Naomba kuelimishwa ni kwanini Makamu wa Rais Samia hakuwa mtu wa kwanza kupewa taarifa ya kifo cha Hayati Dkt. Magufuli?

Naona una hoja 2 hapo
1: kwamba kuna uwezekano kuna hila zimefanyika

2: ni kwamba umedharau hivyo vyeo viwili vya waziri mkuu,mkuu wa majeshi na katibu mkuu kiongozi Basi nkujuze,

Kwa kuanza kukukumbusha ni kwamba katibu mkuu kiongozi ndio kiongozi wa shughuli zote za raisi plus yeye ndo kiongozi wa ulinzi na usalama ndani ya ikulu na hata ni kiongozi ndani ya TISS,

Hivyo katibu mkuu kiongozi anaplay part kubwa hasa kwenye swala la ulinzi na taarifa zote ambazo zinafanywa au ziko mezani kwa raisi mfano kuna kazi fulani ya 2B ambayo haikutangazwa kwa umma ambalo alipewa waziri fulani basi ni lazma KK kiongozi ahakikishe ameliweka sawa mostly kwenye situation kama hizi. Bila kusahau issue za ulinzi na usalama kwa kuhakikisha amesuka taarifa ya taratibu zote za ulinzi na usalama wakati wa msiba na maziko kwa ujumla.

Mkuu wa majeshi yeye ndo kiongozi mkuu wa maswala ya usalama ndani ya nchi yeye ndo mwenye kuhakikisha anazuia au kuvunja kila kiashiria cha uvunjifu wa amani au uhaini kipindi taarifa za kifo cha rais kinatangazwa/kutokea.

Naweza kusema hiki ndo kipindi ambacho jeshi linakuwa allert mno na masuala ya ulinzi hasa uhaini na hapa viongozi wengi wa juu wa jeshi wanakuwa under government surveilance kwa kujua au kutokujua maana nchi inakuwa haiko stable.

waziri mkuu huyu ndiyo mwenye kamati zote za maafa na misiba ya kitaifa na yeye ndo mratibu mkuu wa shughuli hizo habari za msiba ufanyike wapi nan ahudhurie na bajeti ya bei gani iandaliwe huyu ndiyo master minder

Mwisho na isiyo na muhimu ni makamu wa rais huyu yeye huandaliwa njia zote na hao watajwa hapo juu,kuhusu lini na muda gani apewe taarifa na lini aapishwe au kukabidhiwa nchi.

Sababu za kutokuambiwa kwa wakati hasa huwa ni kutotengeneza taharuki ndani ya nchi sababu rais wangu samia kama angeambiwa kuwa mwenzake amefariki sidhani kama angekuwa yule aliyekuwa ziarani vile na kumbuka wakati huo kulikuwa na fukuto la rais yuko wapi rais yuko wapi

Nimalizie kwa kusema kipindi kama hichi huwa ni kipindi kibaya mno kwa maropo ropo au wenye uchu wa madaraka kwani huwa ni kipindi cha lala salama jeshi linakuwa macho na ukiwa kimbele mbele au tishio ndug yangu tunakuaga
Afadhali wewe umejibu hoja na siyo yule ccm Rabbon ndugu yake Lukas alikuwa anamtisha.

Hapa Lukas ndo ajue na aelewe kuwa wanaposema kuwa ccm wengi wanajivika uchawa wakidhani kuwa ndo kufia chama kumbe wasijue kuwa wanabomoa. Hapa amepata elimu kwa asiye chawa na s kama alivyokuwa anatishwa na Rabbon.
 
Wanadai anaetakiwa kupewa taarifa namba 1 ni Katibu Mkuu Kiongozi ndio amjulishe Makamu.

Ila Kwa kesi ya Magufuli Bashiru na genge lake hawakutaka VP apewe taarifa na kama angepewa wangekuwa wameandaa Mpango wa kupindua meza.

Inaonekana Bashiru na genge lake walishurutishwa.

Masisitiza ningekuwa Mimi ndio Samia,hakuna rangi wangeacha kuona kuanzia Katelephone na wengine.Kuwatoa kwenye cheo kina Bashiru haitoshi huku wengine Bado hapana.
Hata mimi ningekuwa Samia ningeshughulika sana na wote waliotaka kupindua katiba..... kwa maelezo ya CDF ni kuwa kwanza walitaka kubishia mwongozo wa katiba na baadae wakataka Rais aapishwe baada ya mazishi na mwisho kabisa wakataka kumuapisha kihuni bila utaratibu. Mimi ningewanyoosha na wangejuta maisha yao yote. Tunaposema Mama Samia ni mtu mwema asiye na visasi watu wawe wanaelewa.
 
Unaachaje bosi wako kitandani anapigania uhai wake wewe unakwenda kupiga posho za ziara Tanga? Waliotaka asiapishwe Wana hoja.
Sasa angefanyaje kama alikuwa amefichwa kupewa taarifa? Hujaona katika andiko langu nimeuliza kwanini walimpangia ziara Mh makamu wa Rais kwenda Tanga?
 
Afadhali wewe umejibu hoja na siyo yule ccm Rabbon ndugu yake Lukas alikuwa anamtisha.

Hapa Lukas ndo ajue na aelewe kuwa wanaposema kuwa ccm wengi wanajivika uchawa wakidhani kuwa ndo kufia chama kumbe wasijue kuwa wanabomoa. Hapa amepata elimu kwa asiye chawa na s kama alivyokuwa anatishwa na Rabbon.
Watu wengine wajinga tu .eti badala akuelimishe anaanza kukupa vitisho utafikiri nchi hii ni ya wazazi wake.
 
Kwa sababu katiba haifatwi.

Na hata Samia huyu huyu haiheshimu katiba ndio maana aliita"KIJITABU"

Tunahitaji katiba itakayombana yeyote yule awaye madarakani akikiuka sheria na taratibu .

Katiba hii chakavu ya sasa ina miaka 47 imeshakuwa kama "past papers " za mitihani iliyowahi kufanyika hivyo even nobody no longer give a damn about it.
 
Hata hivyo, pamoja na katiba kumbeba ila walijua fika hana uwezo.... na ndo hiki tunachokiona leo.

Hivyo walijua kabisa ni garasa ndiyo maana ulitokea huo mzozo kabla ya kuamua kukubaliana na hiyo mnayoita katiba.

Je, umewahi kujiuliza kwanini hao wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliomweka hapo wote aliwafurusha?
Unatumia kipimo gani ewe mnyamwezi na sisi tukakinunue? Kipindi Magufuli yupo walikuwepo Kama wewe walimwita the worst president..Mara dikteta uchwara nk. KWA HIYO HATA WEWE KUMUITA HATOSHI WALA SI AJABU NA WALA HUTAENDA KUKIKALIA KILE KITI kwa ufupi vumilia tu mpaka amalize wewe endelea kulima huko ushetu😃
 
Mimi nimeomba kuelimishwa kuwa anayefuatia kimamlaka baada ya Rais ni makamu wa Rais. anayetangaza kifo cha Rais kikitokea ni makamu wa Rais.sasa ni kwanini hakuwa mtu wa kwanza kupewa taarifa ya kifo cha Rais wake? Kwanini walipewa viongozi wengine taarifa mapema ambao ni wadogo kimamlaka na kimadaraka kwa makamu wa Rais?
Hoja yako ni ipi "wa kwanza kupewa taarifa" au "anayetangaza?"
Kuna mahala Katiba imeelekeza juu ya kupewa taarifa? Mkewe angekua wa kwanza pia kupewa taarifa ungelelalamika?
 
Hoja yako ni ipi "wa kwanza kupewa taarifa" au "anayetangaza?"
Kuna mahala Katiba imeelekeza juu ya kupewa taarifa? Mkewe angekua wa kwanza pia kupewa taarifa ungelelalamika?

..kwa hali aliyokuwa nayo Magufuli, Mama Samia alipaswa kuwa ACTING PRESIDENT.

..Na wakati wote Wakuu wa vyombo vya ulinzi na Madaktari walipaswa kuwa wanampa Mama Samia taarifa za hali ya mgonjwa ili afanye maamuzi.

..hivi kwa mfano nchi ingevamiwa wakati ule, ina maana Kassimu, Venance, na Bashiru, wangeendelea na danadana zao?
 
Back
Top Bottom