Naomba kuelimishwa ni kwanini Makamu wa Rais Samia hakuwa mtu wa kwanza kupewa taarifa ya kifo cha Hayati Dkt. Magufuli?

Lucas Mimi Si chawa mwenzio,

Nimekushauri pima ulichokiandika kabla ya kupeleka public,

HOJA Yako unalazimisha watu waulize maswali ambayo majibu yake kamwe hayawezi kupatikana Kwa sababu maalum.

Pima uzito wa kinywa chako kabla hujaongea Lucas.
Huyu chawa upeo wake ni mdogo sana yeye anachofikiria ni uteuzi tu.
 
Pia inaonesha cheo Cha Makamu wa Rais ni cheo Cha maigizo kisicho na maana.

Yaani Waziri Mkuu ndio anapata nafasi ya kwanza kabla ya VP? Haikubaliki kina haja ya kubadili sheria au kufuta hiki cheo
Nafasi ya MwR kipo kisiasa tu, tena kwa sababu ya muungano ili kubalance equation ya muungano ila hakina maslahi yoyote kwa taifa. Ni hasara kw ataifa kuwa na MwR na WM kwa wakati mmoja, huyo mmoja yupo yupo tu.
 
Makamu wa Rais wetu ni cheo cha kisiasa, ila hakina mamlaka. Ndiyo maana hawatengui uteuzi na wala hawateui.

Pia, ieleweke kubwa Rais anapokuwa mgonjwa, ndipo ratiba ya kazi ya Makamu wa Rais huongezeka zaidi ya awali, za kwake na za Rais.

Majukumu ya nchi lazima yaendelee, maana maelezo yako yamekuwa kama unadhani Makamu wa Rais ni mke wa Rais.

Kwamba Makamu wa Rais awe kando ya kitanda cha hospitali cha Rais na afute ratiba zote za kazi. Hili nadhani si sawa. Kazi lazima iendelee.

Ova
 
Ndugu zangu Watanzania,

Nimeisikiliza mara mbili mbili video ya mkuu wa majeshi mstaafu jenerali Venance Mabeyo aliyekuwa ndiye mkuu wa majeshi wakati wa kifo cha hayati Dkt Magufuli. Nimemsikiliza neno kwa neno na mstari kwa mstari na kufanya uchambuzi wa kina sana kichwani mwangu juu ya mambo mbalimbali ambayo viongozi wetu hasa wa kisiasa walikuwa nayo vichwani mwao, kila mtu alikuwa na lake kichwani mwake na matamanio yake na kiu yake baada ya kifo cha Hayati Dkt Magufuli.

Nitaanza na mara baada ya kifo juu ya nani awe mtu wa kwanza kupewa taarifa. Hapa tumeelezwa na mkuu wa majeshi kuwa waziri mkuu na katibu mkuu kiongozi ndio viongozi waliokuwa wa kwanza kupewa taarifa ya kifo cha Mpendwa wetu Hayati Dkt Magufuli. Sasa swali nalojiuliza mimi Mwashambwa ni kuwa kwanini waliitwa viongozi hawa kupewa taarifa za kifo cha Rais ambao kiwadhifa ni wadogo kwa makamu wa Rais? Pili kama ilionekana Tanga ni mbali sana kwa makamu wa Rais kufika Dar na badala yake kuamua kuwaita wa Dodoma, je ni kwanini Makamu wa Rais asingetumiwa usafiri wa ndege au helikopta kurejea haraka sanaaa Dar es Salaam tangia siku moja ya kabla ya kifo chake hayati Dkt Magufuli tokea pale alipomwambia mkuu wa majeshi kuwa yeye hawezi kupona na awaamuru madaktari wampeleke kwao Chato ili akafie huko?

Kwanini pia mkuu wa Majeshi alipotuma gari na dereva kuwaita Kardinali Pengo pamoja na paroko Makubi kuja kumfanyia maombi hayati dkt Magufuli asingetuma usafiri wa haraka kwenda mkoani Tanga kumrejesha Makamu wa Rais Dar ili awe karibu na asiendelee na ziara mkoani Tanga? Kwanini pia Makamu wa Rais alipangiwa na aliendelea na ziara wakati kipindi Rais wake akiwa mahututi kitandani? Kwanini hakupewa taarifa za mapema? Mfumo wa taarifa serikalini upoje? Inakuwaje makamu wa Rais akose kuwa mtu wa kwanza kuwa na taarifa ya kifo cha Rais wake halafu aende apewe waziri mkuu pamoja na katibu mkuu kiongozi ambao kikatiba hawana hata mamlaka ya kutangaza kifo cha Rais?

Hamuoni hii jambo lilimdogesha Makamu wa Rais? Hamuoni hili jambo liliwapa nguvu kubwa watu ambao hawakustahili kikatiba? Kwa sababu nguvu nayoizungumzia ni ile iliyoelezwa katika katiba kuwa akitoka Rais nani anafuata kimamlaka. Nani alipanga ziara ya Mheshimiwa Makamu wa Rais kwenda Tanga? Je makamu wa Rais alikuwa anafichwa taarifa nyingi za Rais wake ikiwepo hali yake ya afya? Kama jibu ni ndio kwanini ilikuwa hivi? Je pale Rais alipokuwa hayupo vyema kiafya na amezidiwa kama ilivyokuwa mpaka kifo, je mkuu wa majeshi kwa niaba ya wakuu wenzake wa vyombo vya ulinzi na usalama kwanini alikuwa hampatii taarifa Makamu wa Rais? Kama alikuwa anampatia taarifa makamu wa Rais naamini basi hata ziara ya Tanga ingekatizwa Haraka Sana na kurejea Dar ili kujiandaa kwa lolote lile ambalo lingetokea na hivyo kuutangazia umma wa Watanzania akiwa hapa hapa Dar.

Kwa sababu katiba ipo wazi kabisa kuwa anapokuwa amefariki Dunia Rais anayetakiwa kutangaza kifo hicho ni makamu wa Rais na hivyo huyu aliyetajwa katika katiba ilipaswa awepo karibu hapa hapa Dar, na ikiwezekana pembeni kabisa ya kitanda cha Rais wake katika dakika za mwisho za uhai wake mpaka anapokata roho kama walivyokuwepo viongozi hao watatu wa vyombo vya ulinzi na usalama. Hapo ndipo sasa majadiliano yangeanza kufanyika nani sasa wapewe taarifa zaidi, ambapo ndipo sasa waziri mkuu na katibu mkuu kiongozi wangeitwa haraka sana kuja Dar ili mipango mingine ya uratibu wa taarifa iendelee kama ilivyokuwa kumpa taarifa mke wa marehemu pamoja na kutuma usafiri kwenda kumfuata mama mzazi wa marehemu kule Chato kuja Dar.

Pili katika maelezo ya jenerali Venance Mabeyo ukimsikiliza kwa umakini kabisa unagundua waziwazi bila kutumia akili kubwa wala elimu kubwa, kuwa kuna watu wenye nia ovu walitaka kupindisha katiba na matakwa ya katiba juu ya kukabidhiwa na kuapishwa kuwa Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan. Ndilo maana kuna mahali wengine wakatoa ushauri wa kupotosha na wenye nia ovu kusema kuwa tupo kwenye msiba kwa hiyo baadhi ya taratibu zisifanyike. Lakini jenerali Venance Mabeyo akawaambia wazi na kwa ujasiri kuwa ni lazima taratibu zote zifanyike katika kumuapisha maana zisipofanyika basi jeshi halitamtambua Rais.

Na hapo inanipa jibu kuwa waliokuwa wanashauri haya wali kuwa na malengo yao, kuwa baadhi ya taratibu zisipofanyika basi waje watumie mwanya huo kutimiza malengo yao ovu na yenye kuleta taharuki hapa nchini pengine hata kuhatarisha usalama wa Taifa. Kwa sababu katiba yetu ipo wazi kabisa juu ya nini kifanyike pale Rais aliyepo madarakani anapofariki Dunia.

Kwa hiyo ni Mungu aliamua kulivusha salama Taifa letu katika wakati mgumu ambao kuna baadhi ya watu pengine waliingiwa na mioyo ya tamaa ya kutaka kutimiza haja za mioyo yao yakutaka kutwaa madaraka kinyume na katiba inavyosema.

Watanzania wote hatuna budi kusimama kwa pamoja kumpongeza kwa dhati kabisa jenerali Venance Mabeyo kwa ujasiri wake na uzalendo wa kuamua kusimamia katiba na kuitii na kuiheshimu kuhakikisha kuwa inafuatwa bila kupindishwa na mtu yeyote yule kwa maslahi yake binafsi. Japo naamini ametumia hekima, busara na uzalendo mkubwa sana. Maana naamini kifua chake kimebeba makubwa moyoni yaliyotokea na yaliyotaka kutokea na kufanyika baada ya kifo cha hayati Mwalimu Dkt John Pombe Joseph Magufuli ambayo yeye aliyazuia na kuamua kuilinda katiba. Kwa sababu za kiusalama na kimaadili, naamini hawezi kuyasema mpaka anaingia kaburini. Siri inabaki kwake na Mungu wake.

Somo hapa ni kuwa ukiwa Rais wa nchi basi kosea vyote lakini usikosee wala kufanya makosa ya kuteua mkuu wa majeshi. Teua mkuu wa majeshi mzalendo, mwenye utulivu wa akili na moyo, mwenye upendo na aliyetayari kuifia nchi yake, aliye tayari kuilinda katiba kwa jasho na damu. Teua mtu mwenye utimamu wa akili na mwili, mwenye busara, hekima, utulivu, ukomavu wa akili asiye na mihemuko na tamaa ya madaraka wala pesa wala vyeo wala nini. Teua mtu anayewapenda Watanzania wote bila kujali ukabila, udini, ukanda wala jinsia ya mtu.

Kwa hakika Jenerali Venance Mabeyo ataingia katika kitabu cha majenerali wazalendo wa Taifa letu na waliolivusha Taifa letu katika kipindi na nyakati za giza na ngumu sana.

Asante Mungu pia kwa kuendelea kuweka mkono wako juu ya Taifa letu. Si kwa ujanja wetu bali ni kwa neema yako. Ndio maana Taifa letu linaendelea kutamalaki kwa amani na utulivu.

Asante Rais Samia kwa kuendelea kuongoza Taifa letu kwa uzalendo na upendo mkubwa. Usikivu wako umepongezwa waziwazi na jenerali Venance Mabeyo mwenyewe kwa ulimi wake. Ni Mungu tu ndiye amekufanya ukawa hapo ulipo, ila kuna watu naamini walitamani usiwe katika kiti hicho. Hata hivyo, naamini kwa uchapa kazi wako na uzalendo wako uliouonesha ndani ya uongozi wako, naamini wanaona aibu na wanajuta huko waliko kwa mawazo mabaya waliyoyawaza juu yako na kuwa na hofu na wewe.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia Watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya Watanzania wanyonge wasio na sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.
Unaachaje bosi wako kitandani anapigania uhai wake wewe unakwenda kupiga posho za ziara Tanga? Waliotaka asiapishwe Wana hoja.
 
Nafikiri hapa ni vitu viwili tofauti. Kama rais wa nchi Janeth hahusiki na taarifa. Ila kama Magufuli angekuwa mume wa Janeth tu bila kuwa Rais taarifa ya kwanza ingemhusu. Ila pale Magufuli alikuwa anauguzwa na nchi, siyo mambo ya kifamilia yale

Kahiyo Magufuli alivyokuwa anaumwa taarifa ya kwanza ilipewa nchi? Kumbuka Katelephone alisema Rais yupo fiti anachapa kazi ,katika kipindi cha rais anachapa kazi(kwa mujibu wa katelephone) ina maana Janeth alikuwa hajui kama yupo Mzena?
 
Back
Top Bottom