Naogopa kumueleza Mke wangu ukweli kwamba nilichepuka

Hziyech22

JF-Expert Member
Jun 8, 2019
13,576
18,894
Habari Wana Jf wenzangu

Kuna jambo limenikuta Jana, wakati wa mida saa 4 napita kutokea kwenye mishe zangu pembezoni mwa bar moja hivi maarufu hapa Dar nikaitwa na rafiki mmoja hivi wa kike ambaye sikuonana nae muda kidogo nikaenda tukaa pale.

Binafsi sio mnywaji wa pombe tofauti na huyo dada yeye anapenda tukapiga story kazaa baada ya pale sikumbuki kilichoendelea nimejikuta nipo ghetto la huyo dada wakati nimemka leo asubuhi Tena nikiwa nipo uchi hata huyo dada hivyo hivyo.

Kwa mazingira hayo nivyoyaona sikutaka hata nimuulize je tumefanya mapenzi maana sikumbuki chochote kikichotokea kwanini nimekuwa na wasiwasi huyu demu mafaili yake nayajua ana list ndefu Sana na ameshawahi kudate na wasanii wawili maarufu wa hapa Bongo ambao wanajulikana kabisa kwakugonga Sana mademu.

Ukiachana na Hilo me nina mtu wangu ambaye ninaishi nae kama mke na Mume ninampenda Sana, ananiheshimu na mimi namuheshimu,ni mtu muhimu Sana kwenye maisha yangu yeye ni kama kiungo kwenye chakula.

Sijawahi kuchepuka wala sijawahi kufikiria hicho kitu kwa namna navyompenda mtu wangu nimeamka nimekuta missed call 4 zake kwenye simu yangu.

Ndugu zangu ninashindwa sijui nitamuambiaje mtu wangu na je nikimwambia ukweli ulivyo atanielewa kwa sababu binafsi sijadhamiria kufanya hivyo na sijui kilitokea kitu gani kikatokea hicho kitu.Naombeni ushauri wenu ndugu zangu nimwambie nini mke wangu anielewe.

to yeye
Zero IQ
Yna2
financial services
Darmian
Mzigua90
Carleen
Joanah
Amehlo
DeepPond
Watu8
joseph1989
Numbisa
Shunie
Usher-smith MD
Bujibuji Simba Nyanaume
Saint Anne

NB: Naomba tusiweke masiala kwenye issue sensitive kama unataka kufanya hivyo Bora tu usicomment kabisa kwenye uzi wangu nipo serious
 
Mchukue huyo dada mpeleke kituo cha afya mpime afya kisha uanze PEP kukuzuia usipate HIV ikiwa huyu dada anao.

Ila mtihani sasa ukiwa unatumia hizo dawa inabidi usikutane kimwili na mke wako mpaka dozi iishe. Sijui utapata namna gani ya kumwambia.
 
Hapo cha kukushauri fanya mchakato wa kupima VVU. Kama ana list ndefu uwezi jua afya yake...kwa sasa hakuna umuhimu wa kumtaarifu mpenzi wako, maana anaweza kukwazika au kujikuta anapata hasira.
 
Aise we jamaa ni mdhaifu. Kwa hiyo unataka kutuaminisha kwamba alikuwekea kilevi umefika getho kwake ukiwa haujitambui au? Kama ndivyo, uliwezaje kusimamisha? Ongea ukweli ili usaidiwe.

Halafu liwe funzo, siku nyingine usikubali wito wa marafiki usio na mpango nao.
 
Aise we jamaa ni mdhaifu. Kwa hiyo unataka kutuaminisha kwamba alikuwekea kilevi umefika getho kwake ukiwa haujitambui au? Kama ndivyo, uliwezaje kusimamisha? Ongea ukweli ili usaidiwe.
Halafu liwe funzo, siku nyingine usikubali wito wa marafiki usio na mpango nao.
Mzee baba sikumbuki chochote kikichotokea huo ndio ukweli naomba ushauri wako nifanye nini?
 
Mchukue huyo dada mpeleke kituo cha afya mpime afya kisha uanze PEP kukuzuia usipate HIV ikiwa huyu dada anao.

Ila mtihani sasa ukiwa unatumia hizo dawa inabidi usikutane kimwili na mke wako mpaka dozi iishe. Sijui utapata namna gani ya kumwambia.
Ushauri wako ni mzuri Asante Sana ila utekelezaji wake ni mgumu
 
Kwanza kanunue PEP anza kubwia maana huyo dada kupima itakua shughuli au kama unaweza kwenda nae kupima nenda naye.

Hapa inabidi umchote mwambie ume enjoy sana na ungependa muendeleze ila kwa sharti la kupima. Usimuonyeshe kukasirika wala nini....

Mpenzi wako usimwambie chochote we tafuta mbinu za kijasusi umdanganye. Sema hata ulimezwa na samaki kama Yona na ukatapikwa ila usithubutu kufungua bakuli lako la uoga...

Anyway!! How old are you?
 
giphy.gif
 
Kuwa mpole...pengine joto lilikuwa kali akaona akupunguze nguo tu upate hewa safi
 
Nawaambiaga vijana "pombe sio mikato kabisa".
Anyways......
Kwanza nikupongeze kwa kupata free "nunu"..😋 which is not easy...😉
Alafu ebu punguza kulalamika mkuu, yaani misused calls 4 ndio unakuja kunaomba ushauri..🤔 Wenzako wanapataga miss calls hadi 50 na sim wanazima alafu the next day wanaenda duka la madawa wananunua gozz na kujizungushia kichwani kana kwamba walipigwa ngeta...😂
 
Back
Top Bottom