Naomba kufahamishwa Cloud Storage ya bure at least 30 GB

Naomba kufahamishwa Cloud Storage ya bure at least 30 GB

Erick Martie

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2015
Posts
341
Reaction score
371
Wakuu ningependa kujua Cloud Storage ya bure na yenye at least GB 30 capacity inayohusisha mfumo wa android, kama unaifahamu yoyote tusaidiane kufahamishana [emoji120]
 
Unatumia simu ya kampuni gani? Ni km Samsung huwa wanatoa 115GB bure (km sijasahau).
 
Unatumia simu ya kampuni gani? Ni km Samsung huwa wanatoa 115GB bure (km sijasahau).
Simu nabadilisha badilisha sana mkuu hivyo ningependa nikiwa na simu yoyote niweze kupata access na cloud storage
 
Tupe elimu na sisi hiyo Cloud storage ndo nini na inasaidia nini kwenye simu
Cloud Storage: Nitaelezea kwa lugha ya kawaida na Kwa lugha ya kitaalamu (More Technically)...

Kwa Lugha rahisi/ya kawaida - ni technolojia inayokuwezesha kutunza mafile yako (picha,video,documents nk) katika huduma ambazo zitakuwezesha kuweza kupata(kuchukua/kuendelea kutunza) izo files zako popote kwa kutumia device/kifaa chochote, unachotakiwa kufanya ni kuwa na account kwenye izo huduma(google, microsoft, amazon etc..) ambayo kupitia application zao kwenye devices mbalimbali unakua unalogin tu kwenye account yako(kwenye izo apps/website/any platform ) na kuweza ku-access files zako

Technically:- Cloud Storage ni moja kati ya huduma za Cloud Computing..
Simply Cloud Computing include:
Cloud Computing infastructures (eg. Virtual Machines like Operating Systems, VPNs etc),
Cloud Computing Platforms (mara nyingi for developers),
Cloud Computing Services (hapa watu wengi huzitumia kila siku bila kujua kua wanatumia cloud services eg. emails, Cloud storage services (google drive, dropbox...), aws, microsoftAzure etc, hata matumizi ya facebook, instagram, twitter etc uses cloud storage), kuna mifano mingi sana),

Yote hayo hupatikana kupitia kampuni mbalimbali kama Google, MicroSoft, Amazon etc
 
Unapozungumzia cloud storage unamaana gan mkuu? Samahan lakin nimeuliza kwa niaba ya wasiojua wenzangu......!! Kaka chief mkwawa ebu tusaidie sis tusiojua maana ya cloud storage
 
Cloud Storage ni nini na Inafanyaje kazi?
Tafadhali msituache hapa Mkuu!
Cloud storage ni mfumo wa kuhifadhi mafile kupitia internet. Kunakuwa na computer zenye storage za kutosha, kupitia internet unahifadhi mafile yako kwenye hizo computer.

Kuelewa zaidi hata wewe unaweza ukanunua Nas server, ukawa na app mahala popote ukawa unahifadhi mafile yako kwenye server yako Nyumbani.

SYNOLOGY_DS1019P_01.jpg
 
Shukrani Mkuu kwa Ufafanuzi!
 
Cloud Storage ni mfano wa kompyuta (Cloud Computing) ambayo huhifadhi data(mafile) kwenye mtandao kupitia mtoa huduma ambaye anasimamia na kuendesha uhifadhi wa data.

Cloud Storage hutumia vituo vya data na seva kubwa za kompyuta ambazo huhifadhi data(mafile) na kuifanya ipatikane online kwa watumiaji kupitia wavuti(website au App). Watumiaji wanaweza ku-upload data(mafile) zao kwa mbali, kuzihifadhi na kuzipata (data/mafile) wakati na anapohitaji.

Cloud Storage inajumuisha angalau seva moja ya data ambayo mtumiaji huunganisha kupitia mtandao. Mtumiaji hutuma faili manually au kwa mtindo wa kiotomatiki mtandaoni kwa seva ya data(mafile) ambayo inasambaza information kwa seva nyingi. data(files) zilizohifadhiwa zinaweza kupatikana kupitia wavuti, applications nk mfano (Google Drive, Dropbox, One Drive nk).

Mfano wa Cloud Storage inayotumika sana ni Google Drive...

Google Drive
ni suluhisho la kuhifadhi data/mafile linalokuruhusu save faili online na kuzifikia/kuzipata mahali popote kutoka kwa smartphone yoyote, tablet, au kompyuta.

Unaweza pia kutumia Google Drive kwenye kompyuta yako au Smartphone u ku-upload data/mafile salama na kuedit online.

Google Drive pia hufanya iwe rahisi kwa wengine ku-edit(kufanya mabadiliko yoyote) na kushirikiana kwenye faili (kama word documents au excel nk.) kama tu mtakua mnashare google account moja.

NB: data/mafile = picha, video, documents nk
 
Namna ya kutumia Cloud Storage haswa Google drive kama kuna uhitaji nitaendelea...
 
Cloud storage ni mfumo wa kuhifadhi mafile kupitia internet. Kunakuwa na computer zenye storage za kutosha, kupitia internet unahifadhi mafile yako kwenye hizo computer.

Kuelewa zaidi hata wewe unaweza ukanunua Nas server, ukawa na app mahala popote ukawa unahifadhi mafile yako kwenye server yako Nyumbani.

SYNOLOGY_DS1019P_01.jpg
Mkuu, hizi naona bei zake zimesimama sana, mimi niliamua kutafuta desktop kutumia kama saver ingawa hizo NAS ni nzuri zaidi
 
Mkuu, hizi naona bei zake zimesimama sana, mimi niliamua kutafuta desktop kutumia kama saver ingawa hizo NAS ni nzuri zaidi
Changamoto ya desktop ni ulaji umeme ikikata on 24/7, Sema ni kweli desktop ni alternative ya bei rahisi.

Siku hizi vipo videsktop kama vya raspberry ama vinavyotumia Atom cpu watu wanatumia kwa ajili ya Nas vinakula umeme kidogo sana.
 
Back
Top Bottom