Nani yupo sahihi: Magufuli vs Lissu

Kuna mtu kakomenti kwenye uzi fulani anasema eti"toka kuahidiwa noah hadi kuambulia mirinda nyeusi mojamoja
 
Acacia wanagawa hela tu coz wanajua kuna watu wanashida. Lkn hawajaona wapi wanadaiwa. Angalia mtu anatoa 0.002% ya teh, wanautan sana hawa
 
Uchambuzi Wangu wa Tarehe 12 June, 2017 Ndani ya JF

Hatua zilizochukuliwa
1. Hatua ya Magufuli kusitisha mchanga kwenda nje kwa ajili ya uchunguzi ni sahihi.
2. Report ya kwanza na Mapendekezo yake ni sahihi.
3. Report ya pili na Mapendekezo yake ni sahihi pia.

Mkakati ya Team Magufuli
Hatua zote tatu ni sahihi kwasababu alichofanya Magufuli sio kuvunja mkataba au kuzuia moja kwa moja usafilishaji wa mchanga bali ni strategy za kuwafanya ACACIA warudi kwenye meza ya majadiliano wakiwa hawana confidence kwa kudai share kubwa ukilinganisha kama wangeitwa bila Magufuli kutengeneza Cheos, kwahiyo uundaji wa tume zote mbili pamoja na ya Tatu ambayo alisema yeye mwenyewe haijui ni mpango mkakati wa kutengeneza room nzuri ya negotiation ili apate faida kama nilivyoanisha hapo chini.
Kumbukeni kamati ya bunge ilishawahi kupitia sera na mikataba ya madini wakaishia kuambulia mabadiliko madogo sana.

Faida ya kutengeneza mtafaruku

1.Magufuli atakuwa na evidence ya uwizi wanaofanya wakati wa majadiliano mapya

2. Magufuli atakuwa anajua na ataenda na share anayoitaka kuidai kwenye meza ya majadiliano

3. Hata kama ACACIA wanabebwa na baadhi ya vipengele kwenye mkataba, watakuwa hawana confidence ya kudai share kubwa kutokana na Guilty Consciousness baada ya kuvuliwa taulo.

4.Magufuli atakuwa na room ya kudai share nyingi hadi kwenye pure gold mbali na makinikia

5.Magufuli atapata room kubwa ya kureview mikataba ya madini na gas kama ambavyo ameshaagiza kwasababu wawekezaji watamuona yuko serious tofauti na waliopita.

6.Kulingana na mazingira na ukweli uliojulikana, ni ngumu kwa ACACIA kwenda mahakamani, watataka hili swala liishie mezani. Kwahiyo habari ya ACACIA kwenda mahakamani sahauni.

Toafuti ya Magufuli na Lissu kimkakati

1.Magufuli aliamua kutengeneza mgogoro ili apate faida nilizo hainisha hapo juu na zitampa faida-Best Approach.

2.Lissu alitaka tuilete mikataba bungeni kwa ajili ya marekebisho, akaiponda aproach ya Magufuli-Weak Approach

Kwanini Magufuli yuko sahihi

Mikataba itakavyorudishwa bungeni kujadiliwa JPM atakuwa na evidence, na watajadili kulingana na evidence na Loop holes zilizoainishwa na kamati zote.

Kwanini Lissu hayuko sahihi sana

Approach yake ingesababisha bunge kiadili mikataba Blindly bila evidence yoyote hivyo serikali kuambilia kiduchu kama kamati ya akina Zitto/Bomani

Lissu kaboa. Period!
 
Hatuja shitakiwa badala yake tumekubali kulipwa $300 million km kifuta machozi badala ya fortune of $194 Billion tumeangukia kwenye pasu kwa pasu ya 50/50 ambayo baada ya muda kidogo wana weza Fungasha vilago wakiamua Je gharama za haya majadiliano yaliyo dumu kwa zaidi ya miezi 3 na zile kamati 2 ni kiasi gani
 
Mimi siafiki kabisa kuwa Mkapa na Kikwete walikuwa ni sehemu ya wezi. Kwani kwenye haya majadiliano kuna wizi wowote uliodhihirika?

Mimi nimekuwepo kwenye sekta hii kwa zaidi ya miaka 20 nikifanya kazi Tanzania, nchi nyingine za Afrika na mabara ya nje. Kwa dhamira ya moyo wangu kabisa, naamini hakuna mtu aliyefanya kazi kubwa kwenye sekta ya madini zaidi ya Mkapa. Kilichotia doa kwa Mkapa ni kutaka kununua mgodi wa makaa ya mawe. Lakini nje ya hilo, alifanya kazi kubwa sana kuifanya sekta hii iweze kuanza baada ya kufa kwa miaka mingi. Ujue kuwa hakuna mwekezaji aliyekuwa anataka kuja kuwekeza kwenye madini ya Tanzania kutokana na historia mbaya ya Tanzania ya kutaifisha migodi mwaka 1967.

Watanzania wengi hawajui. Lakini hakika, hakuna aliyefanya kazi kubwa zaidi ya Mkapa, hakuna hata mmoja.

Taarifa ya Prof. Osorro inaonyesha kulikuwa na maamuzi ya ajaabu, kwa mfano TZ wakati mgodi unaanza tulikuwa na hisa 20%, akaja waziri mwingine zikapungua mpaka 15% akaja mwingine 5% then 0%......... kwenye hili huitaji kujiuliza sana..
N pia kwenye hotoba za JPM mara nyingi husema ameamua kusimamia rasilimali na sio kama wengine waliopita, na yeye angekuwa haipendi TZ angewaambia wampe mgao then awe anajifanya anasafiri kumbe anakwenda kuweka bank nje kama waliopita......Anatumia lugha ya staha tu...

Mkapa na kazi kubwa ni sawa...Ila ilitakiwa asomeshe wataalam kwanza then ndiyo wachimbe, hakupaswa kufanya haraka matokeo yake nchi haijanufaika chochote na madini so far.......refer JK Nyerere, madini hayaozi
Angeweza hata kuomba serikali ya South Africa ikasimamia na kutupa muelekeo kutoka mwanzo, nadhani wangekubali kulipa fadhila, ila dhamira ilikuja changanyika na wizi......

Makosa yote yaliyofanywa kwenye madini ni ya Makusudi.
 
Pia mahali ambapo makampuni yanatumia fursa ya 'tax avoidance' kugawana 50/50 pia kunaweza kutufanya tusifaidi sana. Jambo la msingi ambalo lingetusaidia zaidi na zaidi ni kuboresha sheria zetu na kuondoa legal loopholes zinazosababisha 'tax avoidance' na hata kama kutakuwa na makubaliano mazuri kama hayakuwekwa kisheria ni rahisi sana kugeukwa na hivyo kukosa mahali pa kuegemea. Sijui kwa nini tunaogopa kuboresha sheria zetu, tukianza na katiba yetu ili tuweze kulinda raslimali zetu kwa maneno na matendo.

Nadhani sheria nyingi zimebadilishwa kwenye hati ya dharula kabla ya bunge la juzi na Barrick wamekubali mabadiliko yote ya sheria nadhani Nilimsikia vizuri Prof. kabudi.
Na uanzishwaji wa taasisi ya kusimamia madini na mgawanyo wa nafasi za juu kwenye migodi pamoja na makampuni kutumia bank za ndani huenda kukawa na mabadiliko ya haraka na TZ ikaanza nufaika na madini....

Nadhani tuwe na mtazamo chanya kwenye hii atua ya sasa...........
 
Gharama zilizotumika katika shughuli yote hii ni vizuri zikawekwa wazi ili kubalnce story.Kutoka trllion 425 hadi $ 300 millions, ni dharau ya karne hii.
Hii 50/50 tunayoishangilia kama mazuzu ni pesa ambayo kama bahati nasibu kwetu, tunaweza tukaipata au tusiipate.Hawa jamaa tangia waanzishe huu mgodi wa buly hadi sekunde hii wanadai hawajawahi kupata faida.Kwa hiyo wakiendelea na kauli hiyo, maana yake ni kwamba hiyo 50/50 ni kama nightmare kwetu kama taifa.
Bado safari ya rasilimali za taifa ni ndefu sana, tuzidi kumuomba sana Mungu.
 
Taarifa ya Prof. Osorro inaonyesha kulikuwa na maamuzi ya ajaabu, kwa mfano TZ wakati mgodi unaanza tulikuwa na hisa 20%, akaja waziri mwingine zikapungua mpaka 15% akaja mwingine 5% then 0%......... kwenye hili huitaji kujiuliza sana..
N pia kwenye hotoba za JPM mara nyingi husema ameamua kusimamia rasilimali na sio kama wengine waliopita, na yeye angekuwa haipendi TZ angewaambia wampe mgao then awe anajifanya anasafiri kumbe anakwenda kuweka bank nje kama waliopita......Anatumia lugha ya staha tu...

Mkapa na kazi kubwa ni sawa...Ila ilitakiwa asomeshe wataalam kwanza then ndiyo wachimbe, hakupaswa kufanya haraka matokeo yake nchi haijanufaika chochote na madini so far.......refer JK Nyerere, madini hayaozi
Angeweza hata kuomba serikali ya South Africa ikasimamia na kutupa muelekeo kutoka mwanzo, nadhani wangekubali kulipa fadhila, ila dhamira ilikuja changanyika na wizi......

Makosa yote yaliyofanywa kwenye madini ni ya Makusudi.
Usichanganye siasa za majukwaani na ukweli. Sijui una umri gani, na sijui wakati Mkapa anaingia madarakani ulikuwa na umri gani.

Wakati Mkapa anaingia ikulu, hazina ilikuwa haina hata dola moja. Ilikuwa jambo la kawaida mfanyakazi mwezi huu wa 10 kupokea nusu mshahara wa mwezi wa 7 au wa 6. Tulikuwa hatukopesheki. Hatukuruhusiwa kupata msaada wowote wala mkopo kutoka mashirika ya fedha Duniani. Mkapa akaingia madarakani. Angefanya nini zaidi ya kukubali masharti ya walimwengu ili angalao watu waishi?

Sharti la kwanza lilikuwa ni lazima serikali ijiondoe kwenye biashara zote maana tunatumia fedha kidogo zinazopatikana kuendeshea mashirika ambayo hayaleti faida yoyote. Wakati ule hata bidhaa za Tanzania ilikuwa siyo rahisi kuzikuta madukani kutokana na uzalishaji duni kutoka kila shirika. Kama sehemu ya utekelezaji wa matakwa ya WB tuliamua kuuza hisa za serikali kwenye mradi wa Bulyanhulu kwa dola milioni 5. Pesa hiyo ilikuwa ni nyingi sana kwa mradi wa utafiti. Pesa hiyo ililipwa hazina, na Sutton resources iliyonunua hisa hizo ililalamika sana kuwa ni nyingi mno. Ikumbukwe Buly ulikuwa mradi wa utafiti, siyo mgodi.

Hizo hisa za 20% kupungua kuwa 10% mpaka 5%, ni ajabu kuona mtu anashindwa kuelewa kuwa hisa zako zinakuwa diluted kutokana na contributions zako! Hisa za 20% hazikuwa free carried shares bali zilitokana na kazi ya drilling iliyofanywa na STAMICO kabla mradi haujanunuliwa. Kadiri mradi ulivyokuwa unaendelea, sisi hatukuwa na pesa za kuchangia ndiyo maana umiliki wetu uliendelea kushuka.

Mkapa hakuona namna nyingine yoyote ya kuikwamua Tanzania zaidi ya kuruhusu uwekezaji binafsi. Lakini wawekezaji walikuwa hawataki kuja Tanzania. Alihangaika sana kuwatafuta wawekezaji kwenye sekta ya madini. Barrick walikuwa hawataki kuja Tanzania. Watu wa kati kama Andrew Young wakatumika kuwashawishi Barrick, ikishindikana. Akaombwa Bush ikashindikana. Bush akaiomba WB, ambayo ndiyo iliyowashawishi Barrick kuja Tanzania kwa kuwaahidi mkopo wa kujengea mradi wa Buly wakikubali kuja Tanzania. Tanzania ilikuwa na rekodi mbaya ya kutaifisha mali za watu binafsi na kutoheshimu mikataba. Ndiyo sababu iliyoifanya Tanzania kutopendwa na mwekezaji yeyote Duniani. Lakini pia Tanzania haikuwa na umeme. Umeme haukuwepk Buly wala Kahama, hakukuwa na barabara kwenda Buly, hakukuwa na maji, hakukuwa na simu. Barrick wakajenga njia kuu ya umeme toka Shinyanga karibia kilometer 140, wakajenga bomba la maji toka ziwa Viktoria kilometer 80 wakienda wanagawa maji kwenye vijiji vyote linakopita. Wananchi wale waliona kama muujiza.

Katika maneno ya kipuuzi kabisa ni hayo kusema tuache madini yetu mpaka tuwe na wataalam. Hao wataalam watapatikana vipi kama hawana mahali pa kujifunzia? Utajifunzia hewani. Kinachosababisha madini yachimbwe ni mtaji na siyo uwepo wa wataalam wa nchi yako. Tangu madini yaanze kuchimbwa Tanzania, leo Tanzania ni nchi ya tatu Afrika baada ya SA na Ghana kwa kuwa na wataalam waliotapakaa Duniani nzima. Tanzania ina wataalam wengi wa kiwango cha juu kuliko mataifa kama China, na wote hao wamepatikana kutokana uwepo wa migodi nchini.

Kwa kuzingatia mazingira yaliyokuwepo, hakuna mtu aliyefanya kazi kubwa kwenye uchumi wa Tanzania kama Mkapa. Maendeleo ni process, mmoja anafikia mahali fulani, mwingine ananzia pake kwenda mbele. Aliyefuatia kwa kufanya kazi kubwa kwenye sekta ya madini ni Kikwete.

Kikwete ndiye alibadili sheria ya madini ya mwaka 1998 na kuandaa ya mwaka 2010. Kwenye sheria hiyo mrabaha uliongezwa toka 3% mpaka 4%; free carried shares za serikali aliibadilisha kutoka 0% mpaka 10%. Aliandaa sera mpya ya madini ya 2009 iliyoyalazimisha makampuni yote kuwa succession plan ili watanzania wachukue nafasi za wazungu, aliyalazimisha makampuni yote kufanya procurement locally kwa kiwango siyo chini ya 45%; aliweka kiwango cha chini cha mishahara kwa wafanyakazi wa migoni kuwa juu kuliko sekta zote. Aliwalazimisha expatriates wote kulipia michango ya hifadhi ya jamii nchini.

Utofauti wa tawala mbili zilizotangulia, ya Mkapa na Kikwete, na huu wa sasa, tawala zilizopita walifanya mambo makubwa bila kelele na kwa weledi mkubwa, bila kelele nyingi na bila ya kuharibu mazingira ya uwekezaji na wala kuwatia hofu wawekezaji kama ilivyo sasa. Utawala wa sasa, jambo dogo, pengine lilihitajika kufanyika ofisini, litafanyika kwenye uwanja wa mkutano, mbele ya camaera kwa kelele nyingi sana. Wale ambao hawajui wanadhani ni jambo jipya hata kama lilikuwepo.
 
  • Thanks
Reactions: AWM

Nashukuru mkuu wa kushare experience yako na sisi, ni elimu kubwa, lakini hoja yangu waliweza kuona mbali ila walifanya makosa ya makusudi mengi, na Mkapa kitu anachojutia kwenye uongozi wake ni makosa aliyofanya kwenye sera ya madini na ubinafsishaji kwa ujumla, na tena alikuwa anaambiwa na alijibu kwa jeuri, ila mwisho wa siku alikuja kujuta kwa kinywa chake, nadhani unajua maana ya mtu mzima mwenye mamlaka kama yeye na akaondoka madarakani na kujutia jambo....

Kuhusu wataalam, nakubaliana na wewe ila sijui kama ilikuwa vingumu kuattach wataalam wetu South Africa kama fadhila kwa msaada tuliowapa....
Na je nyerere alikosea kukataa kuchimba madini mpaka apate wataalam?
All in all dhamira njema ndiyo kitu muhimu zaidi.....
 
Yawezekana Mkapa kama binadamu kuna makosa alifanya lakini sishawishiki kuwa alifanya kwa makusudi. Hata utawala wa sasa kwa muda mfupi umefanya makosa mengi. Tukiwa hai tutakuja kusikia wakati wa utawala wa mwingine. Mimi naamini kwa muda mfupi utawala wa sasa umefanya makosa mengi kuliko utawala wa Mkapa. Sasa hivi ninmapema sana kusema, hata makubaliano ya jana, na mabadiliko ya sheria, yale ni maandishi tu. Jambo la muhimu ni kungojea matokeo. Je, tutapata zaidi? Je uwekezaji utaongezeka? Mataifa mengi yanapunguza kodi kama njia ya kuongeza uwekezaji na kuongeza mapato. Sisi tunaongeza kodi ili kuongeza uwekezaji na kuongeza mapato.

Ghana wameshusha VAT mpaka 5% kwa wafanyabiashara wakubwa na 3% kwa wafanyabiashara wa kati na 0% kwa wafanyabiashara wadogo.

Dubai ndiyo inayoongoza kwa kodi ndogo, na ndiyo iliyopata maendeleo makubwa kwa muda mfupi kuliko Taifa lolote Duniani.

Mimi naamini kwa nchi kama Tanzania kwa sasa tulistahili kuweka mazingira mazuri sana ya kuvutia uwekezaji. Tunahitaji massive investment ili watu wetu waajiriwe. Tukiwa na watanzania 10m wenye ajira rasmi wanaolipa PAYE 10m kila mmoja kwa mwaka, tutapata 100 trillion. Hata tukipata kodi sifuri toka kwenye corporates tutakuwa much better kuliko tulivyo sasa.
 
Thanks!
 
Taasisi si watu ama? yaani kuna kundi la watu wanaoitwa taasisi ya Uraisi/Raisi ndiyo inashindanaga na huyu ndugu yetu...

Alichokua anaongea lisu ni mikataba mibovu ambayo tuliishangiria sana mmoja wapo Leo anatwambia tunaibiwa apo mlipokua mnapitisha hamkujua, au ao tunaowasema Leo wametuibia walituamulia tu nasisi tumewakubalia, Magufuli alikuwemo kupitisha mikataba hakujua inatunyonya amejua leo hii ,acheni kupumbazwa mkapumbazika , yaani mtu anatupa taka halafu anazizoa mnamsifu kwa kumshangilia hii itakua akili au matope
 
Nadhani sheria nyingi zimebadilishwa kwenye hati ya dharula kabla ya bunge la juzi na Barrick wamekubali mabadiliko yote ya sheria nadhani Nilimsikia vizuri Prof. kabudi.
Na uanzishwaji wa taasisi ya kusimamia madini na mgawanyo wa nafasi za juu kwenye migodi pamoja na makampuni kutumia bank za ndani huenda kukawa na mabadiliko ya haraka na TZ ikaanza nufaika na madini....

Nadhani tuwe na mtazamo chanya kwenye hii atua ya sasa...........

Kuhoji au kuwa na maoni tofauti siyo sawa na kuwa na mtazamo hasi. After all, wote ni Watz na kama ni kunufainika tutanufaika wote na ikitokea ikala kwetu itakula kwetu kwa wote pia.
 
Back
Top Bottom