Naogopa kuitwa M'MBEA

Rafiki yangu alifunga ndoa miezi miwili iliyopita na mchumba wake wa siku nyingi.
Kutokana na ukali wa foleni huwa ninakuwepo maeneo ya mjini nikipata moja baridi, moja vuguvugu na nyingine moto.

Kila siku huwa namuona huyu shemeji yangu akiwana na kasharobaro kamoja kenye kuvaa milegezo huku wakinyweshana pombe, denda kidogo na kutomasana kwa fujo.

Natamani kumwambia mumewe licha ya kuwa naumia moyoni.
Najua nikimwambia mumewe nitaharibu uhusiano wao, na siku wakipatana wataniita M'MBEA.

JE NIFANYEJE?

Mhhhhhhhhhhh! Kumbe wapo wanaume wanaoumia kwa kuona vya watu vinaliwa! Binafsi huwa hii tabia sina, nikiona huwa napotezea ila huwa najitahidi mhusika asinione isije jamaa yake akajua kwa njia zake mwenyewe akahisi mie ndo niliyotoa siri.
 
Buji, kama kweli huyo ni rafiki wa ukweli, tafuta line mpya mtumie meseji inayoeleweka, mda wanaokutana, jina sahihi la mahali wanapokutana nk. Hakikisha maelezo yako yanaeleweka vizuri, ukihakikisha msg imemfikia tupa hiyo line. Utakuwa umemsaidia mno. Kumbuka kutuma wakati ambao huyo mdada hana uwezekano wa kuwa karibu na simu ya mumewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom