Biashara ipi kati ya hizi mbili inalipa zaidi kati ya Fusso Tippa Vs Coaster ya Kubebea abiria

Brown Mduma

Senior Member
Sep 29, 2020
180
283
Wakuu nataka kufanya biashara mbili kati ya hizi niwe na fusso tipa la kubebea mchanga, kokoto, vifusi na n.k au niwe na coaster kwa ajili ya kubebea abiria kutoka wilaya moja kwenda nyingine au kutoa mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine.

Naomba wazoefu hizo biashara moja wapo mnipe muongozo mzuri ili nione kipi kitanifaa kati hizo biashara mbili.

Niko hapa nasubiria muongozo wenu wakuu
 
Biashara zote ni nzuri kama wewe ndio utakuwa msimamizi mkuu, upo kushoto unapokea fedha na kusimamia hizo gari , iwe. coaster ama Fuso tipper.

Kama huna muda wa kusimamia na kufuatilia Kwa ukaribu Usijaribu kumpa mtu akuletee hesabu.

Kuliko kumkabidhi mtu ni Bora ukaweka Hela yako Bank na kuhifadhi Mazao ama kujenga nyumba ya kupangisha ya room kumi upate hata laki Tano Kwa mwezi.

Biashara za magari ukimkabidhi mtu. Hupati pesa na gari zinakufaa bila kukuleteya hata Milioni mbili.

Kama wewe ni dereva utaweza , ila vinginevyo subiria maumivu
 
Mbona unawadanganya watu wewe umewahi kuifanya hiyo biashara?
 
Zote Pasua kichwa Tipper unaweka 100 huko then kwa mwezi 6M unaitafuta kwa Tochi Coaster unaweka 60 had 70 Kwa siku unaingiza laki moja … plus Usumbufu madereva bado maintainance na gharama za spare … Ushauri tu kama Iyo hela ndo Main Base yako , Utaumwa vidonda vya Tumbo kila kukicha
 
Mbona unawadanganya watu wewe umewahi kuifanya hiyo biashara?
Nimekulia kwenye hiyo industry , nimeona na kuexoerience mengi sana,
Kujifunza ni rahisi wewe nenda kalipe millioni 90 then umkabidhi dereva au toa 62millioni ununue Coaster umpw dereva na kinda mlevi wakuletee fedha nyumbani, nina uhakika ndani ya miezi mitatu utatupa mrejesho wenye akili.
 
Waajiriwa wengi wanafeli kwenye biashara sababu hawana mda biashara sahihi ni real estate yaani biashara za ardhi na cement aka biashara za kuchukua Kodi.
Labda tu kama una mwenza wako SI muajiriwa yeye akasimamie hapo mtakwenda.
Huna mda tunza pesa zako bank wakati wa likizo kanunue nyumba,viwanja,mashamba,kujenga hapa ndo utaiona Hela Yako hata ukija kustaafu utolia njaa utaishi hata miaka 30 baada ya kustaafu.
Uzeeni unataka sana pesa asikuambie mtu.
Mke na watoto siku hizi ni probability nao wanaweza wakakutelekeza hapo unakufa njaa.
 
Nimekulia kwenye hiyo industry , nimeona na kuexoerience mengi sana,
Kujifunza ni rahisi wewe nenda kalipe millioni 90 then umkabidhi dereva au toa 62millioni ununue Coaster umpw dereva na kinda mlevi wakuletee fedha nyumbani, nina uhakika ndani ya miezi mitatu utatupa mrejesho wenye akili.
Ingekuwa hivyo kama unavyotaka kupotosha watu kusingekuwa na watu waliofanikiwa kwenye biashara hii...hapo inaonyesha haujakulia kwenye biashara ya magari,nina ndugu zangu wengi mno waliofanikiwa kwenye hiyo biashara,Tatizo la humu kila mtu ni mjuaji
 
In
Ingekuwa hivyo kama unavyotaka kupotosha watu kusingekuwa na watu waliofanikiwa kwenye biashara hii...hapo inaonyesha haujakulia kwenye biashara ya magari,nina ndugu zangu wengi mno waliofanikiwa kwenye hiyo biasharaea
Kumbe umesikia Kwa Ndugu zako , Subiri ukiokota Hela. Na wewe ujaribu hiyo biashara.
Unajuwa Bei ya Coaster
Bei ya Fuso?
Halafu unakuja kumpa mjinga Moja anaanza kulewa na kufuata Malaya wa Kutumia nao Hela za Gari zako?
Kama Mtu hana muda wa kusimamia mwenyewe achana nae , fanya issue zingine, Bora ujikite kwenye Ardhi , nunua ekari zako mbili maeneo ya Kibaha , subiri mwaka Moja au miwili unaanza kukata viwanja, ekari Moja , then unasuburi Tena unauzw. Kidogo kidogo , utapata fedha nzuri ,
 
Kwa Tanzania yetu unapopata wazo la kufanya biashara jiulize una muda wa kuisimamia? Kama huwezi kuisimamia je una mtu sahihi wa kusimamia. Uaminifu kwenye jamii yetu umenasibishwa na ujinga. Hata mtu akianza na nia safi atapata wakumshawishi afanye wizi. Tuna maneno mengi ya kuhalalisha wizi.

Nakumbuka rafiki yangu alilipa kodi ya duka milioni 12 kwa mwaka na hakufunguwa hata siku moja. Sababu alisema aliyepanga kumuweka dukani alipata safari kwenda masomoni na akaona bora kupoteza hiyo kuliko kuweka ambaye hamuamini na kuibiwa na mtu wa ndani.
 
Ebhana nenda na fuso la mchanga Hilo

Ukiwa serious na hiyo kazi inakulipa vibaya sana KULIKO gari za abiria

Tipa ya mchanga inaweza ikagonga miaka 10 ila DALADALA ikitoboa miaka minne Kila siku unagombana na madereva

Tipa ya mchanga unaweza ukakaa wiki kijiweni ila kazi zikifululiza tu unalaza Hela nzuri kwa wiki

Imagine Kila trip ushatoa Kila kitu umelaza 100k

Kwa siku ukipiga trip 5 unalaza 500k bila presha na chombo haitembei sana !

Katika hizo ideas zako naenda Moja kwa Moja kwenye tipa mzeee wangu.!

Nafanya kazi area hiyo naona mambo yalivyo !
 
Biashara zote ni nzuri kama wewe ndio utakuwa msimamizi mkuu, upo kushoto unapokea fedha na kusimamia hizo gari , iwe. coaster ama Fuso tipper.

Kama huna muda wa kusimamia na kufuatilia Kwa ukaribu Usijaribu kumpa mtu akuletee hesabu.

Kuliko kumkabidhi mtu ni Bora ukaweka Hela yako Bank na kuhifadhi Mazao ama kujenga nyumba ya kupangisha ya room kumi upate hata laki Tano Kwa mwezi.

Biashara za magari ukimkabidhi mtu. Hupati pesa na gari zinakufaa bila kukuleteya hata Milioni mbili.

Kama wewe ni dereva utaweza , ila vinginevyo subiria maumivu
Mkuu...technology bado hazisaidii?

Kama matumizi ya Car track system?fuel sensor?...ambapo utapata report aina nyingi (hapa unapata nafasi ya kufaham mengi yanayojiri wakati chombo inasafiri Kana Kwamba nawe ulisafiri)
 
Ukitaka kufa mapema na uongee peke yako barabarani miliki chombo cha usafiri bila usimamizi mzuri

Dereva anaiba,fundi anaiba,konda anaiba, trafiki wanataka pesa

Mi niliwahi lala na viatu siku .....kwanza ukiona simu ya dereva....mapigo yanabadilika kabisa

Mi najiulizaga wanaomiliki mabasi na malori hivi cjui hawana mioyo?
 
Mkuu hizi coster tunazoona zinapiga kazi mjini wamiliki wake hawanufaiki nazo? na mnapozungumzia usimamizi mzuri, mnamaanisha mmiliki ndie akawe kondakta au dereva?
 
In

Kumbe umesikia Kwa Ndugu zako , Subiri ukiokota Hela. Na wewe ujaribu hiyo biashara.
Unajuwa Bei ya Coaster
Bei ya Fuso?
Halafu unakuja kumpa mjinga Moja anaanza kulewa na kufuata Malaya wa Kutumia nao Hela za Gari zako?
Kama Mtu hana muda wa kusimamia mwenyewe achana nae , fanya issue zingine, Bora ujikite kwenye Ardhi , nunua ekari zako mbili maeneo ya Kibaha , subiri mwaka Moja au miwili unaanza kukata viwanja, ekari Moja , then unasuburi Tena unauzw. Kidogo kidogo , utapata fedha nzuri ,
Mkuu, hizi daladala tunazoona zinapiga kazi mjini, je, wahusika hawanufaki nazo? na je, mnapozungumzia hoja ya usimamizi mzuri mnamaanisha mmiliki ndio uwe kondakta au dereva? tafadhali mtupatie uzoefu juu ya hili maana sekta ya daladala hata mm naipigia hesabu kwa sasa.
 
Back
Top Bottom