Naomba kujua tofauti kati ya Watekaji na Magaidi ili wakija niweze kuwagundua na kujihami nao haraka

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,018
16,801
Kama kuna yoyote anayejua tofauti kati ya Mtekaji na Gaidi tafadhali anisaidie kuwajua ili niweze kujiandaa kama nikikumbana nao kwani huwezi jua kwa haya matukio yetu tunayoyaona hapa Tanzania kuchukua tahadhari mapema ni jambo la muhimu sana.

Kwa mfano Mwanaume anayetembea na Mkeo ataitwa Mtekaji au Gaidi?

na je

Kwa mfano Mwanamke anayemtupa Mwanae mtaroni atakuwa ni Gaidi au Mtekaji?

Karibuni.
 
wewe ni cleverbright, utawatambua tu bila hata JF kukupa mbinu za kuwajua
 
Mtekaji hutekeleza shughuli zake za uhalifu kupitia kuteka (kukuchukua na kukupeleka kusiko julikana au kukuzingira katika eneo hilo hilo) kisha hukuachia kwa masharti husika .
Ghaidi aweza kuwa mtekaji lakini aweza kushambulia hadharani bila kukuteka. Ghaidi wanajulikana ila watekaji wapo kisiri siri sana.
Ghaidi wako kimataifa zaidi na shuguli zao zinaathiri watu wengi zaidi ya Mtekaji.
Kwa ufupi Utekaji uko ndani ya ughaidi .
 
Utekaji na Ughaidi ni zaidi ya Mwanaume kutembea na mkeo au Mwanamke kutupa mtoto.
Mmoja hapo ni Mchepukaji mwingine ni Katili
 
Kuanzia sasa yeyote unayepishana naye ni mtekaji mpaka rais atoke nje aseme kuwa usalama umeimalishwa na hakuna mtekaji
 
Gaidi anaweza ua watu mia 200 wakati aliemkusudia ni m1 au wa2. Ila mtekaji anamlenga muhusika au wahusik n kwenda kusikojulikana na kuwatesa au kwa masharti maalum utoe pesa then wamuachie.
 
Jichunguze kwanza. Nadhani hujanielewa. Lakini ni vizuri na muhimu kumpoteza kila anayepanga kukupoteza, na umefikilia mengi kuhusu kiongozi, umetamani kufanya maamuzi ambayo kwako unaona ndio sahihi. Hadi hapo wewe pia ni gaidi na mtekaji, shida umekosa kampani tu.
 
Back
Top Bottom