Naomba kujua sifa za sufuria za non stick

Habari wakuu.

Natamani nifanye jiko la nyumbani kwangu liwe la tofauti kidogo na nimeona Kuna hizi sufuria za non stick ambazo zimekuwa maarufu sana.
Naomba mwenye kuzijua vizuri anielezee sifa zako.
Moja ya kitu nachotaka kujua ni kama naweza kunitumia kama sufuria lakini pia kama hotpot.

Wanasema kuwa haziunguzi chakula. Kuna ukweli ndani yake au lah?
Vipi kuhusu usalama kiafya ukizingatia material yake.

Asanteni
Sizipendi haziweki UKOKO ukipika wali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala lawali ni special Case mie lazima nipike wali kwenye Mkaa aisee wali wa kupalia mtamu bhana
Mchele uwe wa Mbeya
Nazi ziwe halisi
Sufuria liwe la alminium
d23325c6e656336ff3da0add2c2aeb82.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Non stick fry pan ni nzuri, mi natumia kukaanga mayai, chapati ya Mchele au chapati maji, chapati ya kawaida, bila kuweka mafuta na zinatoka vizuri, kwa wale wasiopenda mafuta Kama Mimi ni nzuri kupikia vitu hivyo.
 
Sizipendi haziweki UKOKO ukipika wali

Sent using Jamii Forums mobile app
Na raha ya wali asubuhi uamkie kiporo chenye ukoko a.k.a carpet(enzi hizo chuo cha mipango kwa mama mjeshi unanunua ukoko kabla hata hajapika wali alafu unazama class kugonga pindi ukitoka unakuwa na chupa ya maji masafi unazama toilet una-download maji direct kwa mama mjeshi kuchukua order yako
 
Tulikuwa tunapenda sana hayo ma non stick, baadae ukishakuwa na familia unaanza kuwa na machale kwenye kila unachonunua, ndipo nilipokutana na scandal ya teflon na wakaazi mji wenye viwanda vya kutengeneza hizo teflon marekani walikuwa wanakufa kwa cancer
Sufuria za bati hizo zinazouzwa mitaani ni bora mara elfu, kawaunge mafundi na pia wewe kwa afya yako

View attachment 2760879
Hebu toeni picha ya sufuria ya teflon. Tuwahi huko home tuombe wife akague.
 
Haya masufuria yamekuwa mengi sana Hadi yanachanganya. Kila rangi ipo aisee
 
Haya masufuria yamekuwa mengi sana Hadi yanachanganya. Kila rangi ipo aisee
Fake yapo kibao mkuu...ukitaka og Sana nenda supermarket kubwa masaki na Samora...kuna za Professional na Tefal my favourite brand...
Mfuko uwe vizuri Sana kununua hizo uwe na 300 na zaidi
 
Kama ni rangi ya shaba ndani, itakuwa ni copper pia inasemekana sio nzuri kwa kuwa matumizi ya muda mrefu hasa kwa mapishi yenye tindikali(acid) ya asili i ikiwemo nyanya na malimau, husababisha mmomonyoko wa shaba kuchanganyikana na chakula ambao shaba ni hatari ikingia mwilini.
Hizo zenye utando mweusi, ambazo zinaitwa non stick, zinatengenezwa na mchangayiko wa kemikali hatari sana ambazo zingine zimepigwa marufuku, lakini sasa kwa nchi kama Tanzania sijui hata watafuatilia zinatoka wapi au zinatengenezwa vipi
Sufuria nzuri ni zilizotengenezwa na stainless steeel kama hizi chini hapa ambazo ndio zinazojulikana kwa kuwa ni salama zaidi kwa matumizi ya vyombo vya mapishi.

View attachment 2777205
Barikiwa Sana Mkuu. Taken with care. Much appreciated.
 
Habari wakuu.

Natamani nifanye jiko la nyumbani kwangu liwe la tofauti kidogo na nimeona Kuna hizi sufuria za non stick ambazo zimekuwa maarufu sana.
Naomba mwenye kuzijua vizuri anielezee sifa zako.
Moja ya kitu nachotaka kujua ni kama naweza kunitumia kama sufuria lakini pia kama hotpot.

Wanasema kuwa haziunguzi chakula. Kuna ukweli ndani yake au lah?
Vipi kuhusu usalama kiafya ukizingatia material yake.

Asanteni

Kwa upande wangu faida zake ni tatu

Hazigandishi chakula
Haziunguzi chakula
Nikiosha ni rahisi manake chakula hakigandi
 
Zina chemchemi ndani yake kwamba haziunguzi chakula? Hizo ni lugha za wafanyabiashara tu, na kuwanasa wanaopenda "vitu vya tofauti"

Mimi si mfanyabiashara ila nimtumiaji suala la kutounguza ni kweli haizunguzi chakula kitachemka mpaka kikauke huezi kuta kina ukoko wa kuungua labda uichune na upate original
 
Back
Top Bottom