Naomba kujuzwa tofauti kati ya Mtu na Binadamu

Mtu ni kiumbe yeyote mwenye ubin wa Adam na ambaye ana utu. Utu ni kuwajali na kuwathamini wengine.

Binaadam ni kiumbe mwenye ubin wa Adam
 
Hakika Haya maneno yananisumbua kuyaelezea kwa tafsiri sahihi.

Naishia kusema tu mtu ni binadamu na binadamu ni Mtu.

Karibuni wataharamu wa lugha. Munisaidie Kunipa tofauti Ya haya Maneno.

Asante
Habari waheshimiwa!!

Kwa mukhtadha wa lugaha ni kuwa, Binadamu ni mtu ila mtu siyo lazima awe Binadamu. Sababu ni kama ifuatavyo:-

Neno Binadamu ni muunganiko wa maneno mawili ya kiarabu yaani Bin (hii inawakilisha uzao wa kiume) na Adam/Adamu, huyu kiimani ndiye binadamu wa kwanza kuumbwa. Sasa waarabu wakiita Bin Adamu humaanisha mtoto wa kiume wa Adam (uzao wa kike huitwa "Binti" japo haijazoeleka)

Lakini sisi waswahili kutokana na lahaja zetu tumejikuja tukiunganisha maneno hayo mawili na kuwa neno moja yaani Binadamu. Hivyo basi ukisikia neno Binadamu hasa huwa inalengwa mtu mwanaume. ni sawa na tulivyounganisha "Mussa Hassan" na kuwa "Msasani".
 
mtu-person
Binadamu-Human Being

watu wote ni Binadamu ila sio kila binadamu ni mtu...
Mtu ni binadam mwenye utu,A human being with personality.

Mtoto mchanga ni binadam maana anapumua ana miguu miwili vidole kumi macho mawili pua moja lakini sio Mtu maana bado hajadevelop personality(utu)
 
Oouh...
 
Hakika Haya maneno yananisumbua kuyaelezea kwa tafsiri sahihi.

Naishia kusema tu mtu ni binadamu na binadamu ni Mtu.

Karibuni wataharamu wa lugha. Munisaidie Kunipa tofauti Ya haya Maneno.

Asante
Nami napenda kuchangia kwa haya maneno haya mawili ;mtu na binadamu

Kwa mtazamo wangu neno binadamu limetafsiriwa kwa mtazamo wa kidini zaidi - watu wote wametokana na Adamu, hiyo imeleta maana ya Bin - adamu au wana - Adamu. Haina tofauti na maana ya mtu. Mtu ni tafsiri ya kijumla sahihi ikiwa na maana ya binadamu lakini hii tafsiri ni ya kawaida wala haina msingi wa kidini

Walaiotafsiri "man" kuwa binadamu walikuwa na mlengo wa kidini kutofautisha na hilo la mtu, na kuongeza utajiri wa Kiswahili.

Kuna maneno kama "utu" au "ubinadamu" yote yanaweza kuwa na maana moja. Kiswahili hatuna maneno mengi kama Kiingereza - human, person, etc.,
 
Back
Top Bottom