Nanunua nguo kila ninapokutana na machinga hata kama sizihitaji, nifanyeje kuondokana na tabia hii?

Nani mwingine ana zoea kama la kwangu la kununua nguo kila unapoletewa na mtembezaji. Nikikaa home naona nimejaza sana nguo hata ambazo sizivai masanduku Kwa makabati Mpaka chumba kinageuka kero kinanuka nguo(mitumba hasa +dukani).

Kila nikitaka kuzigawa nashindwa nianzie wapi ama nimpe nani na hata kama nikimpa mhitaji siku moja moja awe mnywaji mwenzangu au mzoa taka basi nitaishia kumchagulia dosho kadhaa moja au mbili na sio nguo kali ya fashion zile nzuri zinazoita ingawa sizivai hata mwaka mzima.

Kugawa imekuwa ni kama nataka, sitaki maana kuna kipindi unachafua nguo zote zile code za kwendA ila bado unakuwa na mzigo wa akiba still unatoka nazo Safi kwenye mishe.

Sasa cha ajabu najua Nina nguo kibao ila bado Nikikaa bar au kitaa ikaletwa nguo naiona kazi nzuri hii lazima nilipe hela.

Hii sijui tunaita ulafi, uchoyo au roho mbaya au ubinafsi Kwa maana akili Kiukweli inataman jambo moja niwe na nguo chache ila nzuri na mambo yataenda tu fresh mfano form six zako kali 5,jeans na cardet 10 kali, t shirt 5, boxer 10 kali.

Inakuwa imeisha Sasa Mara makanzu kibao, makoti kibao, ma suruali ya mwaka juzi, mashati ya 2021. Chumba kinatia Mpaka uvivu kupumzika Kwa utuli.
Ahaaa we mkuu vaa tu maana walio wengi habari nguo alizovaaa mwingine
 
Sasa job unaenda na hizo kadeti 2 na Suruali 2 na mashati 4 pekee?
.mashati hayo ni wiki moja, wiki inayofuata unarudia tena hizo hizo?

Sioni shida kurudia nguo mkuu.
Hizo nguo ni nyingi mno. Ni ishu ya mpangilio tuu.
Hapo kuna Tsheti, kuna mashati ya mikono mirefu na mikono mifupi. Suruali ya kadeti 2 na kitambaa mbili. Jeans utavaa siku ya Casual
 
Bora wewe rafiki, mwenzio nikikaa bar kila kitu cha kula kikipita ninacho ndiyo maana toka nianze kulewa sina kumbukumbu siku gani sijaondoka bar tumbo likiunguruma kama mashine ya mahindi .😭
Ila weye wapunguzie wahitaji na punguza tamaa ya mavazi utakufa utayaacha
 
Back
Top Bottom