Kuhusu mwimbaji wa nyimbo za dini Sifa Bujune anayeshikiliwa na polisi kinyume na sheria Mbeya

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
Moja ya vitu vilivyonishangaza kwa huyu RPC wa Mbeya ni pale nilipojua kuwa amesoma sheria na ni wakili aliyeapishwa. Najiuliza maswali kadhaa juu ya RPC huyu

1. Aliwezaje kuwa wakili kama ni kilaza wa sheria za haki jinai namna hii kiasi kwamba anaweza kumshikilia mtu siku 7 kinyume na sheria?

2. Tangu lini tuhuma za uchochezi zikawa kipimo cha kujua uraia wa mtu? Au CCP chuo cha polisi wanafundisha kuwa ukiona mtu anaimba nyimbo za kukosoa serikali si raia wa Tanzania?

3. Kwamba Jeshi la Uhamiaji Mbeya ambalo askari wake wamefunzwa na wana taaluma ya kutoka chuoni ya kujua na kutambua uraia wa mtu yeyote walishindwa kumtambua Bi. Sifa Bujune isipokuwa polisi Mbeya wasiokuwa na taaluma hiyo? Au ni kiherehere tu cha polisi kutaka kuwaharibia uhamiaji Mbeya ioneshe ni wazembe kutambua wahamiaji haramu mpaka wasaidiwe na polisi?

4. Kwamba tuhuma za Bi. Sifa Bujune zinahusiana na nini uraia wake? Si afikishwe mahakamani kwa tuhuma za uchochezi kama uhamiaji nao wameona sio raia watamhoji kwa muda wao?

5. Bado najiuliza kama RPC huyu ni wakili ni mteja gani anaweza kumpa kazi ya kesi yake kama uwezo wake ndio huu? Yani ana taaluma ya sheria na ni wakili halafu performance yake inakuwa mbovu namna hii? Ni uoga wa maisha kwamba hawezi ku- survive bila u- RPC?

Mwisho timu yetu ya mawakili kuanzia kesho watakuwa wanaanda mashitaka binafsi dhidi ya askari wanaovunja sheria kwa utashi wao binafsi. Kwa hiyo watashitakiwa wao kwa majina yao na sio vyeo vyao na watetewa na mawakili wao binafsi na sio wa serikali. Mashitaka hayo yatatanguliwa na samasi ya kuwajulisha askari hao na watapelekewa na karani wa mahakama majumbani kwao.

Asanteni Sana.

Mdude Nyagali 7 x 70

Pia Soma: Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara
 
Msaidieni huyo dada, mfundisheni mipaka ya kutunga nyimbo za Mungu.

Pengine elimu yake kuhusiana na Neno la Mungu bado ni changa.
 
Moja ya vitu vilivyonishangaza kwa huyu RPC wa Mbeya ni pale nilipojua kuwa amesoma sheria na ni wakili aliyeapishwa. Najiuliza maswali kadhaa juu ya RPC huyu
Bado najiuliza kama RPC huyu ni wakili ni mteja gani anaweza kumpa kazi ya kesi yake kama uwezo wake ndio huu? Yani ana taaluma ya sheria na ni wakili halafu performance yake inakuwa mbovu namna hii? Ni uoga wa maisha kwamba hawezi ku- survive bila u- RPC?
 
Moja ya vitu vilivyonishangaza kwa huyu RPC wa Mbeya ni pale nilipojua kuwa amesoma sheria na ni wakili aliyeapishwa. Najiuliza maswali kadhaa juu ya RPC huyu
Mwisho timu yetu ya mawakili kuanzia kesho watakuwa wanaanda mashitaka binafsi dhidi ya askari wanaovunja sheria kwa utashi wao binafsi. Kwa hiyo watashitakiwa wao kwa majina yao na sio vyeo vyao na watetewa na mawakili wao binafsi na sio wa serikali. Mashitaka hayo yatatanguliwa na samasi ya kuwajulisha askari hao na watapelekewa na karani wa mahakama majumbani kwao.
 
Utawala wa Sheria unafeli sana kwanini mtu awekwe remanded muda wote huo?
 
Msaidieni huyo dada, mfundisheni mipaka ya kutunga nyimbo za Mungu.

Pengine elimu yake kuhusiana na Neno la Mungu bado ni changa.
Huo wimbo kwa maoni yako una elements zozote za uchochezi?

Bibie, hata ukeshe usiku na mchana hakuna uchochezi wowote hapo na ndiyo maana wame divert kosa badala ya uchochezi sasa imekuwa ni mashaka ya uraia wa binti huyu!!

Very pathetic and unprofessional police force..
 
Back
Top Bottom