nani walikuwa ma partners wenu?

nani walikuwa ma partners wenu?

papag

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
1,171
Reaction score
1,733
Habari Wakuu?
hii ni spesheli kwa wale waliosoma kipindi kilee change mwalimu mpaka mzee rukwa.mliofanikiwa kufika sekondari za bweni. wakati wa madisco shule zilikuwa na partners wako.naanza kwa hawa:-
mzumbe SEC=Kilakala secondary
Mazengo=Msalato secondary
....
,...Unaweza endeleza shule zingine na si Vibaya ukaweka na kumbukumbu ya mambo yaliyojiri kipindi hicho.nawakilisha
 
Milambo- tabora girls, japo tabora boys walikuwa wanaleta upinzani kwa hizi ortho directors
tukawa na spare kazima high school nao tunashare na washkaji wa pale pale
 
Dah umenikumbusha mbali, mambo ya MSA-ZENGO
 
Mtwara Girl's tulikuwa mapartner wetu ni Chidya Boyz a.k.a CHIBOSECO na COTC.
Chezea Mabebis wa enzi hizo.
Wazuri Mtwara nzima.
CC: MMAHE & snowhite & Miss Kinondoni Edna.
 
Last edited by a moderator:
Zanaki girls na Tambaza.... nimeikumbuka TAMBAZANA LOL!

Binti ungelikuwepo enzi za Wu-Tamba...wale jamaa hawakuwa na muda wa disko ila wao walikuwa wanapuliza tu...

Kuna mwaka nadhani 1993 hao jamaa walitembeza mkong'oto kwa wanafunzi na waalimu wa shule zote za msingi Da'slam
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ilboru Sec ndani ya Arumeru, sisi nakumbuka tulikuwa tunagombaniwa tu na mashule ya Moshi...Weruweru, Ashira na Kibosho ndio walikuwa wanakuja sana pale Assembly Hall kuja kutikisa nasi nyonga...

Hao wakikomaa sana basi tulikuwa tunawaalika Wamenye wa Enaboishu...kuna wakati kina Chifu na Kitemango walikuwa ni wanoko sana basi mnakuwa na disko isiyo na watoto wa kike...
 
Milambo- tabora girls, japo tabora boys walikuwa wanaleta upinzani kwa hizi ortho directors
tukawa na spare kazima high school nao tunashare na washkaji wa pale pale

hahahahaa bora umeongea ukweli mkuu maana boyzia na girlz mwee..Ila tulikuwa na mambo ya kitoto asee..mara tuwaalike tabora girls wasije!! yani ilimradi tu..afu wasipokuja roho zinatuumaaaa, tunawavizia kuwamwagia maji ya maharage..dah!!!! na vipamba vyetu vya kukodi (kwa wengine)...Kuna siku bwana t.girls walitutumia vi form one disco bwana..watu walimaindije sasa!!!!!
So far so goood!!!!!
 
Lake Sec = Bwiru girls seco
Mwanza Sec = Nganza

mmmh Mkuu lake na bwiru girls kweli labda kwa sasa hivi nakumbuka zamani ni Bwiru boys na Nsumba ndo tulikuwa na ka ushindani kwa bwiru girls!!!! Ila Nganza walikuwa wanakubali sana Bwiru wavulana!!!!!
 
mmmh Mkuu lake na bwiru girls kweli labda kwa sasa hivi nakumbuka zamani ni Bwiru boys na Nsumba ndo tulikuwa na ka ushindani kwa bwiru girls!!!!
Mpendwa wakati wetu ule Masharubaroo walikuwa waLake !! alafu bwiru gels ilibobea waPwani/Tanga .... Nsumba walikuwa vichanga bado hashakum Mkuu nisamehe... Ola la laaa okay nipahe zenu?
 
Mpendwa wakati wetu ule Masharubaroo walikuwa waLake !! alafu bwiru gels ilibobea waPwani/Tanga .... Nsumba walikuwa vichanga bado hashakum Mkuu nisamehe... Ola la laaa okay nipahe zenu?

hahahahahaa...dah nakumbuka kuna siku tuliwaalika Lake kwenye mechi wakaja pale bwiru ..dah wale jamaa si tukawafunga sasa...wakatuchenjia bwana wakatufukuzia mabwenin woote..yani unapigwa mkwara katika himaya yako...umbulula huu
 
Binti ungelikuwepo enzi za Wu-Tamba...wale jamaa hawakuwa na muda wa disko ila wao walikuwa wanapuliza tu...

Kuna mwaka nadhani 1993 hao jamaa walitembeza mkong'oto kwa wanafunzi na waalimu wa shule zote za msingi Da'slam

hahahaaa....! Sikowepo aiseee hiyo miaka ndio kwanza najifunza kusimama dede LOL!!!! Mie nimekuja cheza nao juzjuzi tu!!!!!!!

Ila nasikia Tambaza enzi hizo walikuwa wababe sana na wanaogopeka sana mpaka kwenye madaladala!!!!!!!!!!!!
 
hahahahahaa...dah nakumbuka kuna siku tuliwaalika Lake kwenye mechi wakaja pale bwiru ..dah wale jamaa si tukawafunga sasa...wakatuchenjia bwana wakatufukuzia mabwenin woote..yani unapigwa mkwara katika himaya yako...umbulula huu
Vizazi,vijana wa jijini si unawajua !....Lakini enzi zetu hazikuwa hivyo tulisasivu vibaya ! Eee mungu atusamehe nnaona haya nikijihisi ubabe niliyokuwa nao! good luck mkuu
 
hahahaaa....! Sikowepo aiseee hiyo miaka ndio kwanza najifunza kusimama dede LOL!!!! Mie nimekuja cheza nao juzjuzi tu!!!!!!!

Ila nasikia Tambaza enzi hizo walikuwa wababe sana na wanaogopeka sana mpaka kwenye madaladala!!!!!!!!!!!!

Haswaaa...hiyo wiki waliyotembeza mkong'oto ilikuwa heka heka hapa mjini maana kila mwanafunzi wa shule nyingine alikuwa anadundwa...
Since then shule ikaja kufungwa kwa muda na wale madent wakasambazwa mashule mengine...baadaye ndiyo ikafanywa kuwa A-Level tu...
 
Mtwara Girl's tulikuwa mapartner wetu ni Chidya Boyz a.k.a CHIBOSECO na COTC.
Chezea Mabebis wa enzi hizo.
Wazuri Mtwara nzima.
CC: MMAHE & snowhite & Miss Kinondoni Edna.

af wewe!
ila chidyaz walikuwa size yenu mi nilikuwa nshakuwa mzee!
wangekuwa na kaka zao wa five na six ingekuwa pooooooaaaaa!
 
Haswaaa...hiyo wiki waliyotembeza mkong'oto ilikuwa heka heka hapa mjini maana kila mwanafunzi wa shule nyingine alikuwa anadundwa...
Since then shule ikaja kufungwa kwa muda na wale madent wakasambazwa mashule mengine...baadaye ndiyo ikafanywa kuwa A-Level tu...
halafu ile alevel ya tambaza PAPER II walikuwa mabitoooooz jamani!
yani utafikir walikuwa wanachovywa kwenye pipa la ubishoo wakishavaa ziel soksi zao nyeusi!
ehehehheheh!
TAMBAZANA bana!
enzi hzo hapa AZAJANGWA pale FK(hiyo kisutu na forodhani sasa tunapiganaje vikumbo)
maskini kibasila!mwe!yani uwe na boyfriend anasoma kibasila ehehehhe sasa snowcream na fosters mtakaa saa ngapi?
 
Kitu cha TOSA na IRINGA GALS..haha nouma jamn hapo.yn wadada na sket ya orange chn white raba..hatar TOSA Hapoo kwisha habar yao.:-D:-D
 
ihungo sec na rugambwa sec yaliyojiri disco walimu kuingia kutoa mimacho wakati wa zero distance (nyimbo za blues) sasa wanafunzi wanatafuta switch ziliko wanazima taa,walimu wanapigwa upofu. siku rugambwa wakialikwa ma shule ingine kunakuwa ma beef la hatari ma vijana wa ihungo.

Ha ha ha ha ha ha ha mkuu umenikumbusha mbali sana aisee.....siku ukisia rugambwa wanaakuja kila mtu anaakuwa smart ile mbayaaaaa
 
Back
Top Bottom