Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 6,407
- 8,900
Mjadala ni kuhusu washauri wa rais,awamu zilizopita wanafahamika i mean there is transparency kwenye uteuzi wa washauri wa rais,kama unakumbuka kuna kipindi ambacho kingunge alikuwa mshauri wa rais juu ya mambo ya siasa.Uteuzi ni jambo moja lakini inapofikia mahali rais anakuja na majibu mepesi kwa maswala mazito watz inabidi tuhoji weledi wa washauri wake.Hivi watoto walalamike na baba ulalamike nani atakuwa msaada ndani ya nyumba?that house should collapse.
Mimi nimeongelea mjumuisho wa Matatizo yetu kwa ujumla, kwamba tunafikiri kwamba Bw.Kikwete au sijui Bw.Pinda ndio tatizo, kumbe sio, tatizo NI SISI Watanzania kwa ujumla wetu, yaani Utamaduni wetu, na anayoyafanya Bw.Kikwete sio mapya, na yangefanywa na Mtanzania karibu yoyote yule aliyezaliwa na kukulia TZ, kwa maana ndiyo Utamaduni wetu unavyotukuza, hivyo kutegemea kwamba kuna lolote jipya litakuja kutoka kwa Viongozi ambao wametokana na jamii hii yetu ni kujidanganya na tutasubiri mpaka Yesu atakaporudi, na huyo Kiongozi hatotokea!