Nanunua ngozi za Mbuzi na Kondoo !!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nanunua ngozi za Mbuzi na Kondoo !!!

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by fardia, Apr 17, 2012.

 1. f

  fardia Member

  #1
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nanunua ngozi mbichi za Mbuzi au Kondoo zilizotunzwa kwa kupakwa chumvi (Wet Salted) kuanzia ngozi 10,000 na kuendelea tafadhali tuwasiliane kwa simu namba 0659890000 au uni-PM. Ngozi zisiwe na mikato (Cuts), mashimo (Holes) au kuharibika (Red Heat/Over stay). Asanteni.
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu hiyo qunatity unayo itaka ni kubwa sana, na ukizingatia kwamba ni lazima mtu aunge unge kuzipata hizo ngozi na si dhani kama kuna kiwanda cha mbuzi huku,
   
 3. f

  fardia Member

  #3
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu. Nimejaribu kuongea na hao watu wapunguze hiyo minimum yao wamekataa. Kwani wanahitaji ngozi nyingi sana. Nikaona ngoja liilete kwa wanajamii huenda kuna mtu anaweza kufanikisha hilo.
   
 4. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #4
  Apr 17, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,129
  Trophy Points: 280
  Mkuu hichi kiwango si rahisi ukipate, na labuda zingekuwa kavu, kwa mbichi kuzipata ni vigumu sana,
   
 5. f

  fardia Member

  #5
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwa kavu wanatoa bei mbaya sana, haifai kabisa. Ila nimeongea nao tena, wamesema kwa Dar es Salaam wanaweza kuchukua 5,000 lakini kwa mikoani inatakiwa ziwe 10,000 au zaidi kwani chini ya hapo usafiri utawakata.
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Apr 17, 2012
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  Hao jamaa ni wageni hapa nchini? kwa ubora huo sio rahisi kupata kwa kiwango hicho. Mbuzi wengi wanafikishwa Dar wanakuwa na chapa za moto mbavuni,na wale wasio na chapa ni mpaka uende vijijini ndani huko. Ni zoezi gumu.
   
 7. f

  fardia Member

  #7
  Apr 17, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa ndugu yangu Malila. Hata mimi niliona kuna ugumu fulani katika kufanikisha hilo. Ila kabla sijawapa jibu la mwisho kuwa imeshindikana nikaona bora nililete hili swala hapa jamvini yawezekana kuna watu wenye kuweza kufanikisha hilo. Ila kwa hali inavyoenda naona wanajamvi pia wameona ugumu bado upo. Ngoja nivute subira kidogo kabla sijawapa jibu kuwa imeshindikana.
   
 8. a

  akrb Senior Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 103
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  wananunua kwa bei gani ???
   
 9. f

  fardia Member

  #9
  Apr 18, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kati ya 1,500 hadi 2,500 kutegemea na ubora wa ngozi zako. Na mzigo tunaufata mahali popote ulipo Tanzania.
   
Loading...