Naomba ‘Connection’, natafuta kazi CCECC au CRJE

Granite

JF-Expert Member
Jul 6, 2016
268
623
Wakuu wenye connection katika kampuni za kichina zenye miradi mbalimbali Mhandisi nakuja kwenu.

Ninao uzoefu wa kutosha katika Site Supervision na Design, nimejitolea katika miradi kadhaa ya ujenzi wa Barabara na Majengo.

Naweza kufanya kazi popote Tanzania na katika usimamizi mdogo na kutimiza malengo ya kazi kwa wakati.

Naomba fursa niweze kuwa sehemu ya timu inayojituma kufikia malengo ya kampuni
 
hakuna cha ajabu hapo hali halisi unaiona hata ukisema ajiaajiri bado mifumo sio rafiki kwa sasa. Ajira binafsi zinaishiwa pumzi sasa lazima angaze kwenye ahueni.
Waambieni vijana hawa huku mtaani hakuna cha mwandisi, mwalimu, daktari ..wote bila bila hivyo wapunguze nyodo mana wanajikuta wanasoma masomo magumu eti wanadanganyana yana ajira

Wakati kuna waandisi wazoefu hapa jf wanatafuta ajira. ..

Maisha yamebadilika sana..

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kwa uzoefu wako unaweza kuomba hata nje ya bongo. Jaribu nchi za mashariki ya kati, hata ulaya ..utafanikiwa tu ..usiangalie sana hapa nyumbani..

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
Nimepokea ushauri Mkuu, nitaufanyia kazi ahsante sana. Tupeane hata kazi za kuchora ramani za nyumba binafsi kama zitapatikana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom