchukua kiwango kuanzia 50,000/- kwenda chini! Nilishtuka kwakweli. Account yangu ilikuwa na Uwezo wa kunipa muamala mkubwa zaidi. Yaani hata zaidi ya 400,000/- ambayo ni Maximum kwa ATM.

Niliamua kwenda Mlimani City kabisa. Yale yale yalijirudia. Nikaamua kutoa 50,000/- huku nikijifariji ni tatizo la kimtandao maana nilijaribu ATM za CRDB pale nje zikaonesha zipo out of service! Lakini wakati natoa hizo pesa niliomba statement ambayo ilionesha kiwango Kikubwa cha pesa hakipo! Nikajumuika na jamaa zangu huku nikiwahoji kwa kile kilichonikuta. Tukapeana moyo leo niende Bank ya NBC kuhakikisha.

Sikupata usingizi. Asubuhi ikawaidia. Nikaingia tena kwenye ATM kuthibitisha na kujiridhisha kama kweli ulikuwa ni mtandao. Nikakuta salio langu limepungua zaidi.

Nasukuma milango mizito ya pale NBC Mlimani City. Nikaomba statement manually. Zikawa zimepungua tena. Yani mwendo wa kutoka kwenye ATM hadi ndani pesa zilitolewa /ibwa. Dada au customer care aliyekuwa pale akaniambia mbona inaonekana nime swap card Nakumat Supermarket?! Nilishtuka maana sikuwahi ku swap card popote pale toka nizaliwe na hata sijui hiyo kuswap ikoje!

Lakini alipoangalia vizuri akagundua card imekuwa swaped kwenye Nakumat ya Nairobi. Nayeye akastuka. Akaniambia kaka subiri kuna tatatizo. Nikamuomba Bank statement ya miezi 2. Yaani December-2014 na January 2015. Sikuamini nilichokutana nacho. Account yangu nimekuta imeibiwa zaidi ya Tsh Million 6.

Transactions zote zimefanyika Nairobi, Kenya. Wizi huo umeanza kufanyika toka-December 20, 2014. Na sehemu kubwa ni kwenye Nakumat Supermarket. Walichoniambia NBC nijaze claim form na kuandika barua. Nimefanya hivyo. Nasubiri majibu yao. Hata hivyo wakati najaza form nilikutana na watu kadhaa wakiwa nao wameibiwa kwa mfumo huu huu.

Hivyo ndugu zangu, kwa wenye account za NBC wakazikague. Waulize Bank statement. Bank hii siyo salama tena. Nilipata msg ya Wizi huu wa Fedha last year December nikapuuzia. Na bank husika ilitutumia msg wateja wake kwamba habari za Wizi wa mtandao zilikuwa za uzushi tu! Leo nimeamini haukuwa uzushi. Pesa zinaibwa. Angalieni account zenu zote na isiwe NBC tu.

Nawatakia siku njema. Hayo ndiyo yaliyonikuta leo. Sina hamu!
 
Akuna benki wanajitahd kwa huduma nzur kama nbc
 
NBC ni janga la mabenk kwa sasa
 
Akuna benki wanajitahd kwa huduma nzur kama nbc

Mmh Tumboo hapana NBC ni full majanga si kwa wateja tuu bali hata kwa nchi kwa ujumla CPU yake iko South Africa....! Kuna mengi ambayo hayasemwi kuhusu NBC
 
Last edited by a moderator:
Tunashukuru sana kwa kushare na sisi, tumejifunza mkuu, japo kuwa hujatuelewesha vizuri? kwamba ilikuwaje hadi accaunt yako ikafika kenya

maana siku hizi wakenya huwanga wanatuma email zingia kwenye spam, zenye lengo la kukuimbia
 
Hao matapeli wanakuwa wametengeneza kadi na details za wateja walizozipata.

Muhimu ni mtejabwa benki hiyo kutoa taarifa kadi imepotea ili wai cancel na upate ingine.
 
Huu utapeli upo duniani kote ila kwa nchi nyingi zilizoendelea wanazidi kuweka security kuzuia utapeli.
 
pole kwa hilo kama ni kweli ila wenzio tupo CRDB hizo bank za serikali zina madeni kibao kiasi kwamba hata wanaodai mafao yao ya mfuko wa taifa ni shida tupu full kuvurugana mie nakushauri komaa hela yako irudi hao wameichakachua amini hili nisemalo
 
sasa kuna haja yakurudi kwenye vibubu, maana bank full majanga, mara ATM haifanyi kazi, unaweza kuhamisha pesa kwa sim muamala ukachukua zaidi ya siku tatu na ikiwezekana haukamiliki kabisa, wajanja nao ndio washaingia kutuibia maskini sie khaaa!
 
Pole sana lkn mkuu komaa nao usikubali kupoteza pesa yote hiyo inawezekana kuna kitu zaidi ya ulichoambiwa.Kikawaida kama transaction imefanyika nchi tofauti lazima bank hukutumia taarifa siku hiyo hiyo kama sikosei
 
Hili limeseji la whatsup limeshazunguka zaidi ya miezi miwili. Unajisikiaje kuposti stori na kujifanya imekutokea wewe? Account yako haijawahi kuwa na salio la milioni 6 wewe. Unatuchosha
 
Back
Top Bottom