Naomba kuelekezwa namna ya kuchoma nyama kama toroka uje

mwambojoke

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
1,060
630
Nataka kuchoma nyama kwa ajili ya Familia lakin sijui pa kuanzia. Nadhan nikipata majibu ya maswali yangu ntajua cha kufanya.

A). Sehemu gani ya nyama ya ng'ombe ni tamu kwa kuichoma? Ili nikienda buchani niagize hyo.

B). Nitumie spice gani kwa ajili ya kulainisha nyama yangu?

C) .Nitumie spice gani kwa ajili ya ladha ya nyama?

D) Ntaifanyaje nyama yangu isiwe Kavu yaani iwe 'Juicy' baada ya kuchoma?

NB: Kwa ambao mmefika Toroka uje nyuma ya best bite Kinondoni. Napenda nitoe nyama ifanane vile kwa utamu na ulaini kama kuna mtu anaweza niibia siri.

Asalaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ushanikumbusha toroka uje ngoja kesho niende. Wale mwanzo mwisho nyama inaivia kwenye foil. Ni nyama ya kawaida tu ila wanaweka viungo viungo ngoja wadau waje kuongezea. mwambojoke,
 
Kumbe wadau mnakubalian ana mm tastw ya pale kiboka. Nataka ni gapata maujanja kidogo niige ingekuwa bomba. Na hii corona sijaibuka kitambo pale Toroka uje.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Agizia kidari kisha kichane vizuri ukiweke kwenye maji yenye mchanganyiko wa ndimu kiasi na tangawizi kwa masaa kazaa inategemea na wingi wa nyama kisha itoe uiweke kwenye sehem kavu kwenye jua sio mbaya..kisha ivhome kwenye moto kwaa mbali kwenye foili ita faa zaidi...
Ikiferi nishtue nije

Sent by nCOVID-19
 
agizia kidari kisha kichane vizuri ukiweke kwenye maji yenye mchanganyiko wa ndimu kiasi na tangawizi kwa masaa kazaa inategemea na wingi wa nyama kisha itoe uiweke kwenye sehem kavu kwenye jua sio mbaya..kisha ivhome kwenye moto kwaa mbali kwenye foili ita faa zaidi...
Ikiferi nishtue nije

Sent by nCOVID-19
Haha. Umetisha Mwamba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Agizia kidari kisha kichane vizuri ukiweke kwenye maji yenye mchanganyiko wa ndimu kiasi na tangawizi kwa masaa kazaa inategemea na wingi wa nyama kisha itoe uiweke kwenye sehem kavu kwenye jua sio mbaya..kisha ivhome kwenye moto kwaa mbali kwenye foili ita faa zaidi...
Ikiferi nishtue nije

Sent by nCOVID-19
Naweza kuichoma kwa kutumia oven?

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Chukua ukwaju kisha uroweke kwenye maji,hiyo juice ya ukwaju utakayo ipata baada ya kuuroweka huo ukwaju,mix na chumvi,garlic,na pilipili kama ukipenda,

Halafu hiyo juice ya ukwaju ichanganye na nyama unayotaka kuichoma kisha iache ndani ya chombo ulicho kichanganyia na ukwaju kwa muda wa 1hr au 2hr kisha itoe hiyo nyama ili ivuje yale majimaji kabla ya kuanza kuichoma,

Huu utaalamu kuna mtu aliwahi kunielekeza na nikajaribu.
 
Simple=>
Nunua nyama ya mguu
Icharange + safisha
Viungo:
limao
Kitunguu swaumu
Chumvi
Tangawizi
Pilipil
Namna/kuandaa:
Kamua limao+parua kitunguu swaumu na maganda yake/twanga kwa kinu/kimfuko+kwangua tangawizi+tia chumvi
Loweka nyama katika huo mchanganyiko nusu Saa
Andaa mkaa ,weka wavu,weka mzigo ikiendelea kuiva endelea kunyunyiza ule mchanganyiko kwakupasua kwa ndani ukionaa imeanzakuiva vizuri weka kwenye foil sio lazima kama ni mtaalamu .....nb usisahau kufunga geti majirani ni wanoko sana
 
Nataka kuchoma nyama kwa ajili ya Familia lakin sijui pa kuanzia. Nadhan nikipata majibu ya maswali yangu ntajua cha kufanya.

A). Sehemu gani ya nyama ya ng'ombe ni tamu kwa kuichoma? Ili nikienda buchani niagize hyo.

B). Nitumie spice gani kwa ajili ya kulainisha nyama yangu?

C) .Nitumie spice gani kwa ajili ya ladha ya nyama?

D) Ntaifanyaje nyama yangu isiwe Kavu yaani iwe 'Juicy' baada ya kuchoma?

NB: Kwa ambao mmefika Toroka uje nyuma ya best bite Kinondoni. Napenda nitoe nyama ifanane vile kwa utamu na ulaini kama kuna mtu anaweza niibia siri.

Asalaam.

Sent using Jamii Forums mobile app

ushawahi fika AFIATANGA mbezi.. hao toroka uje watatoroka wao kule kino
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom