Naomba kujuzwa namna ya kutengeneza mbege

Naomba kujuzwa namna ya kutengeneza mbege

Ndnda kiwandani

20250411_214614.jpg
 
Nilionaga home wakitengeza hii kitu nyakati za sikukuu na sherehe. Sikumbuki vizuri sana hua walikua Wanachukua ndizi mbivu zinapikwa kwa siku nzima siku ya pili ndio waitisha najua wanatumia ulezi ila sijui wanprocess vipi hapo wajuzi waje watupe hints
 
Mwana Jf mmoja anielekeze namna ya kutengeneza mbege kama Nina ndizi na ulezi tayari.
Chemsha ndizi zako mpaka zibadilike rangi na kuwa nyekundu, ziepue na weka kwenye vyombo kama ndoo, kwa siku tatu au nne,baada ya siku nne unakuja kuziweka ndizi zako kwenye drums kubwa zote kwa pamoja,halafu unaongeza maji kiasi katika zile ndizi jioni,ambapo kesho yake jioni ndiyo utazikamua upate wine ya ndizi kabla ya mbege,Wakati unakamua ndizi zako ndio wakati unapika ulezi wako, ulezi ukiiva unachanganya sasa na ile wine ya mbege halafu unachanganya unapata mbege ambayo siyo kali,ikikaa tena masaa 12 ndiyo inakuwa mbege ukinywa unalewa kama kawaida.
 
Back
Top Bottom