Naomba kujuzwa tofauti ya MC na RAPPER

Naomba kujuzwa tofauti ya MC na RAPPER

mzee wa kasumba

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
1,440
Reaction score
2,966
Kwakua sifahamu sana mambo ya HIPHOP huenda nikawa nimekosea kuuliza swali (Mtanisamehe)

Naomba kujuzwa mambo kadhaa kuhusiana na hiphop.

1. Tofauti ya MC na RAPPER
2. Wanasema hiphop ina nguzo 5, ni zipi?
3. Ila nasikia kuna kitu wanaita PUNCH LINE ni nini?

Binafsi katika michano namkubali sana wasanii hawa.

1. Youngkiller
2. Roma mkatoliki
3. Bando
4. Rapcha
5. Stamina
6. Fid q
7. Boshoo
8. Professor J
9. Maarifa
10. Chuma mbeya boi

Na wengine wengi.

Ila naomba kujuzwa juu ya hayo hapo juu walau kwa uchache.
 
Unapoongelea elements za MC unatakiwa uelewe kwamba ni lazima awe na uwezo wa kuwakilisha jamii

MC anatakiwa awe na uwezo wa kuwakilisha, kuwasilisha na kufikisha taarifa kwa jamii. Na pia anaweza akawa na vinasaba vya upande wa biashara

Jambo ambalo wengi wanashindwa kuelewa ni kua MC ni rapper pia lakini utofauti kati ya MC na rapper ni kwamba rapper mara nyingi huongea kuhusu personal issues.

Mfano mzuri kama madee "nani kamwaga pombe yangu" au young killer "sina swaga" nk. Unaona kabisa kua hivyo ni vitu ambavyo vinamuhusu yeye

MC sasa tukichukulia mfano wa mtu kama Professa j na mtu kama fid q unaweza ukaaona ni watu wenye uwezo wa kuelezea mambo ya kukufundisha, haimuhusu yeye tu bali jamii kiujumla

MC huongea kama mtu wa tatu anapo delivery ujumbe wake. Mfano wa mzuri ni hii verse ya fid Q "ongea maisha ya kuunga unga hii shuhuli mi naiweza, hapa utaambulia ushauri tu ukihitaji msaada wa kifedha.../"
 
Koyo mc
Bando mc

Roma na stamina wao ni majigambo


Young killer rapper

Over🤔🤔
 
Kwakua sifahamu sana mambo ya HIPHOP huenda nikawa nimekosea kuuliza swali (Mtanisamehe)

Naomba kujuzwa mambo kadhaa kuhusiana na hiphop.

1. Tofauti ya MC na RAPPER
2. Wanasema hiphop ina nguzo 5, ni zipi?
3. Ila nasikia kuna kitu wanaita PUNCH LINE ni nini?

Binafsi katika michano namkubali sana wasanii hawa.

1. Youngkiller
2. Roma mkatoliki
3. Bando
4. Rapcha
5. Stamina
6. Fid q
7. Boshoo
8. Professor J
9. Maarifa
10. Chuma mbeya boi

Na wengine wengi.

Ila naomba kujuzwa juu ya hayo hapo juu walau kwa uchache.
Mc ni Microphone controller.

Zembwela, Maulid Kitenge, Profesa Jay and likes.
 
Mc
b Boy
Dj
Knowledge
Graffiti nazifahamu nguzo hizo....Kama nimekosea watanisahihisha wajumbe
 
Back
Top Bottom