Naomba kujua Salimu Mwalimu yuko wapi, kimya kimezidi.

Naomba kujua Salimu Mwalimu yuko wapi, kimya kimezidi.

idawa

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2012
Posts
25,304
Reaction score
38,476
Huyu kijana ni kati ya vijana wachache waliokuwa wanakuja kasi sana kwenye siasa za nchi yetu hasa upande wa upinzani.

Ilifikia wakati akatabiriwa kuwa anaweza kuvaa viatu vya Ukatibu Mkuu Chadema, kulingana na siasa misimamo na uadilifu wake na alionekana kuwa ni lulu ya Taifa kwa baadae.

Lakini mpaka sasa sijui bado ni Naibu katibu Mkuu Chadema ama alisha staafu, ama ujio wa Lowasa umemchanganya kijana hajui afuate njia ipi aache njia ipi.

Salumu Mwalimu tuambie uko wapi,?
mpaka sasa ndani ya Chadema sijaona kijana wa kuvaa viatu vyako...
c0eebb18e68a20b38556bc5282558274.jpg

f263f352789a877734a40eb25190e096.jpg
 
Ujio wa lowasa chadema unaua vipaji. Ukiangalia kwa makini utatambua siyo yeye tu, hata akina Mnyika wamepotea kabisa. Vijana wanaojitutumua wanaenguliwa kwenye kinyang'anyiro kimizengwe. Mfano, Sosopi alivyozimwa ili kumwachia Msigwa uenyekiti wa kanda kisa msigwa ni chaguo la wakubwa. Kwa mwenye akili anaamua kukaa pembeni na kuusoma mchezo.
 
Alishazalisha wa Dada zake ndani ya cdm sasa kapumziaka

Ila urejeo WA sepenga cdm utamuona atarudi siku si nyingi
 
Ujio wa lowasa chadema unaua vipaji. Ukiangalia kwa makini utatambua siyo yeye tu, hata akina Mnyika wamepotea kabisa. Vijana wanaojitutumua wanaenguliwa kwenye kinyang'anyiro kimizengwe. Mfano, Sosopi alivyozimwa ili kumwachia Msigwa uenyekiti wa kanda kisa msigwa ni chaguo la wakubwa. Kwa mwenye akili anaamua kukaa pembeni na kuusoma mchezo.
Mkuu uko sahihi, sasa hivi vipaji vipya Chadema hakuna kabisa zaidi ya vibaraka wa Mbowe.

Ukiangalia wakati ule kulikuwa na vipaji kila mkoa na vilikuwa vinasikika lakini sasa hivi kimya sana.
Ujio wa Lowasa hautamwacha salama Mbowe
 
Kwanza tuambie Josephine Mushumbus yuko wapi? Manake wewe hueleweki; kuna wakati watanzania walihisi wewe ni competitor wa Josephine! Hebu tujuze ulisham-outcompete?
Jielekeze kwenye mada Mkuu
 
Ujio wa lowasa chadema unaua vipaji. Ukiangalia kwa makini utatambua siyo yeye tu, hata akina Mnyika wamepotea kabisa. Vijana wanaojitutumua wanaenguliwa kwenye kinyang'anyiro kimizengwe. Mfano, Sosopi alivyozimwa ili kumwachia Msigwa uenyekiti wa kanda kisa msigwa ni chaguo la wakubwa. Kwa mwenye akili anaamua kukaa pembeni na kuusoma mchezo.

..MARUFUKU ya mikutano ya hadhara nayo inachangia kufifisha zoezi la kuibua vipaji vipya.
 
Back
Top Bottom