Nani yupo nyuma ya kampeni ya kumchafua Chongolo?

Andre-Pierre

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
328
1,209
“Wana CCM hatuaminiani ndio maana ukiacha glass ya maji ukatoka nje ukirudi huwezi kuinywa” - Jakaya Mrisho Kikwete wa Msoga.

Nimeanza kumnukuu aliyepata kuwa mwenyekiti wa ccm, Mzee Kikwete kuhusu hali ya kutoaminiana baina ya wanachama wa chama hiko.

Huko katika mtandao wa X zamani twitter, kuna baadhi ya wadau wanamshambulia Katibu Mkuu wa CCM ndugu Daniel Chongolo kwa tuhuma mbalimbali.

Wameenda mbali zaidi wakitaka avuliwe uongozi lakini kwa tuhuma zinazoonekana za kupika.

Je, Chongolo kachokwa ndani ya Chama? Nani yupo nyuma ya mpango wa kumuondoa Chongolo kwa fitna huko chamani?
 
“Wana CCM hatuaminiani ndio maana ukiacha glass ya maji ukatoka nje ukirudi huwezi kuinywa” - Jakaya Mrisho Kikwete wa Msoga...
Akihisi amechoka au amechokwa, kwa heshima anaachia ngazi tu Kwan hata hivyo ameshafanya mengi ya kutosha kwaajili ya CCM.

Hakuna sababu ya kung'ang'ana akiona kuna watu wa ccm wanamzodoa kwasababu au bila sababu.

Ni hivyo tu..
 
Kwani chongolo ameifanyia Nini ccm hadi aonekana ni wapekee? Anaemfahamu atueleze ili tumpiganie kwa haya yanayo endelea juu yake
images (17).jpeg
 
Kweli ni Siasa za Maji taka
Kwanza kabisa ukitizama hiyo nyaraka(title ya usajili wa gari) utaona kabisa ina mapungufu mengi.

Mfano gari limeandikwa ni Jeupe, picha ya gari ni Kijivu, isitoshe muono wa mbele wa gari aina hiyo ya 2012 ni tofauti na gari pichani.

Hakuna mchawi, ila anatengenezwa.
 
“Wana CCM hatuaminiani ndio maana ukiacha glass ya maji ukatoka nje ukirudi huwezi kuinywa” - Jakaya Mrisho Kikwete wa Msoga...

Aliye nyuma ya mchezo huu wa kwanza ni Wewe

Kuendelea kuandika hapa ni kumchafua zaidi

Ni mchafu hasafishiki
 
Back
Top Bottom