Nani wanamshauri rais TZ? - Lazima tutafakari hili...

nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
3,962
2,000
..Katika nchi nyingi duniani...haswa zile zilizoendelea na ambazo nyingi tungependa kuiga mifano yao katika nyanja za kiutawala (mfano USA etc)..ni jambo la kawaida kwa marais wa nchi hizi kuwa na washauri (presidential advisors)katika nyanja mbalimbali.....mfano washauri wa kisiasa..au uchumi...au afya....au mazingira..n.k n.k....hii yote ikiwa na nia ya kumsaidia rais kuboresha maamuzi yake...ambayo ni kwa manufaa ya nchi nzima...na si chama chake au watu wake wa karibu..

Mara nyingi jopo la washauri wa rais kwa wenzetu hutoka kwenye highly professional think tanks....ambako wataalam waliobobea kwenye sekta husika hutumika na rais kumshauri.....hili wala halifanywi siri....na hamna msingi wa kulifanya siri......That said...tuje kwetu TZ...Nimeleta hii mada ili ijadiliwe (bila itikadi za watu kisiasa)kwa manufaa ya TZ...maana kupiga kelele mara nyingine kunasaidia....Kwa kweli kwa hali ilipofikia tz...kukemea ua kuhoji mambo ni lazima kabisa na ni haki ya kila mtanzania...maana hii nchi si ya chama wala mtu fulani..bali yetu wote...

Nimekua nikijiuliza sana naposikiliza hotuba za rais JK...kwa kweli mara nyingine nashindwa kupata majibu ya kwanini inakuwa hivi...Yaani kwa matatizo yaliyopo kwenye jamii ya tz sasa rais anapokuja na kuanza kutoa malalamiko kwa wananchi wake.....tena katika hali ya kuhuzunisha sana sana....wakati yeye ndie anatakiwa kuyashughulikia manung'uniko ya raia wake haingii akilini hata kidogo...Jibu pekee nililonalo ni kuwa rais JK hana washauri...na kama anao basi ni vihiyo....au washkaji wasio na uchungu na hali inavyoendelea hapa tz......

Kama sikosei...jambo la washauri wa rais kuwepo ni la msingi sana...na si siri hata kidogo katika nchi zenye maendeleo duniani....ni hapa kwetu tz pekee jambo hili wakati huu limekua siri kubwa...pasipo na msingi wowote...labda tujikumbushe tu huko nyuma...marais waliopita waliwahi kuwa na washauri kwenye mambo ya msingi kama uchumi....hata siasa.....namkumbuka mzee Mwinyi aliwahi kumtumia Prof.Lipumba kama mshauri wa uchumi....hata Nyerere alikuwa na washauri wake katika mambo fulani....na haikuwa siri....TZ ya sasa ina mabalaa chungu mzima...kuna migogoro ya kidini....matatizo ya ufisadi...siasa chafu..n.k..n.k...mambo haya yote yanahitaji umahiri mkubwa wa rais. kuyashughulikia....maana haya ni mambo ya kitaifa..na kwa maana hiyo haingili akilini hata kidogo kumwona rais anatoka hadharani na kulalamikia anaowaongoza....kama vile nchi haina kiongozi.....Kwa kweli kwa msingi huo lazima tuhoji nani wanamshauri rais nchi hii?...je wapo???na kama wapo wanafanya nini??...na kama wanafanya wajibu wao je wanasikilizwa??...kwa kweli lazima tujiulize...kwa hali ilivyo sasa TZ...

Kwa kuhitimisha..labda ifike sasa mahaliswala la rais kuwa na washauri iwekwe rasmi kwenye katiba yetu mpya...na mambo ya msingi ya kutolea ushauri kwa rais yaainishwe....yakiwemo maswala ya kisiasa....kidini....kiuchumi..kiafya..n.k..n.k..
 
ferre.g

JF-Expert Member
Mar 3, 2013
2,217
1,195
Mkubwa..washauri wakubwa ni hawa wafuatao;-1.Wasira 2.Riz one 3.salma.k 4.kinana 5.mwigulu 6.lusinde 7.mulugo 8.rweyemamu yulee msemaji wa ikulu 9.ighondu 10.ghasia 11.kombani....hawa ndo wanaharibu kichwa cha rais....maskini kikwete!
 
Galapagos

JF-Expert Member
Nov 26, 2012
252
195
Mkubwa..washauri wakubwa ni hawa wafuatao;-1.Wasira 2.Riz one 3.salma.k 4.kinana 5.mwigulu 6.lusinde 7.mulugo 8.rweyemamu yulee msemaji wa ikulu 9.ighondu 10.ghasia 11.kombani....hawa ndo wanaharibu kichwa cha rais....maskini kikwete!
Mkuu, jamaa anajifanya mbayuwayu, washauri wake wa maana aliwaona hawamfai sasa ndo kakutana na mambayuwayu wenzake, kaaazi kweli kweli.
 
Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
37,623
2,000
Kama anateua washikaji kuwa washauri wake basi hayo ndio matokeo yake.Nafikiri cha msingi ni kuwa washauri wa raisi wasiteuliwe na raisi mwenyewe bali kuwe na chombo maalum cha kufanya kazi hiyo.
 
Loy MX

JF-Expert Member
Mar 26, 2012
1,258
1,195
1. Mwigulu nchemba
2. Ramadhani ighondu
3. Wasanii wa bongo movie
4. Usalama wa taifa
 
Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
3,548
1,225
Tatizo ni kwamba unafanya makosa yaleyale ambayo siku zote tunayafanya, umetolea mfano wa Marekani kwamba tuige wanavyofanya, bila kutambua kwamba Marekani na Tanzania ni jamii 2 zenye Tamaduni 2 tofauti, hivyo linalofanyika Marekani na kuonekana kama ni kitu cha kawaida haliwezi kufanyika kwetu!

Anayoyafanya yote Bw.Kikwete ni sawa kabisa na yanaendana na Utamaduni wetu na ndio jinsi tulivyo, na Watz karibu wote ambao wamezaliwa na kukulia TZ wangefanya hivyo hivyo, kama wangepata hiyo nafasi, na ndio maana hakuna jipya ktk kwa Viongozi wetu!

Unaongelea kuhusu ushauri, we tazama maisha yetu ya kawaida tu, Je tunaweza kutatua matatizo hata madogo tu? Hata magomvi tu ya kifamilia mpaka Wazee wasafiri kutoka vijijini ndio waje watupatanishe, na wote tuko hivyo!
Je Marekani watu wako hivyo?

Jiulize ni lini mara ya mwisho ulishawahi kumshauri Mtanzania wa kawaida na akakusikiliza? Au lini mtu alikufwata akakuomba ushauri wa jambo la maana?
Mtanzania wa kawaida anajua kila kitu, yeye ni mtaalamu wa kila kitu, sasa kwa nini Bw.Kikwete awe tofauti? Kwani Bw.Kikwete ametokea wapi?
 
kapongoliso

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,329
1,500
Nawaelewa baadhi ya washauri wake kama Dr.Ndumbaro ni kipanga kweli wa mambo ya siasa na wengineo wa uchumi nk. Wanatoa ushauri lakini jamaa anategemea zaidi unajimu (nyota)badala ya wanataaluma. Halafu kuna aina ya akina Wasira wao kazi yao ni kujikomba ili kumfurahisha mkuu nao wapate ujiko wao. Wao huangalia lipi linamfurahisha mkuu ndio hujidai kumshauri hilo ili afurahi.
 
Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
51,640
2,000
Washauri wa rais huteuliwa na rais.

Hivyo rais kama anavurunda, hawezi kulaumu washauri.

Kwa sababu kawachagua yeye.

Akilaumu washauri atakuwa anavurunda mara tatu.

Kwanza kwa kuvurunda originally, whatever the issue was.

Pili kwa kuvurunda kwa kutochagua washauri makini.

Tatu kwa kulalamikia kwamba washauri wake aliowateua mwenyewe hawafai.
The buck stops with the president. Washauri hawajaomba kura kuingia Ikulu.

Tusitake kutetea upuuzi kwa kumficha rais nyuma ya kivuli cha washauri.
 
...Kiranga..issue sio kumficha rais nyuma ya kivuli cha washauri...issue ni je hivi inawezekanaje rais asimamie upuuzi..wakati (probably)ana washauri??..Ndio rais anavurunda(personally)...je inawezekanaje hili liendelee kutokea mara kwa mara??wakati ana washauri (kama kweli wapo)??..inawezekanaje watu waendelee kumwona anavurunda na wasichukue hatua??..haya ndio mambo mi najiuliza...otherwise simtetei rais...na sioni la kutetea.....
 
Issue kubwa zaidi ya yote hayo ni, mtu kama huyu kawezaje kuwa rais katika nchi ya mamilioni ya watu?

Hilo la washauri anaweza kusikiliza anayotaka tu, au anaweza kuchagua washauri kwa kujuana zaidi ya taaluma.

Tusitake kumlaumu JK tu wakati hatuna utamaduni wa meritocracy na attention to detail karibu nchi nzima.

JK kapewa urais kwa kikubwa gani alichokifanya kabla?
 
Tatu

JF-Expert Member
Oct 6, 2006
1,080

Ndugu Kiranga umenena! Watu huwa wananishangaza sana wanaposema kuwa raisi anadanganywa na washuri wake. That's nosense na upumbavu usiovumilika.

Raisi anajua kusoma na kuandika. Raisi ana macho na masikio. Kwa maana hiyo anaweza kupambanua maswala muhimu yanayowagusa wananchi na taifa kwa ujumla.

Kwa mfano, issue ya utendaji kazi na ukusanyaji mapato wa bandari. Bandari ya Dar imeoza kwa rushwa, uzembe, wizi na ubadhirifu wa mali za watu, taasisi na pia serikali. Watu na taasisi za ndani na nje wanapiga kelele na kulalamika kila siku. Wateja na nchi jirani wameishia kutumia bandari ya Mombasa.

What to do ( Solution )
Kutatua tatizo hili sio kutoa amri kwa waziri husika na wakuu wa bandari halafu yeye anaenda likizo na baada ya mwaka ndio anarudi kuulizia kama ufumbuzi umepatikana. La hasha. Cha kufanaya ni kukutata na waziri husika na viongozi wake yeye pamoja na timu yake at least once a week. Brainstorm solution and strategies on how to tackle the problems and initiate those solutions one at a time. Akifanya hivyo kwa miezi sita hadi mwaka mzima kwa idara muhimu za serikali, watanzania tutaona matunda ya nchi yetu.

Wakuu wa idara watakaoshindwa kufuatilia utekelezaji, wote wanatemwa. Tuone kama hawatafanya kazi. Simple like that. Akitenga siku moja ya wiki kwa kazi ya ufuatiliaji kama hii badala ya kusafiri na kwenda kwenye misiba kila siku, tutakuwa mbali sana. Zaidi ya hapo, kila siku tutalaumu washauri wa raisi. Na kibaya zaidi, kama hao washauri wa raisi wanamdanganya kila siku, mbona bado wako kazini? Kwa nini wasifukuzwe kazi?

We need to change.
 
..hilo swali si lako tu..kwa mtanzania anayeona madudu yanayofanyika tangu huyu jamaa alipoingia madarakani anajiuliza swali hili...Inauma kwamba amechaguliwa na watanzania hawahawa wanaopiga kelele leo..Pengine tatizo kubwa lipo pia huko kwenye michakato ya kupata wagombea urais....huko kwenye vyama..maana hakika jamii ya mtanzania kwenye hili nguvu hawana...Pengine pia kura ya mtanzania inaweza kuondoa hili...lakini bado issue iko pale pale....jamii hii inayoletewa jina la mtu kwa mtaji wa ugali na vipande vya nguo kwa siku...lini watabadilika na kutambua kuwa kura zao zinaweza kuleta mabadiliko nchini mwao?....Mi huwa nawahusu sana wakenya kwenye hili....maana mpaka kwenye grassroots wanajitambua...pamoja na matatizo yao ya ukabila...ila they are far better than Tanzanians in realizing the true meaning of their votes.....when it comes to presidential elections...
 
Tlehhema

Member
Feb 26, 2013
42
0
Tatizo ni kwamba unafanya makosa yaleyale ambayo siku zote tunayafanya, umetolea mfano wa Marekani kwamba tuige wanavyofanya, bila kutambua kwamba Marekani na Tanzania ni jamii 2 zenye Tamaduni 2 tofauti, hivyo linalofanyika Marekani na kuonekana kama ni kitu cha kawaida haliwezi kufanyika kwetu!

Anayoyafanya yote Bw.Kikwete ni sawa kabisa na yanaendana na Utamaduni wetu na ndio jinsi tulivyo, na Watz karibu wote ambao wamezaliwa na kukulia TZ wangefanya hivyo hivyo, kama wangepata hiyo nafasi, na ndio maana hakuna jipya ktk kwa Viongozi wetu!

Unaongelea kuhusu ushauri, we tazama maisha yetu ya kawaida tu, Je tunaweza kutatua matatizo hata madogo tu? Hata magomvi tu ya kifamilia mpaka Wazee wasafiri kutoka vijijini ndio waje watupatanishe, na wote tuko hivyo!
Je Marekani watu wako hivyo?

Jiulize ni lini mara ya mwisho ulishawahi kumshauri Mtanzania wa kawaida na akakusikiliza? Au lini mtu alikufwata akakuomba ushauri wa jambo la maana?
Mtanzania wa kawaida anajua kila kitu, yeye ni mtaalamu wa kila kitu, sasa kwa nini Bw.Kikwete awe tofauti? Kwani Bw.Kikwete ametokea wapi?
Khaa!maoni gani haya utamaduni unaozungumzwa hapa sio wa kikwere,kizaramo ni utamaduni wa kidemokrasia ambao Usa,uk ni founders,
 
nderingosha

JF-Expert Member
Mar 20, 2011
3,962
2,000
Ndugu Kiranga umenena! Watu huwa wananishangaza sana wanaposema kuwa raisi anadanganywa na washuri wake. That's nosense na upumbavu usiovumilika.

Raisi anajua kusoma na kuandika. Raisi ana macho na masikio. Kwa maana hiyo anaweza kupambanua maswala muhimu yanayowagusa wananchi na taifa kwa ujumla.

Kwa mfano, issue ya utendaji kazi na ukusanyaji mapato wa bandari. Bandari ya Dar imeoza kwa rushwa, uzembe, wizi na ubadhirifu wa mali za watu, taasisi na pia serikali. Watu na taasisi za ndani na nje wanapiga kelele na kulalamika kila siku. Wateja na nchi jirani wameishia kutumia bandari ya Mombasa.

What to do ( Solution )
Kutatua tatizo hili sio kutoa amri kwa waziri husika na wakuu wa bandari halafu yeye anaenda likizo na baada ya mwaka ndio anarudi kuulizia kama ufumbuzi umepatikana. La hasha. Cha kufanaya ni kukutata na waziri husika na viongozi wake yeye pamoja na timu yake at least once a week. Brainstorm solution and strategies on how to tackle the problems and initiate those solutions one at a time. Akifanya hivyo kwa miezi sita hadi mwaka mzima kwa idara muhimu za serikali, watanzania tutaona matunda ya nchi yetu.

Wakuu wa idara watakaoshindwa kufuatilia utekelezaji, wote wanatemwa. Tuone kama hawatafanya kazi. Simple like that. Akitenga siku moja ya wiki kwa kazi ya ufuatiliaji kama hii badala ya kusafiri na kwenda kwenye misiba kila siku, tutakuwa mbali sana. Zaidi ya hapo, kila siku tutalaumu washauri wa raisi. Na kibaya zaidi, kama hao washauri wa raisi wanamdanganya kila siku, mbona bado wako kazini? Kwa nini wasifukuzwe kazi?

We need to change.
ukihoji utendaji wa rais utaambiwa rais si mtu pekee(personally)bali ni taasisi....kwa maana hiyo dhana ya rais kushauriwa iko pale pale..haiepukiki...upende usipende...wengine watakwambia rais hawezi kujua kila kitu kinachotokea TZ...na ndio maana ana wawakilishi kila sehemu(including mawaziri)....all these people are there to work on behalf of the president...pamoja na kwamba yeye ndie mwenye final say ofcourse....
 
Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
3,548
1,225
Khaa!maoni gani haya utamaduni unaozungumzwa hapa sio wa kikwere,kizaramo ni utamaduni wa kidemokrasia ambao Usa,uk ni founders,
Kwanza Marekani wala Waingereza sio waanzilishi wa Demokrasia!

Pili nilichomaanisha ni kwamba huwezi kuiga 1-1 bila kwanza kuangalia Utamaduni wako ukoje! Kwa kifupi kinachowezekana Marekani kinaweza kikashindikana kabisa Tanzania kwa maana ya utofauti wa Utamaduni wa jamii hizo mbili!
 
Tlehhema

Member
Feb 26, 2013
42
0
Ndugu Kiranga umenena! Watu huwa wananishangaza sana wanaposema kuwa raisi anadanganywa na washuri wake. That's nosense na upumbavu usiovumilika.

Raisi anajua kusoma na kuandika. Raisi ana macho na masikio. Kwa maana hiyo anaweza kupambanua maswala muhimu yanayowagusa wananchi na taifa kwa ujumla.

Kwa mfano, issue ya utendaji kazi na ukusanyaji mapato wa bandari. Bandari ya Dar imeoza kwa rushwa, uzembe, wizi na ubadhirifu wa mali za watu, taasisi na pia serikali. Watu na taasisi za ndani na nje wanapiga kelele na kulalamika kila siku. Wateja na nchi jirani wameishia kutumia bandari ya Mombasa.

What to do ( Solution )
Kutatua tatizo hili sio kutoa amri kwa waziri husika na wakuu wa bandari halafu yeye anaenda likizo na baada ya mwaka ndio anarudi kuulizia kama ufumbuzi umepatikana. La hasha. Cha kufanaya ni kukutata na waziri husika na viongozi wake yeye pamoja na timu yake at least once a week. Brainstorm solution and strategies on how to tackle the problems and initiate those solutions one at a time. Akifanya hivyo kwa miezi sita hadi mwaka mzima kwa idara muhimu za serikali, watanzania tutaona matunda ya nchi yetu.

Wakuu wa idara watakaoshindwa kufuatilia utekelezaji, wote wanatemwa. Tuone kama hawatafanya kazi. Simple like that. Akitenga siku moja ya wiki kwa kazi ya ufuatiliaji kama hii badala ya kusafiri na kwenda kwenye misiba kila siku, tutakuwa mbali sana. Zaidi ya hapo, kila siku tutalaumu washauri wa raisi. Na kibaya zaidi, kama hao washauri wa raisi wanamdanganya kila siku, mbona bado wako kazini? Kwa nini wasifukuzwe kazi?

We need to change.
Kula like mkuu umenena vema inshort rais ni dhaifu,legelege na kateua washauri wadhaifu na legelege.
 
Mjadala ni kuhusu washauri wa rais,awamu zilizopita wanafahamika i mean there is transparency kwenye uteuzi wa washauri wa rais,kama unakumbuka kuna kipindi ambacho kingunge alikuwa mshauri wa rais juu ya mambo ya siasa.Uteuzi ni jambo moja lakini inapofikia mahali rais anakuja na majibu mepesi kwa maswala mazito watz inabidi tuhoji weledi wa washauri wake.Hivi watoto walalamike na baba ulalamike nani atakuwa msaada ndani ya nyumba?that house should collapse.
 
Top Bottom