Naomba kujuzwa kuhusu biashara hii yenye utajiri

Dkt Guston

Senior Member
Feb 28, 2022
105
110
Habari wana JamiiForums

Naomba kujuzwa na kupewa muongozo kuhusu biashara hii ya kusafirisha bidhaa kutoka Tanzania kwenda Marekani, Canada, England na South Africa

Naomba kupewa muongozo jinsi ya kusafirisha bidhaa kutoka Tanzania kwenda nchi hizi bidhaa zitachukua muda gani hadi kuwafikia wateja wangu, usafiri gani ni nafuu na hauna gharama kubwa na jinsi ya jinsi ya kusafirisha bidhaa zangu.

Kwa anayefahamu naomba anijulishe na anipatie muongozo sahihi

Natumaini mtanisaidia wakubwa
 
Kwanini mshangae kupeleka phone accessories na sendo marekan?

Kuna phone accessories za simu kama makava yametengenezwa kiasili ukipeleka huko yatauzika tu

Kuna sendo za kimasai je huko huwezi uza?
Hata mimi nashangaa sendo za kimasai, bangili za shanga, neckles za kitamaduni, vinyago na bidhaa nyingi zitakazo kuwa adimu ulaya Ila watu hawajui MTU umewaza nini ila ni ku hate tu
 
Dah baadhi ya wabongo wengi tunakatishana tamaa sijui kwa nn, acha niweke dhana roho mbaya ndio inayotutesa.
Acha tu kuna vitu kama viatu vya kimasai, Ulaya havipo mtu ukitengeneza online store yako vizuri ukafanya promotion kupitia Facebook ads, tiktok ads, Instagram ads kuwafikia wateja wa nje mbona unapata wateja ila watu hawajui MTU umewaza nini ila chuki tu
 
Habari wana jamii forums

Naomba kujuzwa na kupewa muongozo kuhusu biashara hii ya kusafilisha bidhaa kutoka Tanzania kwenda marekani,Canada,England na south Africa

Naomba kupewa muongozo jinsi ya kusafilisha bidhaa kutoka Tanzania kwenda nchi hizi bidhaa zitachukua mda gani hadi kuwafikia wateja wangu,usafili gani ni nafuu na hauna gharama kubwa na jinsi ya jinsi ya kusafilisha bidhaa zangu

Kwa anayefahamu naomba anijulishe na anipatie muongozo sahihi namba zangu +255759952554

Natumaini mtanisaidie wakubwa
Hiyo namba ya simu mbona haraka sana, unaweza ukawa unamsaidia wazo mtu ukimpigia tu wewe ndo unaenda kutapeliwa kuweni makini
 
Back
Top Bottom