Nani yupo sahihi: Magufuli vs Lissu

Nani yupo sahihi: Magufuli vs Lissu

Doh lakini hawa wazungu ni noma. Pamoja na maelezo mazuri yote, yaani kutoka madai ya kamati za maprofessor wetu wapendwa ya Matrilion na hata madai ya TRA ya Trilion 400, eti leo tunaambulia $300m? This is not fair. Sasa Makinikia yanaachiwa hivi hivi tu?

Tuwe tunaacha kukurupuka, dunia ilitucheka na mabili yetu sasa watatuzodoa kwa tulichopata.
 
Ndiyo ni maoni yako. Lakini mbona umehitimisha tu hujajenga hoja?
Kwani mpaka sasa tumepata nini? Hiyo dola milioni 300, kipindi chote uzalishaji uliposimama, tumepoteza kiasi gani kupitia kodi, uwekezaji, michango ya kwenye mifuko ya kijamii, mishahara ya wafanyakazi waliofukuzwa, na zaidi Tanzania kuonekana ni mahali hatari kwa mitaji ya nje?

Leo hii kati ya kampuni 160 zilizokuwa zikifanya utafiti zimesimama. Wafanyakazi wameachishwa kazi, kodi mbalimbali hazipo. Pesa zilizokuwa kwenye mzunguko kutokana na mapato ya wafanyakazi, hazipo tena. Makampuni yote yaliyowekeza Tanzania yamepotea thamani kwenye share markets kwa 30 - 60%. Unaelewa hiyo pesa iliyopotea ni kiasi gani? Una uhakika gani makampuni haya yatarudi tena Tanzania kuendelea na utafiti (kumbuka serikali haina uwezo na haiwezi kufanya utafiti)? Bila utafiti hakuna sustainability ya industry.

Hivi unafahamu kuwa hiyo 50/50 haina maana yoyote kwenye biashara ya madini? Unajua kuwa tuna 50% mgodi wa Mwadui lakini hatupati chochote? Unafahamu kuwa faida kubwa kwenye biashara ya madini haitegemei moja kwa moja mauzo ya madini?

Baada ya miaka mitatu hivi, turudi kujadili faida zilizopatikana kutokana na mabadiliko haya. Ongezeko la mapato litatokana na ongezeko la mrabaha kutoka 4% mpaka 7% lakini siyo kutokana na 50/50. Hata hiyo 7% itaongezeka kutoka kwenye operations zilizopo lakini itasababisha anguko kwenye utafiti na new developments.

Tulisema toka mwanzo Barrick kama kuna hela watatoa haitafikia hata bilioni 1, tukaonekana wajinga. Lakini leo ukweli umedhihiri. Tulisema taarifa ya Mruma ilikuwa ya uwongo, leo imedhihirika, Acacia hawakukutwa na hatia yoyote ya kukwepa kodi au kutoa taarifa za uwongo juu ya dhahabu iliyopo kwenye concentrates.

Nchi ni yetu sote. Kila mmoja ana cha kuchangia. Wapo wanaodhani Tanzania ni ya kwao zaidi kuliko wengine. Wote ni Watanzania, wote tunaitakia mema nchi yetu. Tatizo wengine wanajenga nyumba hewani, wengine tunajua kuwa nyumba ni lazima iwe na msingi jliojengwa ardhini.

Mkuu kutoka zero ha 50/50 si jambo dogo, ila kuhusu faida ipo kwenye mrabaha nadhani wataalam watakuwa wameliona hilo na sina hakika kama halipo kwenye maboresho, lakini pia nimesikiliza hiyo taarifa ya Prof. nimeona kuna maboresho mengi yatakaowafaidisha watanzania kuanzia ajira za juu, mazingira ya kuishi na zabuni mbalimbali zitaelekezwa kwa wazawa....
Kuhusu kurrudishiwa hela hilo nilikuwa nalijua na ndiyo maana sikuiweka kwenye faida tarajiwa, refund iliwekwa kama njia ya kuwalegeza Barrick wapoteze concentration kwenye kuboresha mkataba kwenda kwenye win win situation....

Kuhusu tafiti ni kwamba sasa TZ inashare so itakuwa rahisi kuinfuence vitu tunavyotaka kwenye managment ya barick, na hiyo taasisi mpya ya kusimamia madini itakuwa ni chachu ya kufanya maboresho coz tuna post 3 kubwa...Issue ni dhamira ya dhati.....

Na kuhusu misingi ya nchi, nadhani huu ndiyo msingi mkubwa unaojengwa kwenye udhibiti wa rasilimali zetu.....
 
Doh lakini hawa wazungu ni noma. Pamoja na maelezo mazuri yote, yaani kutoka madai ya kamati za maprofessor wetu wapendwa ya Matrilion na hata madai ya TRA ya Trilion 400, eti leo tunaambulia $300m? This is not fair. Sasa Makinikia yanaachiwa hivi hivi tu?

Tuwe tunaacha kukurupuka, dunia ilitucheka na mabili yetu sasa watatuzodoa kwa tulichopata.
ni upuuzi wa kiwango cha malumumbazi
 
Lis ni mnafiki, ni bora mbow alifanya kazi yake ingawa hakuifanya vizuri sana ya kumtwanga risasi huyu mnafiki

Angekuwa mnafiki wangemkamata na unafiki wake na kumfunga........
Lakini hatuwa ilyochukuliwa dhidi yake historia inaonyesha ni hatua zinazochukuliwa kwa mashujaa na watu wenye uzalendo na wapenda haki na usawa...........
 
kwa uchambuzi huu subiria matusi yako kutoka ba-vicha

Kwaiyo we unaona kachambua hapo??

Bora angekaa na Mme wake wacheze kidali poo kaandika utumbo kachanganya na matapishi

Bunge kina kazi gani??
 
Kama acacia wangesajiwa kisheria, wangekuwa na nguvu ga kwenda mahakamani kama sheria za mikataba zinavyosema. Jambo ambalo limewafanya acacia kuwa daifu, kwani kama wangekwenda mahakamani wasingeshinda kesi kwani hawakusajiliwa. Lissu alikuwa sahihi kwa mujibu wa sheria za makataba zinavyosema, yeye lissu hakujuwa kuwa acacia haikusajiliwa kwani hakuwahi kuiona hiyo mikataba .Magu aliingia kichwakichwa tu kwani na yeye hakulijuwa hilo la kutosajiliwa kwa acacia , hiyo ni bahati kwake. Hivyo basi Lissu alikuwa sahihi zaidi. NA ndio maana wapinzani wanapiga kelele kila siku kwa mijataba iwe wazi. Isiwe ni malibya rais.
 
Kwenye hili la madini weakness zote zilikuwa zinajulikana na watu wengi kupitia hoja za Lissu kwa miaka mingi, na ikapelekea bunge kuunda kamati ambayo iliambulia mabadiliko madogo sana kwali walikuwa wanadiscuss na Baririck huku wakiwa comfortable na wakawa wanauwezo wa kufanya ulaghai wa kuhonga na kadhalika....
So kikubwa ilikuwa ni approch ipi itumike? approach ya kwanza(kamati ya Bomani/Zitto) haikuleta tija, kwahiyo JPM kaja na approach ya kutengeneza mgogoro wenye mchanganyiko wa evidence za uongo na za ukweli lengo siyo kurudishiwa fedha bali ilikuwa kupata stahiki sawa kama nchi, na hili anaelekea kufanikiwa...........

So Lissu alitaka kuaznia bungeni then kwenda kwa Barrick na migodi mingine, lakini JPM ameanzia kwenye migodi- Barrick akaenda bungeni then akarudi Barrick na kwenye migodi mingine...

Kwahiyo kwenye huu mjadala wa makinikia ili TZ inufaike haikuhitaji sana njia ya kisheria, ilikuwa ni kutafuta Best Approach ambayo ndiyo JPM alikoweza kufanikiwa kwa mpaka sasa.......
 
Mkuu kutoka zero ha 50/50 si jambo dogo, ila kuhusu faida ipo kwenye mrabaha nadhani wataalam watakuwa wameliona hilo na sina hakika kama halipo kwenye maboresho, lakini pia nimesikiliza hiyo taarifa ya Prof. nimeona kuna maboresho mengi yatakaowafaidisha watanzania kuanzia ajira za juu, mazingira ya kuishi na zabuni mbalimbali zitaelekezwa kwa wazawa....
Kuhusu kurrudishiwa hela hilo nilikuwa nalijua na ndiyo maana sikuiweka kwenye faida tarajiwa, refund iliwekwa kama njia ya kuwalegeza Barrick wapoteze concentration kwenye kuboresha mkataba kwenda kwenye win win situation....

Kuhusu tafiti ni kwamba sasa TZ inashare so itakuwa rahisi kuinfuence vitu tunavyotaka kwenye managment ya barick, na hiyo taasisi mpya ya kusimamia madini itakuwa ni chachu ya kufanya maboresho coz tuna post 3 kubwa...Issue ni dhamira ya dhati.....

Na kuhusu misingi ya nchi, nadhani huu ndiyo msingi mkubwa unaojengwa kwenye udhibiti wa rasilimali zetu.....
Hiyo 50/50 wala siyo umiliki bali mgao. Umiliki wetu ni 16%. Hiyo 50/50 ni baada ya kuondoa costs of production, royalty, taxes zote na dividents. Bulyanhulu haijawahi kupata faida kwa miaka mingi. Sasa hiyo 50/50 itasaidia nini? Itabakia kuwa faraja ya moyo lakini siyo mapato.

Kuishi nje ya mgodi inamsaidia mwajiri kupunguza gharama haimsaidii mfanyakazi. Wakati nafanya kazi Barrick, walikuja na hilo pendekezo, wakatoa na vivutio vya kukaa nje ya mgodi, tulio wengi tulikataa kwa sababu ukikaa huko nje utajighramia mambo mengi mwenyewe wakati expatriates wakipata kila kitu free ndani ya mgodi. Ukikaa nje na familia yako, utakuwa na likizo moja tu kwa mwaka. Wakati ukikaa mgodini, unapata likizo ya wiki 2 kila baada ya wiki 6 ili ukakae na famikia yako. Sasa naona Barrick wamefanikiwa kwa kupitia serikali.

Kuhusu nafasi za uongozi, hiyo imekuwepo wakati wote. Sasa hivi kuna watanzania wengi kwenye nafasi za juu. Hata mgodi wa Buzwagi Manager ni mswahili.

Kwa ujumla, haya mambo yaliyotajwa yanaonekana kama mapya kwa wasiojua lakini yamekuwepo kama sehemu ya sera ya madini ya mwaka 2010. Mambo ya local procurement, social responsibility yamekuwepo wakati wote.
 
Nakubaliana na wewe, hizo weakness zote zimeonekana kupitia kamati na naamini wamejipanga kukabiliana nazo kimfumo, na ushahidi ni uu udhubutu aliounyosha JPM mpaka hapo alipoa fika, Je ni kweli kwenye hili la madini unaeza mlinganisha na Mkapa na JK kwenye uthubutu na uwezo wa kusimamia unachokiami? huko nyuma ufujaji ulikuwa wa kiwango cha juu coz ma-Raisi walipita walikuwa part ya wezi, kwa hiyo hilo la JPM kutojiunga nao ni nusu ya vita Tz imeshashinda......

Kuhusu makazi ni uhuru na faragha ya mwanadamu ni muhimu kuliko kitu chochote na inajenga kisaikolojia na kuongeza ufanisi na amani....
 
Pia mahali ambapo makampuni yanatumia fursa ya 'tax avoidance' kugawana 50/50 pia kunaweza kutufanya tusifaidi sana. Jambo la msingi ambalo lingetusaidia zaidi na zaidi ni kuboresha sheria zetu na kuondoa legal loopholes zinazosababisha 'tax avoidance' na hata kama kutakuwa na makubaliano mazuri kama hayakuwekwa kisheria ni rahisi sana kugeukwa na hivyo kukosa mahali pa kuegemea. Sijui kwa nini tunaogopa kuboresha sheria zetu, tukianza na katiba yetu ili tuweze kulinda raslimali zetu kwa maneno na matendo.
 
Nakubaliana na wewe, hizo weakness zote zimeonekana kupitia kamati na naamini wamejipanga kukabiliana nazo kimfumo, na ushahidi ni uu udhubutu aliounyosha JPM mpaka hapo alipoa fika, Je ni kweli kwenye hili la madini unaeza mlinganisha na Mkapa na JK kwenye uthubutu na uwezo wa kusimamia unachokiami? huko nyuma ufujaji ulikuwa wa kiwango cha juu coz ma-Raisi walipita walikuwa part ya wezi, kwa hiyo hilo la JPM kutojiunga nao ni nusu ya vita Tz imeshashinda......

Kuhusu makazi ni uhuru na faragha ya mwanadamu ni muhimu kuliko kitu chochote na inajenga kisaikolojia na kuongeza ufanisi na amani....

Kama utaratibu wa kupitisha sheria zetu utabaki ule ule wa siku zote, legal loopholes zitakuwepo tu siku zote. Inabidi sasa tuanze kuona hoja zenye nguvu na hata kama zinaungwa mkono na wachache, kuliko kufuata wingi wa supporters hata kama hoja ni dhaifu. Ili kufanya hili liwezekane inabidi tuondokane na ile dhana ya kujua tu kusoma na kuandika na tuanze kuchagua wawakilishi wetu - wenye sifa za uongozi pamoja na uwezo wa kujadili hoja kwa kina, kuzisimamia na ushawishi.
 
Dah Lissu majamaa yanakili kwamba Magufuli kalambishwa biscuit hana uwezo wa kupambana na wanaume wa barrick
 
Nakubaliana na wewe, hizo weakness zote zimeonekana kupitia kamati na naamini wamejipanga kukabiliana nazo kimfumo, na ushahidi ni uu udhubutu aliounyosha JPM mpaka hapo alipoa fika, Je ni kweli kwenye hili la madini unaeza mlinganisha na Mkapa na JK kwenye uthubutu na uwezo wa kusimamia unachokiami? huko nyuma ufujaji ulikuwa wa kiwango cha juu coz ma-Raisi walipita walikuwa part ya wezi, kwa hiyo hilo la JPM kutojiunga nao ni nusu ya vita Tz imeshashinda......

Kuhusu makazi ni uhuru na faragha ya mwanadamu ni muhimu kuliko kitu chochote na inajenga kisaikolojia na kuongeza ufanisi na amani....
Mimi siafiki kabisa kuwa Mkapa na Kikwete walikuwa ni sehemu ya wezi. Kwani kwenye haya majadiliano kuna wizi wowote uliodhihirika?

Mimi nimekuwepo kwenye sekta hii kwa zaidi ya miaka 20 nikifanya kazi Tanzania, nchi nyingine za Afrika na mabara ya nje. Kwa dhamira ya moyo wangu kabisa, naamini hakuna mtu aliyefanya kazi kubwa kwenye sekta ya madini zaidi ya Mkapa. Kilichotia doa kwa Mkapa ni kutaka kununua mgodi wa makaa ya mawe. Lakini nje ya hilo, alifanya kazi kubwa sana kuifanya sekta hii iweze kuanza baada ya kufa kwa miaka mingi. Ujue kuwa hakuna mwekezaji aliyekuwa anataka kuja kuwekeza kwenye madini ya Tanzania kutokana na historia mbaya ya Tanzania ya kutaifisha migodi mwaka 1967.

Watanzania wengi hawajui. Lakini hakika, hakuna aliyefanya kazi kubwa zaidi ya Mkapa, hakuna hata mmoja.
 
Sorry nilikua pasipojulikana hivyo cjui chochote, kwani kuna nini kimetokea? Noah yangu zipo?
 
Wabunge wenyewe kina Lema, Mdee, Bulaya wanaovuta bangi? Wanafaham nini kuhusu madini, uchumi na mikataba? Bungeni ili Zitto na yule Mgonjwa wajazwe mapesa ili wawateteee? Hapana Magufuli umefanya mapinduzi na utakumbukwa daima najua ni swala la muda mbona Kikwete walimshangilia na kumuona mtukufu?
 
Back
Top Bottom