Sijui ingekuaje kama ningepiga zile namba walizonipa wale Freemason wa Kiswedish

Clepatina

JF-Expert Member
Apr 8, 2023
1,268
2,554
Shikamoo /Mambo.

Kwa mnaofuatilia story yangu ya YULE MZEE ALIHARIBU MAISHA YA MABINTI WENGI ILA YA KWANGU ALIYAHARIBU NA KUYATENGENEZA MWENYEWE ep. 4 niliandika nilivyoenda Ulaya kwa mara ya kwanza ila nikashindwa maisha ya kule nikarudi zangu.

Ilikua ni Sweden na ilikua January ambapo winter inakua kileleni na kwa sbb ya baridi nilikua sitoki nje na kwa sababu ilikua giza usiku na mchana nilikua nalala mpaka saa nane mchana ila wenyewe walikua wanaamka asubuhi wanaenda huko kwenye mishe zao na huo muda mim ninaoamka kuanza siku wenyeji wanakua washaanza kazi ya pili. Kule watu wana kazi hata tatu au nne.

Ilipofika April jua likawa linatoka na siku moja nikachungulia nje nakuona jua ni kali na ghafla nikapata mood ya kwenda kuzurura mjini.

Nilipoona jua nikiwa ndani nilidhan baridi sio kali nikavaa koti jepesi na sikuvaa gloves ila nilipokua mjini katika kunyoosha miguu baridi ikanizidia na nikaamua nitafute sehemu niingie mwili upate joto.

Nikiwa sijui mtaa niliko unaitwaje nikaingia kwenye jengo ambalo kwa nje lilionekana la kawaida tu kama majengo mengine na nilipofika kwenye entrance floor nikaegemea ukutan nikachukua simu yangu nikaingia facebook nikapost tupicha kadhaa vya kiwaringishia wala vumbi😜(Mi pia mla vumbi msipaniki).

Nikiwa pale nazuga na fb ili mwili upate joto ghafla nywele vinyweleo vikanisisimka na roho ikawa kama inatapatapa na then kukawa kama kuna kitu kinaniambia nigeuke nyuma yangu niangalie.

Nilipogeuka nikaona ngazi nzuri ajabu zimejengwa kifahari sana zinaelekeo huko juu lakini pia nikashangaa kwanini macho yangu hayakuziona zile nhazi wakati naingia pale wakati ziko wazi tu na zilipokaa ilipaswa iwe kitu cha kwanza macho kuona wakati naingia pale?

Mwanzoni mwa ngazi zile kwa juu ukutani kulikua na kibao kizuri cha bati la material kama.dhahabu inang'aa kimeandikwa neno la ki Swedish FRIMURARNA yaani freemason au secrety society kikiwa na mshale unaoelekeza juu ya zile ngazi ila kwa vile nilikua sijui ki swedish sikua najua lile neno linamaanisha nini.

Hakika uzuri wa zile ngazi ulifanya nitamani nipande nikaone zinakoishia lkn kulikua na sauti ndani yangu iliyoniambia niondoke pale.

Niliamua kuondoka lakini nikiwa nakaribia kuufikia mlango nilioingilia kutokea mitaani ghafla nikahisi kama macho yangu yameona mtu akinichungulia katika kona kule juu ya zile ngazi.

Nikarudi kinyume nyume kuhakikisha lakini nilipofika pale kabla sijaelekeza macho yangu kutizama nikajisikia kizunguzungu na kudondoka na wakati ninadondoka nikahisi kama nimeona mgongo wa mtu unaishia na kutokomea huko juu ila haikua clear picture ni kama nilikua na mawenge hivi.

Nikasimama na ghafla ndani yangu kukawa na sauti mbili zikiongea. Moja inanishawishi nipande zile ngazi nikachungulie na nyingine inaniambia niondoke pale ila mwishowe niliamua kupanda nikachungulie kule juu.

Nikapanda na kufika kwenye mlango mzuri wa mbao wenye naksi kama ile milango ya Zanzibar ila sikuweza kuingia maana sikuwa na card/ password yakufungulia ule mlango ila nikawa nasikia sauti kama ya watu wanaoimba nyimbo kama za kanisani sio kanisani za kama ibada ila sio ibada bali kitu kama hicho na katikati ya hizo nyimbo ilisikika sauti ya mtu anayeongea kama mtu asiye timamu kichwani.

Ghafla nilisikia mtu akinigusa bega na nilivyogeuka alikua ni msichana mrembo wa kiswedish aliyeniangalia huku akitabasamu. Nikasogea pembeni kumpisha akachanja kadi yake mlango ukafunguka na akaingia ndani lakini muda wote alikua akiniangalia huku akinipa tabasamu la kirafiki lakini pia alifungua mlango na kuufunga huku akihakikisha sipati upenyo wa kuangalia kule ndani.

Alivyoingia tu na mim nikageuka na kuanza kushuka zile ngazi ili niondoke zangu ila nilipofika pale kwenye ile kona nilipohisi kulikua na mtu akinichungulia ghafla moyo wangu ukapatwa na huzuni kisha nikajiona sina haja ya kuendelea kuishi na hivyo nikatamani nijirushe kwenye zile ngazi nidondoke kule chini kwenye entrance floor nife nipumzike na mateso ya dunia lakini ile sauti iliyokua ikiniambia niondoke ikaniambia nisali.

Kwa wakati ule nilikua sijaokoka na walokole nilikua nawaona ni vichaa mapunguan na nilikua sisali nikila wala nikilala wala wakati wowote.

Mama yangu alikua muislam na babu yangu alikua muislam safi na aliniita Yusra ila bahati mbaya sikuwa najua kuswali kwa dini ya babu yangu na kwa baba yangu nilikua mkristo ila tulikua wakristo jina so sikujua nasali vipi ila kwa vile nilishasikia mara nyingi walokole wakisali hivyo sala rahisi kwangu kwa wakati ule ilikua ni kuwaiga walokole kwa kusema tu KATIKA JINA LA YESU.

Nilijikuta nayarudia hayo maneno zaidi ya mara elfu mpaka nikaanza ku vibrate na mbio nikashuka zile ngazi na kutoka nje na kutokomea central na kuingia kwenye mall fulani na huko nikawa naingia kwenye maduka kushangaa shangaa lkn wakati naingia kwenye moja ya duka nikapishana na mwanaume ambae alidondosha kikadi kisha akaingia kwenye zile gari za kubebea maiti.

Nikaokota kile kikadi na haraka nikampelekea kabla gari ile haijaondoka ila nikashangaa akakataa kile kikadi kisha akatabasamu na ile gari ikaondoka. Niliposoma kile kikadi ilikua ni businesscard ya FRIMURARNA. Nikakitupa huku najiuliza maswali na kuendelea zangu kuzurura.

Nikiwa kwenye duka moja la nguo wakati naelekea chumba cha kujaribia nguo nikashangaa kukutana tena na yule msichana wa kiswedish aliyenitabasamulia pale kwenye ule mlango wao kule kwenye zile ngazi. Huku akiwa anatabasamu kirafiki akagusa koti nililovaa kisha akasema "rangi ya koti yako ni nzuri na inaendana na rangi nzuri ya ngozi yako".

Kwa mshangao na woga sikuweza hata kusema asante na yeye huku akitabasamu akatokomea zake.

Nilipofika home wakati navua lile koti nikahisi kitu mfukoni. Kutoa kuangalia ni businesscard kama ile aliyodondosha yule mwanaume aliyeingia kwenye gari ya kubebea maiti.

Sikujua imeingiaje kwenye koti langu ila nilihisi ni yule msichana wa kizungu aliiweka alipogusa koti langu kulisifia.

Nikaenda mpaka kwa mwenyeji wangu aliyekua sebuleni na bwan ake wa ki nigeria wakinywa wine na kuwaonyesha ile kadi na kisha nikawauliza ni cha nini?

Yule mtanzania ambae ndie nilikua naishi nae na yeye hakua anajua ni kadi ya nini ila yule mnigeria alivyoisoma tu akasimama kisha huku akitoa macho akasema
"Who gave you dis?!"

Ikabidi niwaelezee kila kitu kisha nikivyomaliza yule mnigeria akasema
"Do you want to be veeeeery veeeeeery rich!?" Nikamwambia ndio. Akasema"Hii kadi ina thamani kuliko vitu vyote tunavyomiliki sisi wote watatu hapa kisha akatuelezea kuwa hao ni kama freemason na wanachama wake ni watu wazito tu na hakuna popote unapoweza kwenda kuomba kujiunga nao bali wao wenyewe waku recomend na akashangaa kwanini wahangaike kunipa mawasiliano yao wakati mimi ni kapuku tu?

Yule mnigeria alikua na furaha sana na ile kadi na kila saa alikua anaiangalia angalia kama vile haamini kweli ni yenyewe origino na nilipomwambia sitaki kuwapigia akasema haina shida atawapigia yeye kisha akaiweka mezani karibu na glass yake ya wine na kisha akachukua chupa kwa lengo la kuongeza wine kwenye glass yake ila kwa bahati mbaya ile wine ikamwagikia kwenye ile kadi na ile wine ilivyotua tu kwenye ile kadi maandishi yote kwenye ile kadi yakafutika na ikabaki nyeupe pee kama karatasi tu ya kawaida.

Mnigeria akachanganyikiwa. Akaniomba nimuelekeze nilipotupa kile kikadi cha kwanza. Nikamuelekeza ila hakukikuta.

Hata hivyo mpaka leo huwa najiuliza;
JE INGEKUAJE IWAPO NINGEPIGA ZILE NAMBA.

JE wangenitoa kafara?

Je wangenifanya mmoja wao na kunipa utajiri?

Natamani sana kujua ila nadhani mpaka siku nakufa sitapata jibu.

JOANNA Gily Half american Equation x Watu8 mshamba_hachekwi Analyse Binadamu Mtakatifu
 
Shikamoo /Mambo.

Kwa mnaofuatilia story yangu ya YULE MZEE ALIHARIBU MAISHA YA MABINTI WENGI ILA YA KWANGU ALIYAHARIBU NA KUYATENGENEZA MWENYEWE ep. 4 niliandika nilivyoenda Ulaya kwa mara ya kwanza ila nikashindwa maisha ya kule nikarudi zangu.

Ilikua ni Sweden na ilikua January ambapo winter inakua kileleni na kwa sbb ya baridi nilikua sitoki nje na kwa sababu ilikua giza usiku na mchana nilikua nalala mpaka saa nane mchana ila wenyewe walikua wanaamka asubuhi wanaenda huko kwenye mishe zao na huo muda mim ninaoamka kuanza siku wenyeji wanakua washaanza kazi ya pili. Kule watu wana kazi hata tatu au nne.

Ilipofika April jua likawa linatoka na siku moja nikachungulia nje nakuona jua ni kali na ghafla nikapata mood ya kwenda kuzurura mjini.

Nilipoona jua nikiwa ndani nilidhan baridi sio kali nikavaa koti jepesi na sikuvaa gloves ila nilipokua mjini katika kunyoosha miguu baridi ikanizidia na nikaamua nitafute sehemu niingie mwili upate joto.

Nikiwa sijui mtaa niliko unaitwaje nikaingia kwenye jengo ambalo kwa nje lilionekana la kawaida tu kama majengo mengine na nilipofika kwenye entrance floor nikaegemea ukutan nikachukua simu yangu nikaingia facebook nikapost tupicha kadhaa vya kiwaringishia wala vumbi(Mi pia mla vumbi msipaniki).

Brotherhood fraternity HAWANA hayo wasemayo walokole na wasiotafakari wengine......

#YetzerHatov
 
Waafrika walio masikini wa akili wanadanganywa/kudanganyika sana.....mtu anakataa FREEMASON kwa kuihusisha na "ibada za ajabu" lakini anapokea MAFUTA ya maombezi.....anakwenda kwa waganga/wanajimu ili AWE NA MVUTO/AONGEZE NYOTA AOE/AOLEWE ili APATE AJIRA.....ili APANDE CHEO....ili ASIFUKUZWE KAZI....ili nyumba yake isifuatwe na maadui wakiwemo WANGA....ili amcontrol mume/asiibiwe/amuibe wa mwenzake.....biashara yake itoke/saluni ijae wateja/auze sahani nyingi mama lishe.....everyone is aspiring of success though success ain't have a clear cut....iwe umebebwa/umetoa papuchi/umependelewa....hakuna atakayekueleza siri ya mafanikio yake p ya kupigiwa mfano na wengine eti tu ni JUHUDI za kushinda kwake juani na kukesha gizani ,eti tu ni kujibana kwake matumizi kwa kushindia mihogo 3 ya kukaanga eti kunywa vikombe vya kahawa na kashata tu eti ni kukataa anasa tu.....

WATOTO WETU TUSIWARITHISHE UJINGA WA KUYAONA MAISHA WAMEUMBIWA WATU WEUPE TU AMA WALE WANAOISHI KIZUNGU TU....

Natafakari hivi kweli bila ya KUTUMIA UTUMWA(ubaya) UKOLONI(ubaya),DINI ,UKOLONI MAMBOLEO....hivi hao ulaya wangekuwa na maendeleo na maisha hayo tunayoyaona ni ya thamani sana?!!!!

Wao WAMEISOMA NA KUITAFAKARI DUNIA sana......

Nijuavyo mimi hakuna SIRI KUBWA YA MAFANIKIO zaidi ya kutuliza akili....KUCHELEWA KULALA(hutokaa idle tu) na KUWAHI KUAMKA(hutodamka na kukaa idle tu).....mengine ni mbwembwe tu.....

Ni kweli mkuu.
Mafanikio yanahitaji akili.
 
Back
Top Bottom