Naomba kama kuna mtu anaweza kunisaidia chuo chochote Duniani ambacho kinatoa free degree online


Hao university of the people sio bure kabisa japo wana mitaala mizuri na ni nafuu.
Kuna gharama kama usd 60 kwa usajili.
Pia unalipa usd 100 kwa kila mtihani unaofanya kulingana na bachelor uliyoichagua.

Kama lengo ni kupata tu elimu na kuongeza maarifa, kuna hizi sites wanatoa kozi mbali mbali.

www.edx.org
www.coursera.org
www.udacity.com
www.alison.com

Ukiwa na internet na ukajua kuitumia vizuri ni zaidi ya chuo kikuu.

Kupata chuo cha bure kabisa yaani bure inaweza kuwa ngumu lakini unaweza kuomba msaada wa ufadhili kwa vile vyenye gharama nafuu.

Pia open university yetu watu wanaidharau wanasahau ukishahitim una sifa kama ya mwingine kuwa una degree.

Nikutakie kila la kheri.
Nimeona hiki ni chuo kiko vizuri sana. Gharama ndogo sana
 
Back
Top Bottom