Naomba kujuzwa tofauti kati ya Mtu na Binadamu

engine search

Senior Member
Jan 4, 2020
174
88
Hakika Haya maneno yananisumbua kuyaelezea kwa tafsiri sahihi.

Naishia kusema tu mtu ni binadamu na binadamu ni Mtu.

Karibuni wataharamu wa lugha. Munisaidie Kunipa tofauti Ya haya Maneno.

Asante
 
Binadamu ni wale wenye asili (chimbuko) au binadamu wa kwanza,watu ni wale waliopo kwa sasa,waliozaliwa na binadamu,Man vs People
 
Yote ni sawa, ila matumizi ndio tofauti.

Bin-Adamu/Mwana-Adamu, inatumika zaidi kama unataka kusisitiza asili, sayansi (biolojia), uumbaji au kutofautisha na viumbe/wanyama wengine.

Mtu inatatumika kwenye muktadha wa kawaida wa kijamii (social aspect ya binadamu).

My few cents! Mimi sio mtaalamu wa lugha.
 
Hakika Haya maneno yananisumbua kuyaelezea kwa tafsiri sahihi.

Naishia kusema tu mtu ni binadamu na binadamu ni Mtu.

Karibuni wataharamu wa lugha. Munisaidie Kunipa tofauti Ya haya Maneno.

Asante


Japo watu wametoa ufafanuzi ngoja na mimi nitoe kidogo.

Watu ni jamii yote ya viumbe wa makundi fulani wa wanyama wanaihusiana kigenetic na wanaoweza kuzaliana wakikutana kimapenzi, wataalamu wa (mambo ya kale) waliweza kuweka makundi hayo ya watu na kuyapa majina kulingana na maeneo walipotoka, mfano kuna Homohabilis, Homo erectus, zinjanthropus nk, hadi leo akatokea Homosapiens ambao ndio sisi.

Hapo sasa utaona watu wamepitia hatua ndefu mbalimbali mbali hadi hii leo.

Binadamu ni nani???--- ubinadamu ni sifa anayokuwa nayo mtu, kifupi mtu akistaarabika huyo ataitwa binadamu, kifupi ni kwamba mtu wa kwanza kuleta ustaarabu duniani ni Adam (Nabii Adam as), huyu aliletwa/alitumwa na Mungu kwa watu wake kuja kuwafundisha maadili mema, yeye alikuwa mtu wa KWANZA kuwa mstaarabu (civilized) bali hakuwa mtu wa kwanza kuumbwa kama watu wengi wanavyoamini kimakosa.

Kwakuwa Adamu ndiye mtu wa kwanza katika hili kundi letu la Homosapiens kuwa na maadili na ustaarabu ndipo sisi watu waleo tukiwa na maadili mema na ustaarabu pia tunaitwa Wanaadamu (wana wa Adamu) au watoto wa adamu tunaitwa hivyo kwa heshima ya huyo Adamu tu.

Hivyo ubinadamu wa mtu ni sifa njema za kimaadili alizokuwanazo mtu yeyote na ndipo mtu huyo huitwa Binadamu.
 
Naona kama muktadha wa neno binadamu umekaa kiuelezeo wa asili ya binadamu kutoka ktk imani haswa za dini.. Yani binadamu ni sawa na utambulisho kuwa kutoka kwa Adam!.. hivyo neno binadamu limebeba utambulisho wa asili ya binadamu toka ktk imani za dini hasa uislam(kiarabu) kwani neno lenyewe asili yake ni uarabuni.

Watu au Mtu.. binafsi naona ni utambulisho wa kiumbe mtu au watu bila kuangalia itikadi yake au itikadi zao,hii imesimama zaidi kama utambulisho usio na utofauti wa kiimani au itikadi n.k.. hii inabeba sifa zote za utu.. yani kiumbe kinachojitambua kushinda viumbe wengine.. na ndio maana hutumika kuelezea matendo fulani ambayo ni ktk upande wa kujitambua mfano fulani hana utu!.. kukosa utu ni sawa na kufananishwa na mnyama asie na akili Kama mtu!!.

Pia hata katika binadamu tunapata msamiati "ubinadamu" hii inaonyesha utofauti wa sifa ya kuwa binadamu tofauti na viumbe wengine ni kuwa na ubinadamu yani utendaji wa kutumia akili na kutoa uamuzi au kutenda kwa haki.

Na ndio maana ukikosa sifa ya ubinadamu basi unavikwa unyama!.. hivyo umeukosa utendaji wa sifa ya ubinadamu kama kutumia akili,kuwa mpole, kutenda wema n.k

Tofauti ya hayo maneno haswa naona umekaa ki imani kwamba binadamu inaeleza pia asili ya binadamu na mtu au watu haichangamani na kokote..

Inachanganya..😇😇
 
Hamna tofauti, ni utambulisho tofauti wenye maana moja.
 
Hakika Haya maneno yananisumbua kuyaelezea kwa tafsiri sahihi.

Naishia kusema tu mtu ni binadamu na binadamu ni Mtu.

Karibuni wataharamu wa lugha. Munisaidie Kunipa tofauti Ya haya Maneno.

Asante
Uko sahihi!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom