Naomba kujua sehemu ya kupata miwani ya macho kwa bei nafuu

Morning_star

JF-Expert Member
Apr 21, 2018
4,159
11,473
Tayari nina vipimo vya daktari vya macho yangu. Hivi kwanini miwani ya macho inauzwa bei ghali? Nimetembelea maduka kadhaa ya miwani bei sio chini ya 600,000.

Wapi wanauza bei iliyopoa?
 
Mkuu, yaani hata mimi huwa sielewi logic ni nini!
Vipimo na lensi huwa ni bei ndogo, lakini frame sasa, khaa!!

Mimi nakumbuka nilienda clinic flani kule Mbeya pale Kabwe, vipimo ni tsh 5000/= na kama lensi imevunjika inatakiwa kubadilisha ni @ tsh 1000/=

Sasa frame jamaa anauza kuanzia elfu 35 mpaka laki na sabini na tano!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tayari nina vipimo vya dakitari vya macho yangu. Hivi kwanini miwani ya macho inauzwa bei ghari! Nimetembelea maduka kadhaa ya miwani bei sio chini ya 600,000. Wapi wanauza bei iliyopoa?

Halafu eti Bima ya afya NHIF wanalipa 20,000/- hebu oneni jamani

Yani inachosha mpaka basi.

Lakini wao wanajilipa vizuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio vipimo ninavyo! Niko Dar! Ni PM please!

Pale Posta Mpya na Clock Tower kuna jamaa wamepanga miwani mingi sana hapo nje, ya aina zote kuanzia TShs. elfu tano hadi elfu kumi tu, yenye fremu nzuri ndiyo elfu kumi na tano kuendelea. Ila lensi zake ni mwaka mmoja zinaishiwa nguvu. Ni ya kutoka China na Taiwan. Miwani yenye viwango niyo hiyo kuko ulikotajiwa hayo malaki...
 
Nenda macho kule kama unaelekea koko karibu na hospitali ya CCBRT , hapo nje kuna sehemu nyingi wanauza miwani.
Bei kubwa sana hata hapo! Kuna miwani inayoweza kuendana na vipimo lakini kanjanja! Muwani hata ukidondoka toka juu ya coffee table hadi chini lenzi inapasuka au ukiifuta tu na kidole au kitamba lenz inakwaruzika!

Utaitumia wiki mwezi lazima uitupe. Naongelea miwani standard and original (maduka ya miwani wanajua) bei hiko juu. Na zina serial number zake na wakati mwingi unalipia leo utaambiwa njoo uchukue wiki kadhaa au mwezi. Hizi miwani bei imechangamka si chini ya 600k. Nikipata around 350k sio mbaya kwasababu tatizo ndo linaanza!
 
Pale Posta Mpya na Clock Tower kuna jamaa wamepanga miwani mingi sana hapo nje, ya aina zote kuanzia TShs. elfu tano hadi elfu kumi tu, yenye fremu nzuri ndiyo elfu kumi na tano kuendelea. Ila lensi zake ni mwaka mmoja zinaishiwa nguvu. Ni ya kutoka China na Taiwan. Miwani yenye viwango niyo hiyo kuko ulikotajiwa hayo malaki...
Siongelei miwani ya urembo au miwani ya jua! Naongelea medical glasses! Eye glasses! Kwamfano naanza kuexperience long site nikaenda hospital nikafanyiwa vipimo na kupewa namba ya aina ya lenz. Unaenda kwenye duka la eye medical glasses watakachokuomba ni namba ya lens kutoka kwa dakitari. Wataenda kwenye store au database na kuangalia wakiona wanayo wanakupa. Kama hakuna unalipia %fulani unaagiziwa. Hiyo miwani bei.

Nakumbuka kuna jamaa kwa kutojua alivunja miwani ya jamaa yangu kimasiala akadhani ndo hizo unazozisema! Alikamatwa kawekwa ndani! Kutajiwa bei 1.2mil. Ikabidi wazazi wajichange! Don't mess up with eye medical glasses!
 
Nenda Vision plus for eye clinic wapo shoppers plaza Mikocheni, bei zao ni nafuu sana. Mimi nilikwenda hapo checkup charge ilikuwa Tsh. 20,000/= na miwani nililipia Tsh. 150,000/= na chanzo cha kupajua hapo Bima yangu inalipa kwenye tatizo la macho si zaidi ya Tsh. 180,000/= sasa kila nikizunguka kwenye Eye clinic gharama zipo juu ndio nikaelekezwa hapo.

Hiyo bei inasomeka! Umekaa na hiyo miwani muda gani?
 
Ukipata miwani feki inaweza kuharibu kabisa macho yako na kuwa pia umepoteza hela! Ni sensitive issue!
 
In liquid manufactured, ni kitu gani kizuri kitumike kusafishia miwani ya macho ili idumu zaidi.
 
Back
Top Bottom