Naomba kujua utaratibu wa kufunga ndoa ya Kiserikali

Midazolam

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
806
1,337
Naomba kujua utaratibu wa kufunga ndoa ya Kiserikali

Nahitaji kuwa na nini na nini maana mwanamke ninaye. Lengo kuu ni kutaka kufanya mambo mengine nikiwa na huyu mwanamke maana Kuna vitu nashindwa kumkamilishia mpaka awe ndani ya ndoa ya serikali.

Na njia gani naweza kutumia Ili nifanikishe Ili jambo.

Ni hayo tu watanzania wenzangu.
 
Utaratibu unaanzia kwa AFISA Mtendaji wa Kata ya Wilaya unayoishi, Kwa ajili ya kupata barua ya utambulisho wa makazi yako.

Halafu unaipeleka hiyo barua kwa Mkuu wa wilaya kwa ajili ya kuandikisha ndoa, Baada ya hapo Tangazo litabandikwa hapo wilayani kwenye ubao wa matangazo, Utalipia 40,000/=Tsh.

Ndoa itafugwa siku ya Jumanne au Ijumaa Asubuhi (Kulingana na Ratiba ya Ofisi). Atakayefungisha Ni Mkuu wa wilaya au katibu tawala. Ufike na mashahidi wawili kwa kila mmoja wenu Mkiwa mmeva mavazi ya heshima. Baada ya hapo mtapokea Vyeti vya ndoa ambayo inatambulika kisheria.

My take. Nibora Ndoa ya Bomani kuliko kuishi kienyeji hasa Kama una Mali na watoto ili kuwalinda kisheria Pindi ikitokea umewahi kutangulia mbele ya haki.
Nawasilisha.

images (32).jpeg
 
Naomba kujua utaratibu wa kufunga ndoa ya Kiserikali

Nahitaji kuwa na nini na nini maana mwanamke ninaye. Lengo kuu ni kutaka kufanya mambo mengine nikiwa na huyu mwanamke maana Kuna vitu nashindwa kumkamilishia mpaka awe ndani ya ndoa ya serikali.

Na njia gani naweza kutumia Ili nifanikishe Ili jambo.

Ni hayo tu watanzania wenzangu.
Kama lengo lako la kuoa ni kujiepusha na zinaa ndoa ya kiserikali haiwezi kukusaidia nenda kafunge ndoa msikitini, kanisani au hata ya kimila. Ndoa ya Serikali ni zinaa iliyorasimishwa kisheria.
 
Naomba kujua utaratibu wa kufunga ndoa ya Kiserikali

Nahitaji kuwa na nini na nini maana mwanamke ninaye. Lengo kuu ni kutaka kufanya mambo mengine nikiwa na huyu mwanamke maana Kuna vitu nashindwa kumkamilishia mpaka awe ndani ya ndoa ya serikali.

Na njia gani naweza kutumia Ili nifanikishe Ili jambo.

Ni hayo tu watanzania wenzangu.
anae funga ndoa bomani huyo kaikana imani yake ya dini
 
Back
Top Bottom